Habari za siku rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu umekuwa na wakati mzuri sana katika kuhakikisha unachukua hatua ambazo zinaenda kukufikisha karibu zaidi na malengo yako makubwa ya maisha, sina shaka nawewe rafiki yangu kuhusu hilo nimatumaini yangu kuwa unajua kusudi kubwa la wewe kuwa hapa duniani pia umeweka malengo kuhakikisha unafikia malengo hayo.
Sasa twende moja kwa moja kwenye somo kuu la leo linalouliza kwanini ufugaji wa kuku hili niswali muhimu sana la kujiuliza kwanini ufugaji wakuku,
huenda hata wewe utakuwa unajiuliza kwanini frank unapenda kuzungumzia sana ufugaji wa kuku nasiyo vinginevyo. Hakuna ubishi kuwa kwasasa secta ya ufugaji imekuwa ikukua kwa kasi sana hapa nchini na ufugaji wa kuku umekuwa ukiongoza katika secta hii ya ufugaji hii nikutokana na manufaa makubwa yaliyopo katika ufugaji wa kuku. Ikiwa ni pamoja na uhitaji mkubwa wa nyama na mayai kuwa mkubwa kwasasa hapa nchini. Kutokana na uhitaji huu kuwa mkubwa kwa nyama na mayai yakuku kumeongeza fursa kwa watanzania wengi kunufaika na ufugaji huu wa kuku hivyo kufanya uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kukua kwa kasi, hakuna ubishi kwamba kwasasa ufugaji wa kuku umekuwa ni moja ya secta inayoajiri idadi kubwa sana ya watu hapa nchini kuanzia wafugaji, madalali, wafanyakazi na wafanya biashara wa mazao yakuku, hii imekuwa fursa kubwa sana kwasasa.
Hivyo unapozungumza ufugaji jua kuwa unazungumza secta kubwa hapa nchini ambayo inamsaada mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, hata wewe unaweza kuufanya ufugaji kuwa sehemu ya uwekezaji ambao utakupa manufaa makubwa kwa maisha yako,
Uzuri wa ufugaji wa kuku ni kwamba unaweza kuufanya ukiwa hata kama unamtaji mdogo bado unaweza kufanya uwekezaji huu, pia unaweza kuufanya hata kama hauna mda mwingi yaani inakuhitaji dakika sitini hadi tisini tu kwa siku kuweza kuwahudia kuku wako. Yaani ni saa moja hadi saa moja na nusu kwa siku kuweza kunufaika na uwekezaji huu wa kuku. Pia unaweza kuufanya uwekezaji huu hata kama hauna eneo kubwa. hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo zinapelekea ufugaji wa kuku kuweza kuwa ni moja ya uwekezaji bora sana.
Sikia hii pia ufugaji wa kuku unachukua kati ya miezi mitano hadi nane kuanza kukuingizia faida yaani ni nusu ya mwaka toka uanze kuufanya huu uwekezaji ndio unaweza kuanza kula matunda ya uwekezaji wako, huu ni uwekezaji wa kuku ambao unaufanya kwa mda mfupi na ukaanza kukuingizia kipato kizuri.
Mimi huwa nafikiria jambo moja muhimu katika kukuza uchumi wa familia pamoja na uchumi wa taifa ni kwamba waamue kufanya aina hii ya ufugaji wa kuku ili kukuza uchumi wa familia, kwa kawaida familia nyingi za tanzania mama ni mtu ambaye anabaki nyumbani hivyo kuwa na mda mzuri wakuweza kuhudumia kuku hali itakayopelekea kukuza uchumi wa familia na kuboresha hali ya kiafya za wanafamilia. Mnachohitaji kama wanafamilia ni kuamua kuufanya ufugaji kama sehemu ya uwekezaji wa familia.
Licha ya kuwa na manufaa makubwa katika ufugaji wa kuku changamoto nazo hazipo nyuma, kuna changamoto nyingi ambazo zinawafanya watu wengi kushindwa kuufanya ufugaji wa kuku kwa manufaa makubwa na moja ya changamoto kubwa ni kukosa maarifa juu ya ufugaji wa kuku hii limekuwa tatizo kubwa linalowafanya wafugaji wengi washindwe kutimiza malengo yao.
Huenda wewe ni mmoja ya watu wanaopatia changamoto hii au huenda unashindwa kufanya ufugaji kwa sababu hauna maarifa ya kutosha au huenda umekuwa ukifanya ufugaji wa kuku kwa hasara bila ya manufaa yeyote basi mimi rafiki yako nipo kwaajiri yako kwakuona ukubwa wa tatizo hili nikaona nikuandalie kitabu ambacho kitakupa maarifa ya kina ambayo yatakusaidia uweze kufanya ufugaji wa kuku kwa manufaa makubwa karibu sana ujipatie nakala ya kitabu chako.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Mjasiliamali, mwandishi na mshauri wa mambo mbalimbali ya ujasiriamali
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kwa namba
0758918243/0656918243/0786115129/0621132794
Pia tembelea www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
KARIBU UJIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUSOGEZA KARIBU ZAIDI NA MAFANIKIO
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
HARDCOPY 15000/=
SOFTOPY 7000/=
NGUVU YA MAARIFA
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI.....!
0 Comments