Ad Code

Responsive Advertisement

UMEJIANDAAJE KWAAJIRI YA KUPATA MAFANIKIO?~ SEHEMU YA KWANZA



Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri huku ukihakikisha kila siku unachukua hatua kuhakikisha unasogea karibu zaidi katika kulitimiza kusudi kuu la wewe kuja hapa dunuani ndio, hakuna mwanadamu ambaye alizaliwa kuja kuzulula hapa duniani bali kila mwanadamu aliyezaliwa ni mpango wa Mungu kuzaliwa na Mungu kipindi anakuruhusu wewe unazaliwa aliweka kusudi ndani yako ambalo ndio linalobeba maana ya maish yako hapa duniani, hongera sana kwa hilo rafiki.
Nichukue nafasi hii kwa upekee sana kumshukuru Mungu aliye mkuu kwanipa tena kibali cha mimi kuwasiliana na wewe kwa njia ya maandishi siku hii ya leo najua sio kwamba mimi nawewe tumetenda mema sana kuliko wale wengine ambao hawajapata kibari cha kuwa hai au kuwa na afya njema bali nikwaneema yake tu hivyo niwajibu wangu na wajibu wako kuitumia nafasi hii yakipekee sana kuhakikisha tunachukua hatua sahihi kuhakikisha tunaliishi ipasavyo kusudi la Mungu Kuwepo hapa duniani (chukua dakika chache za kumshukuru Mungu wetu aliye mkuu).

Bila kupoteza wakati twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo ambalo lipo kwa muundo wa swali ambalo linauliza umejiandaaje kwaaji ya kupata mafanikio? hili niswali muhimu sana kujiuliza mtu yeyote ambaye anafanya kitu kwaajiri ya kupata matokea fulani. Ipo hivi kuwa kila jambo tunalofanya kuna matokeo ambayo tumeyakusudia kuyapata sasa katika maandalizi ambayo tumeyaweka kwaajiri ya kupata hayo matokeo ndio muhimu zaidi kwasababu kama hatutakuwa na maandalizi bora basi matokeo hayo yanakosa maana ya kuwepo. Vivyo hivyo katika maisha na mafaniko kuna maandalizi muhimu ambayo yanapaswa kuwepo ili kuweza kupata hayo mafanikio na iwapo maandalizi hayo yatakosekana nasi mafanikio yetu yanakosa maana yakuitwa mafanikio. Kabla ya kuendelea mbele nizungumze kidogo kuhusu mafanikio. Mafaniko ni matokeo mazuri ya jambo fulani. Sasa katika kupata hayo matokeo mazuri ya jambo fulani kuna maandalizi ambayo yanatakiwa kuwepo ili kuweza kupata hayo ambayo yanakusudiwa kutokea.

MAANDALIZI AMBAYO YANATAKIWA KUWEKWA KWAAJIRI YA KUPATA MAFANIKIO.

1-KUWA NA MALENGO MAKUBWA JUU YA MAISHA YAKO (NDOTO YAKO).

Moja ya maandalizi muhimu ambayo yanapaswa kuwekwa kwaajiri ya kupata mafaniko makubwa ni kuweka malengo makubwa juu ya maisha yako (katika kitabu cha nguvu ya maarifa sura ya pili nimefundisha kwa undani namna ya kuweka malengo yenye sifa ya kuitwa malengo kwa maisha yako). Kumekuwa na tatizo kubwa katika kuweka malengo watu wengi hawajui kuweka malengo juu ya maisha yao, sasa kama wewe unataka kupata matokeo mazuri katika maisha yako nimuhimu kufanya maandalizo bora na moja ya maandalizi muhimu ni kuweka malengo makubwa juu ya maisha yako.

2-KUFIKIRI NAYANA.
Ninaposema kufikiri baya na ninamaanisha kufikiri kwa uwazi au kwa usahihi kuhusu jambo unalokusudia,  sasa kwakuwa lengo la somo letu ni kujiandaa kupata mafanikio basi namaanisha kufikiri kwa uwazi ili kupata picha iliyo sahihi kuhusu mafanikio unayoyahitaji. Katika kuhakikisha unajiandaa vilivyo kwaajiri ya kupata mafanikio unayoyahitaji basi unatakiwa kujua kuwa unataka kufanya nini ili kuweza kupata mafanikio unayoyataka. Lazima ufikiri bayana na uwe na majibu yanayoeleweka katika eneo hili kwasababu mafanikio sio tukio bali matokeo ambayo mtu anayapata baada ya kupitia  mchakato fulani, sasa wewe ambaye unajiandaa kwaajiri ya kuyapata hayo mafanikio nilazima ujue unatakiwa kupitia mchakato gani ili Kuweza kukuletea mafaniko unayoyahitaji. Jua unatakiwa kufanya nini ili uweze kupata mafaniko hayo unayoyahitaji.

 Sasa katika kuhakikisha unafikiri bayana kuhusu kupata mafanikio yako kuna mambo manne muhimu lazima uyazingatie

1~wewe binafsi.
Jua wewe binafsi unataka kupata mafanikio ya aina gani? Je unataka kufanikiwa kwa kiwango gani? Napia unataka kufanikiwa kupitia nini? Haya ni maswali matatu muhimu kuyajibu ili kuweza kutengeneza ramani sahihi kuhusu mafanikio yako. Tunaposema lazima ufikiri bayana kuhusu mafanikio yako basi nimuhimu kuwa na majibu sasa ambayo yataonesha aina ya mafanikio yako jinsi yatakavyo kuwa. Kume kuwa na changamoto kubwa kwa watu wengi kupenda kuwa na mafaniko makubwa lakini hawajui mafaniko yao yanatakiwa yawaje? Hivyo sipendi wewe rafiki yangu uwe kwenye kundi hilo.

Ngoja twende kwa mifano kidogo ili tuweze kuelewana vizuri zaidi na mfano huu nitajitolea mimi mwenyewe. Nikianza na swali la kwanza ambalo linauliza unataka kupata mafaniko ya aina  gani? Jibu nikwamba nataka kupata mafanikio makubwa kifedha, kiafya,  kifamilia, kiroho na kimahusiano. Haya ndio maeneo makuu ambayo naweka juhudi kubwa katika kujenga mafanikio ninayoyataka. Swali la pili linaulizwa je unataka kufanikiwa kwa kiwango gani? Jibu langu nikwamba nataka kufanikiwa kwa kiwango hiki tukianza kiafya nataka kuwa na afya bora isiyo na malazi, kiroho nataka kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wangu, kikazi nataka  kuwa na branch za kuku zenye uwezo wa kumiliki kuku laki tano katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kifamilia nataka kuwa na familia bora yenye maeleno na iliyojaa furaha na kimahusiano, nataka niwe na mahusiano bora kwa jamii. Hiki ndicho kiwango cha mafanikio yangu. Na tukija kwa swali la tatu linauliza unataka kufanikiwa kupitia nini? Jibu langu nikuwa nataka kufanikiwa kupitia ushirikiano wangu na jamii yangu katika kutekeleza majukumu yangu juu ya malengo niliyojiwekea.

Jambo la kuzingatia nikwamba kila lengo ambalo nimeliweka linamchakato wake ambao lazima niupitie ili niweze kufikia hayo mafaniko ninayoyahitaji hivyo nimuhimu sana kujua mchakato ambao natakiwa niupitie. Lakini moja ya jambo kubwa ninalotakiwa kulifahamu nikwamba siyo rahisi hata kidogo katika kufikia mafanikio hayo ninayoyahitaji hii nikutokana na ukweli kuwa kwenye kupata chochote ninachokitaka kuna changamoto zake nyingi hivyo mimi na wewe kama wasafiri wa basi hili la mafaniko basi natakiwa kufahamu kuwa nitakutana na changamoto nyingi sana hivyo sipaswi kushangaa wala kuzikimbia  hizo changamoto bali natakiwa kupambana haswa ili niweze kufikia mafanikio ninayo yahitaji. Hivyo nimuhimu kujiandaa ipaswavyo kuhusu kupata mafanikio unayoyahitaji.

Kwa leo naomba niishie hapa tutaendelea wakati ujao.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
E-mail: nguvuyamaarifa1@gmail.com
Simu: 0758918243/0656918243/0786115129

JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUSAIDIA KUPATA MAARIFA ZAIDI.

NGUVU YA MAARIFA

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE SANA KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO , MUNGU AKUBARIKI SANA.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu