Ad Code

Responsive Advertisement

TENGA MDA KWAAJIRI YA MIFUGO YAKO


TENGA MDA KWAAJIRI YA MIFUGO YAKO

Habari rafiki yangu mpendwa nimatumaini yangu umekua na siku bora sana nikupongeza kwa hilo lakini natumbua katika maisha changamoto huwa haziepukiki hivyo natumaini umekuwa ukipitia changamoto nyingi katika maisha yako napenda nikutie moyo usikate tamaa changamoto nisehemu ya maisha hivyo unapokutana na changamoto yeyote katika maisha yako usikubali changamoto hiyo iwe sehemu ya wewe kushindwa kusonga mbele bali iwe chachu ya wewe kusonga mbele na kufikia mafanikio makubwa hivyo hautakiwi kuzikimbia changamoto kwasababu hauta weza kufanya hivyo kamwe kufanya hivyo bali utaongeza changamoto kubwa katika maisha yako hivyo kwa kila changamoto unayokutana nayo katika maisha yako chukua hatua ya kuitatua changamoto hiyo na songa mbele.
Kabla hatujaendelea na somo la leo kwa nafasi hii ya pekee sana tumshukuru Mungu kwa wema na fadhila zake kwetu, kwasababu siyo kwa uwezo wetu wala kwa juhudi zetu mimi nawewe kuwa hai hadi sasa bali nikwaneema tu, hivyo chukua dakika chache kumshukuru Mungu kwa neema yake yakipekee sana kwetu.

Sasa nikukalibishe sana katika somo ambalo nimekuandalia siku ya leo, kumbuka somo letu linakichwa kinachosema *Tenga mda kwaajiri ya mifugo yako* hili ni somo muhimu sana kwa sisi wafugaji, kumekuwa na utamaduni kuwa mifugo yetu kuwahudumia kwa habari ya chakula pekee na mala nyingi jukumu hili tumekuwa tunawaachia wasaidizi wetu pekee, hali hii inapelekea wafugaji wengi wapate hasara kubwa sana kwa mifugo yetu kutokana na changamoto za magonjwa pamoja na tabia mbaya za kuku kudonoana pamoja na kula mayai.

Ipo hivi wafugaji wengi hawana utamaduni wa kuingia bandani kila siku asubuhi au mchana au jioni wakuwatazama kuku angalau dakika kumi na kuendelea kulingana na idadi ya kuku kwaajiri ya kujua tabia za kuku, hali zao pamoja na maendelea yao, jukumu hili tumeliacha kwa wasaidizi wetu pekee hali inayosababisha changamoto kubwa kwa wafugaji/wamiliki wa mifugo hii hasa pale tatizo la ugonjwa/tabia mbaya za kuku zinapotokea.

Hivyo basi napenda kukukumbusha wewe rafiki yangu kuwa kila siku tenga mda wakuingia bandani katika mifugo yako kwaajiri ya kuangalia tabia mbalimbali za kuku, kwa kufanya hivi kutakusaidia sana kujua tabia na hali za mifugo yako hivyo kutakufanya ugundue mapema kama kuna ugonjwa umeingia ili kuweza kuwapa tiba, hili jambo linamsaada mkubwa sana katika kuleta ufanisi mkubwa wa uwekezaji wako katika ufugaji hasa wakuku. Hata kama unamsaidizi unahaji wewe kama mmiliki kutenga mda wa kuwa na mifugo yako ili uweze kujiepusha na madhara makubwa ya vifo kwa kuku wako.

Mda mzuri wa kujifunza tabia za kuku nipale kuku wako wanapokula chakula hapa nirahisi sana kujua hali za kuku wako kwasababu kama kuna kuku mgonjwa utamwona hana uwezo mkubwa wa kuchangamkia chakula hivyo iwapo atasukumwa kidogo na kuku wengine nirahi kukubali kupigwa na  yeye kukaa pembeni hivyo utakuwa na jukumu la kuangalia kuku huyo anatatizo gani ili kuweza kumpatia tiba mapema kabla ugonjwa haujamuathiri kwa kiwango kikubwa. Hivyo nikusihi sana ewe mfugaji wakuku kujijengea tabia ya kuwatazama kuku wako kila siku ili kujua hali zao na tabia zao.

Wakati mwingine wakutatazama kuku wako nipale ambao hawana chakula ila wamaendelea na shughuri zao, hapa utajifunza tabia mbaya za kuku kama wanazo kama vile kuku kudonoana na kuku kula mayai hili ni jambo bora sana kulifanya kila siku kwa kuku wako. Iwapo utafanya mambo haya machache lakini niyamuhimu sana basi itakusaidia sana wewe mfugaji kuepuka na matatizo ya vifo kwa mifugo yako kwasababu utagundua dalili mapema   hivyo kuwapa tiba mapema.

Nihitimishe kwa kusema kwamba inawezekana kabisa kufuga kuku bila kuku kufa kwa ugonjwa wowote ila kinachotakiwa nikwamba kuwawahi tiba pale ambapo tunaona kuku wanaugua.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Mwandishi, mshauri na mjasiliamari
Unaweza ukajifunza zaidi kwa kutembelea www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kwa namba 0758918243/0656918243/0786115129/0621132794

KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU 

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

NA

NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBW

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI HADI MWISHO, MUNGU AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu