Ad Code

Responsive Advertisement

MAMBO HAYA YANAMCHANGO MKUBWA KATIKA KULETA UTAJIRI(MAFANIKIO MAKUBWA) KWA MTU YEYOTE YULE JE' UPO TAYARI?






Habari rafiki yangu mpendwa ni mtumaini yangu umekuwa na siku bora sana huku ukiendelea kuchukua hatua sahihi ambazo zinaenda kukusogeza karibu zaidi na mafanikio yako, hongera sana kwa hilo.

Sasa twende moja kwa moja kwenye somo la leo  ambalo linasema mambo haya yanamchango mkubwa katika kuleta utajiri (mafanikio makubwa) kwa mtu yeyote yule je upo tayari? najua unajiuliza kwamba utajiri maana yake nini? Ngoja nikupe maana ya utajiri kwanza ndipo tusonge mbele na somo hili muhimu sana kwa mtu yeyote ambaye anahitaji mafanikio makubwa.


Kwa mujibu ya kamusi ya kiswahili toleo la tatu la mwaka 2012 linatoa tafsiri ya tajiri ni kuwa na mali nyingi hivyo ukileta kweye maana ya utajiri utapata maana hii kuwa utajiri ni kuwa na mali nyingi. Sasa katika Masha yetu sisi waanadamu hakuna mwanadamu ambaye  anapenda kuwa na mali chache au kuwa maskini ila huwa  inatokea tu kutokana na kushindwa kufikia viwango hivyo kutokana na kutokujua mambo ambayo yanaweza kutupeleka kwenye huo utajiri, sasa leo tunaenda kujifunza baadhi ya mambo ambayo yanamchango mkubwa katika kuleta mafanikio makubwa. Mambo haya nimejifunza  kwa kina katika Biblia takatifu hasa katika kile kitabu cha Methali 21:5;17. Hebu twende pamoja.

Jambo la kwanza tunaanza kuliona katika kitabu cha methali 21:5 linasema "5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji." Mwisho wa kunuu. Hapa tunajifunza jambo moja muhimu sana ambalo linavipengele viwili. Chakwanza Biblia inatuambia mawazo, cha pili inatuambia bidii hivi ni vitu muhimu sana kwa kila msafiri wa basi hili linaloelekea kwenye utajiri/mafanikio anatakiwa kuwa nayo. Ngoja tuchambue neno moja baada ya lingine kwa ufupi.

Mawazo maana yake ni dhana au fikra zilizopo kwenye akili ya mtu. Hapa utaona kuna umuhimu mkubwa kuwa na fikra sahihi ambazo zitakufanya uwe na maisha ya aina fulani sasa kwa mujibu wa somo letu la leo linatuambia mawazo ya mtu mwenye bidii inaana kwamba mtu huyu anakuwa na fikra chanya ndani yake kuhusu utajiri fikra hizo ndizo zinazomfanya aweke bidii kuhakikisha anatimiza malengo yake, swali la kujiuliza wewe rafiki umekuwa na fikra gani katika maisha yako kuhusu utajiri/mafanikio hili ni jambo muhimu sana katika kuleta kile unachokihitaji katika maisha yako hauwezi kupata kitu ambacho kinapingana na akili yako, hivyo kitu cha kwanza kabla ya kuweka juhudi katika kikiendea kile unachokihitaji ni kuandaa fikra zako katika hali nzuri juu ya jambo unalolihitaji maisha mwako, hii ni kutokana na nguvu kubwa zilizopo ndani ya fikra zako kwenye kitabu cha nguvu ya maarifa ukurasa ule wa 55 nimelifundisha hili kwa kina sana ambapo nimeelezea ni kwanamna gani unaweza ukaziandaa fikra zako kaulekea mafanikio makubwa (unaweza kujipatia kitabu hicho ili uweze kunufaika zaidi katika kutengeneza fikra sahihi kuhusu maisha na mafanikio yako)

 Vile vile bidii maana yake ni ari ya kufanya jambo kwa jitihada, hima(haraka),  kasi juhudi  na hamasa. Tukiludi kwenye pointi yetu kuu inayosema "mawazo ya mtu mwenye bidii huelekea utajiri" utakuja kugundua kuwa mtu huyu kwanza anafikra chanya katika akili yake lakini hajaishia hapo kuwa na fikra chanya bali ameongeza kitu cha pili muhimu sana ambacho ni bidii katika kutenda kwake, hivi ni vitu muhimu muhimu sana katika maisha yetu.

Hebu leo kaa chini tafakari mawazo yako je nimawazo ya aina gani yaliyopo ndani yako hapo ni muhimu sana kuondoa mawazo yote mabaya kuhusu mafanikio na utajiri kama kweli unataka kufanikiwa, hili ni jambo la muhimu sana kwasababu hauwezi kufanya kitu kinyume na fikra ulizonazo na kitu hicho kikaleta mafanikio, kitu cha kwanza kabla ya yote nikuwa na fikra safi kuhusiana na kile unachohitaji kukifanya. Pia leo hebu jiulize unahitaji kuweka bidii kiasi gani ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayoyahitaji, hili ni jambo la muhimu sana katika kuleta mafanikio ya mtu yeyote duniani, hakuna kitu ambacho kinatokea bila kuwekewa bidii, hivyo chukua mda kutafakari mambo haya mawili na anza kuyafanyia kazi mala moja naamini maisha yako hayatabaki kama yalivyo.

Hilo lilikuwa jambo la kwanza lakini jambo la pili ambalo tunalipa katika kitabu cha Methali 21:17 linasema "17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri." Hapa tunapata pointi yetu muhimu sana ambayo inaenda kutusogeza karibu zaidi na mafanikio makubwa (utajiri) nikutokupenda anasa, najua unajiuliza anasa ni kitu gani? Ngoja nikueleze kidogo maana ya Anasa, Anasa ni mambo au hali ya starehe na raha nyingi au kitu chenye thamani kubwa lakini siyo muhimu. Baada ya kuona maana anasa utakuja kugundua kuwa watu wengi tumekuwa tukishindwa kufanikiwa kwasababu tumekuwa tukipenda kufanya vitu vya  starehe ambavyo havina umuhimu wowote hiki nikitu kibaya sana kwa mtu mwenye nia ya kufikia utajiri (mafanikio makubwa) kwenye kitabu cha nguvu ya maarifa katika ukurasa ule wa 152 kipengele cha pili ambacho kinaelezea kanuni kuu za mafanikio na moja ya kanuni inasema thibiti matumizi yako  nimechambua kwa undani zaidi kuhusu aina ya matumizi ambayo nimeeleza aina kuu tatu za matumizi (jipatie nakala yako ili uweze kunufaika zaidi) hivyo nimuhimu sana kujua matumizi yako muhimu ni yapi na matumizi yako ya anasa ni yapi baada ya kujua hivyo weka kipaombele kwenye matumizi yote muhimu na epuka matumizi yote ya anasa na ambayo yatakusababishia kushindwa kufikia mafanikio makubwa.

Hatua ya kuchukua leo hii
-anza kuiandaa akili yako katika kupata mafanikio unayoyataka na amini inawezekana.
-jenga tabia ya kujifunza mambo yenye manufaa kwaajiri ya mafanikio yako.
-kuwa na mtazamo chanya kuhusu mafanikio na utajiri.
-weka bidii katika kufanyia kazi mawazo yako chanya kuelekea mafanikio makubwa.
-fanya tathmini kuhusu matumizi yako ya kila siku na zingatia jambo hili muhimu sana kuepuka kufanya matumizi ya anasa.

Fanyia kazi maarifa haya na maisha yako yatakuwa bora sana.

Ni mimi rafiki yako
Frank Mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Email: nguvuyamaarifa1@gmail.com
Simu: 0758918243/0656918243/0786115129/0621132794


KWA MAARIFA ZAIDI KARIBU UJIPATIE VITABU 

NGUVU YA MAARIFA
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI HONGERA SANA.....!

NAKUTAKIA UCHUKUAJI WA HATUA NJEMA.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu