Ad Code

Responsive Advertisement

UNAWEZAJE KUJENGA USHUJAA KATIKA MAFANIKIO UNAYOYATAKA?

 

SEHEMU YA TATU


Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema, kama ni hivyo basi ninafasi ya pekee sana kumshukuru Mungu kwa neema yake kuu maishani mwetu,


Naomba twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo lakini kabla hatuajenda kwenye somo ambalo nimekuandalia siku yaleo naomba tukumbushane mambo kaulimbiu yetu kuu ya mwaka huu 2021 KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA haya nimaeneo matatu muhimu sana kuyafanyia kazi, kila siku usikubali ipite bila kujifunza jambo jipya na baada ya kujifunza chukua mda kutafakari kile ulichojifunza, jiulize maswali muhimu je jambo hili linawezaje kunisaidia katika kuhimalisha mahusiano yangu au linawezaje kunisaidia kupata mafanikio makubwa maishani mwangu, je jambo hili linamsaada gani katika maisha yangu, baada ya kutafakari kwa kina nenda hatua ya tatu chukua hatua kwa yale uliyojifunza na kutafakari yale ambayo yanamsaada kwa maisha yako ya sasa na baadae. Baada ya kumaliza kukumbushana mambo haya muhimu sasa twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo,  leo tunaenda kujifunza jambo la mwisho kati ya mambo matatu yakuzingatia katika kijenga ushujaa.


3~TAFUTA WATU WAKUPAMBANA KWAAJIRI YAO. (WATU WAKUWAPAMBANIA)

Hili ni jambo la muhimu sana katika kujenga ushujaa katika mafanikio yako. Jambo la muhimu hapa nikujiuliza kuwa upambana kupata mafanikio kwaajiri ya nani? Kwanini umekubali kuteseka kiasi hicho kwaajiri ya kupata mafanikio, kipi kinachokufanya ushindwe kutulia na uwe bise kuhangaika kuhakikisha unafikia mafanikio makubwa? Majibu ya maswali haya ni muongozo mkuu kwako kwaajiri ya kupata mafanikio. Tukiendelea kujiuliza maswali muhimu katika eneo hili unaweza kujiuliza je unapambana kupata mafanikio kwaaajiri ya watoto wako au familia yako au kwasababu ya ndugu zako au kwaajiri ya jamii yako? Nivema sana ukajua kwanini unateseka kupata mafanikio? Ukubwa wa sababu ndio unaokupa kiwango kikubwa cha mafanikio na udogo wa sababu ndio unaokunyika fulsa ya wewe kuwa na mafanikio makubwa. 


Ngoja twende kwa mifano kidogo:- Mimi frank mapunda ni mwalimu, hivyo jukumu langu kubwa katika ualimu wangu nikufundisha maarifa ambayo yatakuwa na msaada mkubwa kwa jamii hivyo nimechagua kuteseka kwaajiri ya jamii ambayo naona inahitaji maarifa haya muhimu kwaajiri ya kutimiza ndoto zao, na iwapo nitashindwa kufandisha iwe kwa maandishi kama hivi au kwanjia yamafundisho ya mazungumzo huwa najihisi ninadeni kubwa sana ndani yangu, nakosa furaha na ili niweze kuirejesha furaha yangu huwa inanilazimu kumtafuta mtu mwenye changamoto ambayo mimi naweza kumfundisha na yeye akatoka kwenye hiyo changamoto basi hapo nakuwa na furaha, hapo utaona kuwa naandika na kufundisha kwaajiri ya wengine na siyo kwaajiri yangu, nimejitoa kufundisha kwaajiri ya wengine waweze kupata fursa ya kupata maarifa yakuweza kuwatoa katika sehemu moja kwenda sehemu nyingine na ndio maana siandika habari za udaku bali naandika maarifa ambayo yanaweza kuwasaidia watu kuweza kupiga hatua. Hata wewe rafiki yangu unapotaka kuwa na mafanikio makubwa unaposwa kuchagua watu ambao upo tayari kupambana kwaajiri yao kama ilivyo kwa wazazi wapo bise kupambana kwaajiri ya watoto wao wahakikishe wanakula vizuri, wanasoma vizuri na wanavaa vizuri sababu hii ndio inayowafanya wazazi wengi wawe bise na maisha ili kuhakikisha mahitaji yote yamuhimu ya watoto wao wanayatimiza vizuri. 


Hilo nijukumu ndogo sana rafiki yangu, Oooh! Najua unashangaa unasema Mr frank unasema nini hapa? Najua haujanielewa kwasababu ukifikiria juu ya jukumu kubwa la kulea familia lilivyo gumu na mimi nakwambia ni jukumu ndogo sana! Ndio narudia tena kwa mkazo hilo nijukumu ndogo sana. Ngoja nikufafanulie kidogo, hebu fikiria yani wewe Mungu alikuleta duniani kwaajiri ya familia yako tu? Yani unataka kuniambia kuwa Mungu alikuepusha na kifo kipindi upo mdogo kwaajiri ya kuja kuihudumia familia yako tu? Ahaa Aaah! Haiwezekani kabisa ya Mungu huyu alikulinda na kuepusha na mabaya yote eti uje utunze familia yako tu? Hapana yani unataka kusema wewe ndio nasema na wewe unayesoma hapa yani wewe na Mohamed dweji Mungu aliwaumba na malengo tofauti? Hapana hapo unanidanganya au unajidanganya, nachotaka kusema hapa Mungu kipindi anakuumba wewe aliona tatizo katika ulimwengu huu na katika watu aliokuwa nao alikuona wewe unayesoma hapa unauwezo mkubwa wakuja kutatua tatizo kubwa linaloikumba dunia hii, ndio maana akakuepusha kifo kipindi upo mdogo ndio maana akakuepusha na kifo kipindi ukiwa unakuwa, ndio maana akakuepusha na ugonjwa mbaya katika maisha yako, ndio maana akakuepusha na hatari kubwa ambayo ilitaka kukupata kipindi kile yote haya aliyafanya ili uje utatue tatizo kubwa la dunia yetu ya sasa, hivyo acha kufikiria kuwa wewe ulizaliwa kwaajiri ya familia yako tu hapa na anza kufikiria ukubwa wa tatizo la dunia na anza kulitatua, rafiki kwajinsi Mungu anavyokuamini na jinsi wewe ulivyoacha kufanya makubwa ambayo Mungu anategemea ufanye Mungu huyu naona unasikitika sana, hebu leo acha kumhuzunisha Mungu inuka nenda katatue tatizo la dunia, kaa chini angalia ni watu gani unachagua kupambana kwaajiri yao, kama ilivyo kwa wagunduzi na wafanyaji wa mambo mengi hapa duniani wanafanya hivyo kwaajiri yetu na sisi tufanye kwaajiri ya wengine.


Ngoja tuzame ndani kidogo, aliyegundua simu aligundua kwaajiri yetu ili kuturahisishia sisi mawasilianao ndio maana mimi na wewe tunafurahia huduma hii sana, lakini chain hii haikuishia kwa mgunduzi pekee yake bali kuna mtu mwingine akubuni usafirishaji ndio maana simu ikaweza kutufikia hadi huku tulipo sisi lakini hali halikutosha, dunia ilimwitaji mtu afungue duka na auze simu ili mimi nawewe tuweze kununua, lakini cheni bado ikaendelea kuna mwanadamu mwingine akabuni laini, namwingine akabuni vocha na mwingine akabuni barabara na wingine akabuni kibanda na mwingine akabuni biashara yenyewe, hapo ikiangalia kuna msululu wa watu ambao wamebuni vitu mbalimbali kwaajiri ya wengine hadi kuweza kutufikia mimi na wewe na tukanufaika, na wakati mwingine haihitaji hadi kubuni vitu kama wabunifu wasimu bali inahitaji kuiga tu na kufanyia maboresho kidogo ndio kuiga tu kama ilivyo wa wanafungua maduka ya simu wewe unadhani wote wanabuni biashara ya simu? Hapana kuna mtu mmoja akabuni wengine wakaiga na mwisho wa siku wote wananufaikia hivyo. 



Nini ninachotaka kusema  na wewe hapa? Ninachotaka kukwambia kuwa hata wewe bado unanafasi kubwa yakuhakikisha kuwa unakuwa mmoja ya watu wanaopambana kwaajiri ya wengine unapoona tatizo sehemu usiwe mmoja ya watazama tatizo katika hali yake ya tatizo bali angalia upande wa majibu ya hilo tatizo na hapo ndipo ilipo fursa ya wewe kufanya biashara na kufanikiwa, wewe rafiki yangu kama hauna watu wakupambana kwaajiri yako basi leo chagua na naanza na kupambana kwaajiri yao kadri unavyopambana kuleta majibu kwa watu wengi ndivyo unavyosogelea mafanikio kwa kiwango kikubwa. 


Natamani niongee namama maandazi, mama vitumbua mama kuku, mama lishe hapa ninyi ndio ninyi niliwataja hapa na wengine ambao sijawataja jueni kuwa hamkuletwa kutatua matatizo madogo ya watu wa mtaani kwenu pekee bali mliletwa kutatua tatizo la watu wengi sana hapa duniani,   siku moja nikiwa dodoma nilikutana na mama mmoja anauza vitumbua na vitumbua vyake nivitamu sana nilipokaa kuzungumza naye akanimbia yeye alizawa kwaajiri ya kuja kutengeneza vitumbua pekee na sikushangaa kusikia hivyo kwasababu mama yule hauzi vitumbua kwaajiri ya mtaa wake pekee bali anatengeneza vitumbua kwaajiri ya jiji lote la dodoma, mama huyu aliniambia anawauzia vitumbua kwenye mahoteli mengi sana katika jiji ladodoma na ameajiri watu zaidi ya mia moja kwaajiri ya kupika tu vitumbua, sasa sijuwi wewe mama vitumbua hapa barabarani,  Iseee! Kuna mambo mengi sana ya kuelezea hapa ila mda hautoshi, itoshe kusema kwamba chagua watu ambao upo tayari kupambana kwaajiri yao na jitoa kweli kweli kwaajiri yao na maisha yako yatakuwa bora sana.


Ni mimi rafiki yako

Frank mapunda

Www.nguvuyamaarifa.blospot.com

Simu:- 0758918243

0656918243

0621049901


KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU

NGUVU YA MAARIFA

SOFTCOPY 10000/=


TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU

SOFTCOPY 7000/=


JIFUNZE , TAFAKARI NA CHUKUA HATUA


Post a Comment

0 Comments

Close Menu