Ad Code

Responsive Advertisement

CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA KUKU

*KONA YA UFUGAJI*

SHEHEMU YA TATU

Habari rafiki yangu, nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora sana hili nijambo bora na lamuhimu sana kwa maisha yetu, kila siku tunajukumu kubwa kuhakikisha maisha yetu yanakuwa bora sana kwa kufanya yale yaliyo bora ambayo yatatufanya tufikie malengo makubwa tuliyonayo katika maisha yetu hii ndio sababu kubwa ya mimi nawewe kuwa hai hadi leo.
hivyo hakikisha kila siku unafanya yale muhimu ambayo yatakufikisha kwenye eneo nzuri zaidi la mafanikio makubwa. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kuweza kutupa uhai a afya njema hadi hii leo tunaweza kukutana kwenye somo hili, siyo kwa juhudu zetu wa kwa uwezo wetu bali nikwaneema tu mimi nawewe kuwa hai hadi sasa niwengi walitamani kuiona siku hii ya leo wakiwa na afya njema kama mimi nawewe lakini sana hawana hata uwezo wa kushika simu zao lakini mimi nawewe tumepata neema hii ya pekee sana hivyo nijukumu letu kuweza kuitumia siku hii ya leo vizuri huku tukahakikisha tunachukua hatua sasa ambazo zitakuwa na manufaa makubwa kwetu na jamii nzima.


CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA KUKU

Ufugaji wa kuku umekuwa ni sehemu nzuri sana ya kujipatia kipato kwa watu tulio wengi hivyo kuchangia maisha yetu kuwa bora sana kwa wakati wa sasa na wakati wa baadae, lakini licha ya uzuri na faida nyingi zilizopo katika ufugaji wakuku pia kuna upande wa pili ambapo zipo changamoto kadhaa ambazo zimekuwa tatizo kubwa kwa wafugaji wengi wakuku hali inayopelekea watu washindwe kunufaika na ufugaji huu wa kuku. Kuwepo cha changamoto hizi hakubadili ukweli kuwa ufugaji ni sehemu nzuri ya kukuza kipato cha mtu binafsi na taifa bali faida hizi zinaendelea kuwepo na zitaendelea kuwepo siku zote.

Hivyo jukumu kubwa tulionalo sisi kama wafugaji ni kuzijua changamoto mbalimbali zilizopo katika ufugaji huu wa kuku na kutafuta majibu ya changamoto hizi ili tuweze kunufaika na ufugaji huu wa kuku.

Zifuatazo ni baadhi ya changamoto kubwa zilizopo katika ufugaji wa  kuku.

MAGONJWA

Hii ndio kubwa kuliko, changamoto ya kwanza na kubwa katika ufugaji wa kuku ni magonjwa, magonjwa kwa kuku yamekuwa sehemu ya tatizo kubwa ambalo linapelekea wafugaji wengi wakate tamaa kabisa na ufugaji huu wa kuku hali inayowapelekea watu wengi kuacha kabisa kufanya ufugaji wa kuku, ni ukweli usiopingika kuwa kuku wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mbalimbali katika ukuaji wake lakini jambo la muhimu sana kufahamu kuwa kwa kuku kuugua siyo jambo baya sana bali kushindwa kupewa tiba sasa hii ndio tatizo kubwa sana kwa kuku wetu, katika sehemu kwanza na yapili nimelezea changamoto hii na hatua za kuchuku ili uweze kuondoka katika eneo hili la changamoto. Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku ambaye umekuwa ukikutana na changamoto mbalimbali katika ufugaji wa kuku naomba tuwasiliane ili nikipe ushauri bora ambao utakudaidia kuondoka kwenye changamoto hizo.

2)GHARAMA KUBWA YA CHAKULA.

Hii nisehemu ya changamoto kubwa katika ufugaji wa kuku, watu wengi wamekuwa wakifanya ufugaji lakini wamekuwa wakiteseka sana na gharama kubwa ya chakula hali inayowapelekea wafanye ufugaji kwa kiwango kidogo sana au kufanya ufugaji usio na faida kulingana na gharama kubwa ya chakula ambayo wamekuwa wakitumia, hii imekuwa ikiwakatisha tamaa wafugaji wengi hali inayowapelekea kufikiri kuwa ili uweze kufanya ufugaji basi unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa, hivyo kwa baadhi wamefikia kusema kuwa ufugaji wa kuku ni uwekezaji usio na faida. Naomba nikwambie rafiki , ufugaji wa kuku ni moja ya uwekezaji bora sana na wenye faida nzuri iwapo utajua njia sahihi ya kuweza kupunguza gharama hizi za chakula na baadhi ya njia hizo ni kutengeneza chakula wewe mwenyewe nyumbani pamoja na kuwatengenezea kuku wako chakula cha ziada kama vile azolla, hydroponic fodder pomoja na funza. Njia hizi zinamsaada mkubwa kuweza kupunguza gharama za chakula kwa kiasi kikubwa sana na wewe ukanufaika na ufugaji huu wa kuku.

 Ngoja nikupe mfano kidogo. Iwapo chakula utanunua dukani kwa mfuko wa kilo 50 huuzwa kwa wastani wa 50,000Tsh. Lakini iwapo utatengeneza wewe mwenyewe nyumbani utafanikiwa kupunguza gharama ya 20,000 hadi 15000Tsh hivyo kuwa umetengeneza chakula chenye ujazo huo huo kwa gharama ya 30,000Tsh hadi 35000Tsh. Hebu angalia huoni faida hapo ya kutengeneza chakula wewe mwenyewe kuliko kununua chakula cha mfuko dukani (wauzaji wa chakula naomba mnisamehe kidogo kwa leo), ipo hivi rafiki mtu anayeuza chakula cha kuku ambacho kimeshachanganywa kabisa anakuwa amepitia hatua mbalimbali ambazo zimesaidia chakula hadi kikiwe pale dukani. Njia hizo ni kama ifuatavyo

➡Chakula hicho hajatengeneza yeye bali amenunua kwa watu ambao wametengeneza hicho chakula

➡Amesafirisha kuleta hadi hapo dukani.

➡Aliye tengeneza pia ametumia gharama hivyo akachukua gharama hizo akaongeza sehemu ya faida na kumuuzia muuza duka.

➡Nayeye muuza duka akaongeza sehemu ya faida ndipo na yeye akakuuzia wewe.

Hebu angalia huo mlolongo ulivyo kuwepo je hauoni kuwa kuna haja ya wewe kutengeneza chakula wewe mwenyewe na kuweza kuwalisha mifugo yako? Rafiki kwa kufanya hivi utafainikiwa kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa. Hebu leo amua kuanza kutengeneza chakula wewe mwenyewe nyumbani.

Lakini unaweza kupunguza zaidi gharama ya chakula kwa kutumia Azolla pamoja na hydroponic fodder hii itakusaidia kupunguza gharama kwa kiasi kukubwa zaidi.


Oops! Naomba tuishie hapa kwa leo tutaendelea tena wakati ujao hivyo usipange kukosa mwendelezo wa somo hili muhimu katika kukupatia maarifa muhimu ya ufugaji wa kuku.

NB: jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe nyumbani nimekuandalia kitabu ambacho nimeeleza kwa undani kuhusu jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, pamoja na jinsi ya kutumia azolla na hydroponic fodder kwa manufaa ya ufugaji wako, siyo hayo tu kitabu hiki nimejaa maarifa bora kuhusu ufugaji wa kuku wenye manufaa makubwa.

Ni mimi rafiki yako.
Frank mapunda
Unaweza kuwasiliana nami kwa mawasiliano zaidi kwa namba
0758918243
0656918243
0786115129

Pia unaweza kutembelea  *www.nguvuyamaarifa.blogspot.com*

JIPATIE VITABU ILI UONGEZE MAARIFA ZAIDI KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu