Ad Code

Responsive Advertisement

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUTHIBITI CHANGAMOTO

KONA YA UFUGAJI

SEHEMU YA PILI

Habari rafiki yangu, nimatumaini yangu kuwa umeamka salama na kufanikiwa kuianza siku hii ya leo kwa ubora wa hali ya juu sana, kama ni hivyo nakupa hongera sana lakini pia natambua siyo wote tumepata nafasi ya kuioa siku ya leo tukiwa na afya bora bali kuna wengine  niwagonjwa au wemeamka na changoto nyingi ambazo zimewafanya waianze siku hii kwa unyonge sana hawa nawapa pole sana,
kama kuna changamoto yeyote ya kiafya inakusumbua basi chukua hatua mala moja kuweza kuitatua changamoto hiyo na wewe ambaye umeianza siku yako kinyonge kwasababu mbalimbali basi chukua hatua kutatua changamoto hiyo mapema ili uweze kuishi maisha yenye maana. Kabla ya kuendelea mbele kwa heshima ya kipekee sana tumshukuru Mungu kwa neema yake yakipekee sana kwetu kuweza kutufanikisha mimi nawewe tuweze kuiona siku ya leo, siyo kwamba sisi ni wema sana au tunastahili sana kuliko wengine bali ni kwaneema yake pekee tumepata kibari kuiona siku hii ya leo,  hivyo tunalo jukumu kubwa kuhakikisha tunaishi maisha yenye maana kwa kwenda kuchukua hatua sahihi ili kuhakikisha tunafikia viwango vya juu vya maisha yetu, kwakuchukua hatua sahihi kwakila jambo basi maisha yetu yatakuwa bora sana.

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUTHIBITI CHANGAMOTO

napenda nichukue nafasi hii yakipekee sana katika mwendelezo wa somo la leo, katika somo lilopita tuliona jinsi changamoto ya magonjwa ilivyo tatizo kwa ufugaji wa kuku lakini hatukuishia hapo tu bali tulenda mbele kidogo kuona hatua za magonjwa ya kuku na hatua za kuchukua kwa kila hatua na leo twende tukaone hatua ya pili muhimu kuchukua ili kuweza kutatua changamoto ya magonjwa kabla hayajaingia.

2)THIBITI MAGONJWA KABLA HAYAJAINGIA

Katika ufugaji wa kuku kwa upande wa magonjwa kuna njia/vyazo mbalimbali vya magonjwa ambayo yamekuwa yakituletea hasara kubwa pale tunaposhindwa kuwapa tiba sahihi. Hivyo ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto hizo za magonjwa nimuhimu sana kufahamu vyanzo mbalimbali vya magonjwa ili tuweze kudhibiti magonjwa hayo yasiweze kuwaathiri mifigo yetu.

>chanzo cha kwanza.~mfugaji kutokuzingatia chanjo sahihi.
Ndio kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafugaji kuto kuzingatia chanjo sahihi kwa kuku hai inayopelekea kuku kukosa kinga mwili kiasi ambacho ugonjwa kuwa rahisi kuingia. Changamoto hii inatokana na wafugaji wengi kufanya ufugaji kwa mazoe bila kuzingatia chanjo muhimu. Rafiki nimuhimu sana kuwa na maara ya chanjo sahihi kwa kuku wako kuanzi wakiwa na umri wa siku moja na kuendelea, chanjo hizo zinasaidia sana kuwakinga kuku na magonjwa, mfano wa chanjo hizo nikama vile kideri, mdondo, ndui na magonjwa ya matumbo. Kwenye kitabu nimeeleza hili kwa kina katika sura ile ya kumi na saba na ukurasa wa 250.

>chanzo cha pili~ mazingira machafu ya kuishi mifugo.

Hii ni moja ya sababu kubwa ya kuku kuugua magonjwa mala kwa mala, kuku wanapokuwa kwenye mazingira machafu inawasababishia wale sehemu ya kinyesi chao na uchafu mwingine uliopo kwenye banda kiasi ambacho inakuwa rahisi kuku kupata magonjwa. Njia sahihi ya kudhibiti tatizo hili nikuhakikisha banda lako linakuwa safi nakavu mda wate hii itakusaidia sana kuwakinga kuku wako na magonjwa ya mala kwa mala, lakini pia unaweza kuwatengenezea cage ambayo itawafanya kuku wako wale kwa juu na uchafu wowote uweze kushuka chini hii itawasaidia sana kuku wako washindwe kula uchafu ulio bandani kwasababu uchafu wote unakuwa upo chini, hii ni moja kati ya njia bora sana kuhakikisha unapungua kwa sehemu kubwa ya magonjwa kwa kuku wako.

3)chanzo cha tatu~kuku kukosa kinga katika mwili wake.

Hii ni sababu muhimu sana ya kuku kupata magonjwa ya mala kwa mala. Ipo hivi rafiki, chanzo cha kuku kuugua nikutokana na kuku kukosa/kupungua kwa kinga ambazo zinahusika katika kudhibiti ugonjwa huo na hii inasababishwa na aina ya chakula ambacho kuku wetu wanakula, hivyo ili kuongeza ufanisi mkunwa kwa kuku wako nimuhimu ukawapa chakula ambacho kinaenda kuogeza kinga kwa wingi katika miili yalo hali itakayopelekea kuku wako kuishi bila kuugua, hapo ndipo utakapo kutana na mimea ambayo inakiwango kikubwa cha kinga ambacho kinasaidia kuwafanya kuku wako wawe na kinga nyingi mwilini zakuweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali. Hapo ndipo unapokutana na mimea yenye viwango vikubwa vya kuwaongezea kinga kwa kuku, uzuri wa mimea hii ni sehemu ya lishe kwa kuku na baadhi ya mimea hiyo nikama vile azolla, hydroponic fodder (mimea hii nimeieleza kwa undani kwenye kitabu katika sura ile ya kumi na sita na ukurasa wa 229) ukiachana na mimea hiyo ipo mimea mingine kama vile alovera, majani ya mpapai, majani ya mpera, mronge, mwarobaini, pilipili kichaa, na mrose (mimea hii yote nimeieleze kwa undani kwenye kitabu katika sura ile ya kumi na tisa ambayo inapatikana kwenye ukurasa wa 303) kwa kufanya mambo haya utapunguza kwa kiasi kikubwa cha magonjwa kwa kuku wako hali itakayopelekea uweze kupata faida kwa kuku wako.

Rafiki kama umekuwa mmoja ya wafugaji ambao unapitia changamo kubwa katika ufugaji huu wa kuku basi naomba tuwasiliane ili nikushauri njia sahihi zakuweza kuondoka katika changamoto hizo.

Ni mimi rafiki yako
Mwandishi na mwalimu wa ujasiriamali
Frank mapunda
Unaweza kunipata kwa mawasiliao namba
0758918243
0656918243
0786115129

PIA UNAWEZA KUJIFUNZA ZAIDI KUTOKA KWANGU KUPITIA VITABU HIVI

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

HARDCOPY 15000/=

SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI ENDELEA KUNIFATILIA KWA MAARIFA BORA YATAKUYO INUA MAFANIKIO YAKO, MDA SI MREFU UTAWEZA KUNIPATA KWA NJIA YA BLOG HII *www.nguvuyamaarifa.blogspot.com*

Post a Comment

0 Comments

Close Menu