Ad Code

Responsive Advertisement

JE NI KWELI UFUGAJI UNAWEZA KUNIPA MAFANIKIO MAKUBWA (UTAJIRI)



Habari rafiki yangu mpendwa? Ni matumaini yangu umekuwa na wakati mzuri sana huku ukiendelea kuchukua hatua sahihi kila siku ili kuhakikisha unasogea karibu zaidi na kusudi kubwa ambalo Mungu aliweka ndani yako, hongera sana kwa hatua kubwa unazoendelea kuchukua. Kwanafasi ya kipekee sana Tumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwakuturuhusu mimi na wewe tuweze kuwasiliana tena kwa njia hii ya maandishi, siyo kwa juhudi zetu wala uwezo wetu mimi na wewe kuweza kupata nafasi hii ya kipekee sana bali nikwaneema yake tu mimi nawewe kupata nafasi hii ya kipekee sana hivyo niwajibu wetu mkuu kuhakikisha tunachukua hatua zilizo sahihi ili kuweza kuitumia nafasi hii yakipekee sana, hakuna wakati mwingine bora wa sisi kuchukua hatua zaidi ya sasa twendeni tukafanye makubwa siku hii ya leo.


Sasa twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo ambalo limekuja kama swali linalouliza je nikweli ufugaji wa kuku unaweza kunipa mafanikio makubwa (utajiri)? hili Limekuwa swali kubwa ambalo limekuwa likiulizwa na watu wengi sana, watu wanajiuliza swali wakiwa hawana imani kama kweli kupitia ufugaji wa kuku unaweza kuwapa mafanikio makubwa. Wamekuwa na imani hii nikutokana na ukweli ambao wamekuwa wamejione wao wenyewe kupitia kwa jamii kubwa ya watu ambao wamekuwa wamewaona wakufanya ufugaji kwa mda mrefu lakini hakuna hatua kubwa ambayo wamekuwa wakipiga katika maisha yao.

Leo napenda nilijibu swali kwa uhalisia kabisa. Jibu la halaka nikweli kwamba ufugaji wa kuku unaweza kukupa mafanikio makubwa (utajiri) iwapo utaufanya ufugaji wako kibiashara na siyo kimazoea. Ninaposema kibiashara ninamaanisha kuwa unapotaka kupata mafanikio kwenye ufugaji unatakiwa kuondoa dhani uliyonayo kwamba ufugaji wa kuku ni sehemu tu ya maisha bali ufikiri kwa mapana na kuuchukulia ufugaji kuwa nisehemu yako ya kutengeneza pesa kama zilivyo biashara nyingine. Sasa ninaposema ufugaji wako ufanye kama biashara yako ninamaanisha kuwa unatakiwa uwe na malengo makubwa katika ufugaji wako. Malengo yamekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi wa kuku, wafugaji wengi wamekuwa na malengo ya hewa katika ufugaji wao na siyo malengo halisia sasa kama umekosa malengo halisia katika ufugaji wako unategemea mafanikio yatakujaje? Haiwezekani hata siku moja. Na ninaposema kuwa na malengo ninaanisha malengo yenye sifa ya kuitwa malengo kwenye kitabu cha nguvu ya maarifa kwenye ukurasa wa 15 nimeleza mambo mengi muhimu kuhusu jinsi ya kuweka malengo na sifa kuu za malengo unayoyaweka nilazima yawe SMART nitafafanua ninaposema nilazima malengo yako yawe SMART namaanisha nini?

Specific- liwe linaeleweka (nikweli unataka kufuga kuku je ni kuku gani na idadi gani) siyo usema tu nataka kufuga kuku sema aina gani ya kuku na idadi gani ya kuku, wafugaji wengi wamekuwa wanaweka malengo yaliyokosa sifa ya kuitwa malengo ndio maana wanaona ufugaji hauwezi kuwapa mafanikio.

Measurable- malengo yanayoweza kupimika. Sasa malengo mengi ya wafugaji yamekosa sifa hii utakuta mfugaji anakwambia mwaka huu natamani niwe na kuku wengi hasemi wangapi na wala hajaandika sehemu yeyote wewe unadhani kwa stahili huu utaweza kufikia mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku? Hapana haiwezekani hata kidogo.

Attainable-inayoweza kupatikana, ni lazima kuweka malengo ambayo yanaweza kupatikana au kufikika hiii ni jambo la muhimu sana katika kuweza kufukia mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku. Nikweli unatakiwa kuwa na malengo makubwa lakini siyo kwamba uweke malengo ambayo hauna uwezo wa kuyafikia mfano mtu anamalengo ya kufuga kuku laki moja alafu leo anaweka lengo la kufuga kuku laki moja ndani ya mwezi mmoja wati huo hata eneo hauna mmmh huu ni uongo mkubwa sana nimuhimu kuweka malengo ambayo yanaweza kufikika nikweli kufuga kuku laki moja inawezekana basi katakata lengo hilo kwa vipindi huenda lengo la kufika idadi hiyo ndani ya miaka kumi basi ligawe katika vipande vidogo vidogo.

Reality- linaloenda sambamba na hali halisi. Ndio utaweza kufikia mafanikio makubwa iwapo umeweka malengo yako katika uhalisia, sasa wafugaji wengi wanashindwa kufikia mafanikio makubwa katika ufugaji wao kwasababu malengo yao yamekosa uhalisia wa kuitwa malengo. Unakuta mtu anakwambia nataka kufuga kuku kwa mafanikio makubwa wakati huo huo hajishughurishi kabisa na ufugaji wa kuku au anafuga lakini unaona kabisa hana mpango wa kukua kibiashara katika ufugaji.

Tangible-malengo yanaonekana. Hapa mtu unaweka malengo na kuyafanyia kazi na ikaonekana lakini sivyo wanavyofanya wafugaji, wafugaji wengi unawaona kabisa wanafanya ufugaji kimazoea sana alafu wanategemea mafaniko makubwa hata sijui hayo mafanikio hayo yatatoka wapi?

Hebu leo anza kuweka malengo sahihi kuhusu ufugaji wako na yafanyie kazi hayo malengo uliyonayo katika ufugaji wa kuku, Kwenye kitabu kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku ukurasa wa 113 nimefundisha kwa undani kanuni kadhaa za jinsi ya kufanikiwa katika ufugaji wa kuku, jipatie nakala yako ujufunze kwa undani kanuni hizo zitakusaidia sana.

Najua kweli hauna mtaji mkubwa lakini hiyo siyo sababu ya wewe kushindwa kutimiza malengo yako ya kufanikiwa katika ufugaji wa kuku bali unachotakiwa kupata maarifa sahihi ambayo yatakufanya ufanikiwe zaidi katika ufugaji wa kuku. Katika ukurasa huo ambao nimeutaja hapo juu ambao unapatikana ndani ya kitabu hicho kuna sura nzima ambayo nimeitenga kwaajiri ya kukuonyesha jinsi ambavyo utaweza kufikia mafanikio makubwa.


Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
E-mail: nguvuyamaarifa1@gmail.com
Simu:0758918243/0656918243/0786115129
Kwa ushauri wa kina kuhusiana na ufugaji wa kuku tuwasiliane kwa namba hizo.

JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUONGEZEA MAARIFA ZAIDI KATIKA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

NGUVU YA MAARIFA

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI👏 MUNGU APATE KUKUBARIKI SANA.

Post a Comment

1 Comments

  1. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)


    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete

Close Menu