Ad Code

Responsive Advertisement

UMEJIANDAAJE KWAAJIRI YA KUPATA MAFANIKIO? ~ SEHEMU YA PILI



Habari rafiki, nimatumaini yangu kuwa upo salama sana hivyo unachukua hatua sahihi kuelekea mafanikio makubwa ambayo unayahitaji, hakuna njia ya mkato kuelekea mafaniko zaidi ya kuchukua hatua kila siku hata kama kwa udogo lakini hizo hatua ndogo ndogo ndizo zinazokuja kuzalisha matokeo makubwa hivyo nikusii sana wewe rafiki yangu mpendwa usiache kuchukua hatua kila siku zakuweza kukupeleka karibu zaidi na ndoto zako, sina shaka kuhusu kuwa wewe kuwa na ndoto kubwa naamini  unayo.
Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii ya kipekee sana kumshukuru Mungu wetu  aliye Muumbaji wa vyote kwa wema na fadhili zake juu yetu mimi kupata nafasi ya kuandika siku hii ya leo siyo kwa nguvu na uwezo wangu bali  nikwaneema ya Mungu tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna wengi walitamani wawe na nafasi ya uzima kama hii ili waweze kuandika mambo mengi makubwa lakini sasa wapo kitandani na hawawezi hata kushika kifaa cha kuandika, kuna wengi walitamani leo wafanye mambo makubwa ya kuleta matokeo makubwa kwa dunia lakini sasa wamelala kaburini, hivyo mimi nawewe kupata nafasi hii siyo kwa juhudi zetu wala kwa uwezo wetu,  wala siyo kwamba tumetenda wema sana kuliko wengine bali ni kwaneema tu, hivyo tunao wajibu wakiitendea haki siku hii nzuri ya leo, tunawajibu wakwenda kuchukua hatua sahihi ambazo zitaenda kutupeleka karibu zaidi na kusudi letu la kuwepo hapa duniani.

Bila ya kupeteza mda nichukue nafasi hii kukubaribisha kwenye somo letu la leo, somo la leo ni mwendelezo wa somo ambalo tulilianza siku zilizopita linakichwa kinacho sema  umejiandaaje kwaajiri ya kupata mafanikio? katika siku ya kwanza tulijifunza maandalizi makubwa mawili ambayo tunatakiwa kuyafanyakwaajiri ya kupata mafanikio ambayo tunayahitaji, lakini katika kufanya maandalizi hatua ya pili tuliishia kwenye kipengele cha kwanza na leo tutaendelea kipengele cha pili na kuendelea.

2~KUFIKIRI BAYANA

Kipengele cha pili
2~FIKIRI BAYANA KUHUSU JAMII YAKO

Katika eneo hili nimuhimu sana kufikiri kuhusu jamii ambayo unalenga kuihudumia. Je unataka jamii yako ikuone wewe ni mtu wa aina gani? Hapa tunaita kujibrandi. Katika kujiandaa kupata mafanikio lazima uwe mtu wa kuleta matokea kwa jamii na jamii ikutambue kuwa Frank ni mtu aina gani? Je jina lako likitajwa mtaana unataka jamii ikuone wewe nimtu wa aina gani? Je wewe kwenye jamii unatoa mchango gani ambao unakutambulisha wewe? Ngoja twende kwa mifano kidogo, leo hii tukutaja jina la Mbwana samata akilini mwako unafikiria nini? Je tukilitaja jina la Kikwete akilini mwako unapata picha gani, je tukilitaja jina la Mengi unapata picha gani, je tukilitaja jina la Rose muhando unapata picha gani? Naamini bila shaka tukilitaja tu jina fulani unapata picha ya mtu huyo ni mtu wa aina gani,  hata kama nitakuwa simaanishi mtu huyu lakini akilini mwako utapata picha ya mtu huyo hii ni kutokana na matokeo ambayo mtu huyo ameyadhalisha katika kitu fulani. Sasa nawewe jina lako likitajwa watu wanatakiwa wapate picha fulani kuhusu wewe. Hii siyo kazi rahisi ambayo unaweza kuifanya kwa siku moja au mwezi mmoja bali unahitaji ufanye kwa kipindi kirefu bila kuacha nakuleta matokeo chanya kwa jamii. Kwa kufanya hivyo unakuwa umejitengenezea njia nzuri kuelekea mafanikio unayoyataka, haikuwa rahi kwa Rose muhando kutengeneza jina (brand) alinalo sasa bali nimatokea ya kuweka juhudi kubwa bila ya kukata tamaa, hata wewe unaweza unachotakiwa nikuchagua kuwa unataka kuwa na mafanikio kupitia nini na kuweka juhudi kubwa katika kulifanya hilo jambo na maisha yako yatakuwa bora lakini pia jamii yako itanufaika sana na wewe.

3~KIPAJI/TAALUMA
Kipaji ni uwezo ambao amezaliwa nao ambao humwezesha kufanya jambo fulani vizuri. Na taaluma ni Elimu ambayo mtu anaupata kwa kufundishwa au kujifunza.(kwenye kitabu cha nguvu ya maarifa katika sura ya tatu nimefundisha kwa undani jinsi ya kugundua kipaji chako, jipatie nakaa ya kitabu hicho ujifunze na uweze kugundua uweo mkubwa ambao Mungu ameuweka ndani yako). Sasa katika kuweza kujiandaa vizuri ili kuweza kupata mafanikio makubwa ni muhimu sana kuwa na kipaji au taaluma ambayo utaifanyia kazi ili kuleta matokeo mazuri kwa jamii yako. Hivyo ni muhimu sana kujiuliza kuwa unataka kuwa na taaluma/kipaji gani ili uweze kupata mafanikio. Ukiangalia kwa undani utagundua watu wengi waliofanikiwa katika maisha wamefanikiwa kupitia taaluma fulani au kipaji fulani,  mfano ukimwangalia Bwana samata amafanikiwa kupitia kipaji chake lakini ukimwangalia mtu mwingine utaona amefanikiwa kupitia taaluma fulani, hivi ni vitu muhimu sana kuwa navyi katika kuelekea mafanikio makubwa unayoyahitaji.

Yafuatayo ni maswali muhimu sana ya kujiuliza ambayo yatakusiadia kujenga taaluma/kipaji ambacho kitakusaidia kupata mafanikio makubwa.
~je wewe unakipaji gani ambacho unataka jamii inufaike sana kwa kipaji ulicho nacho? Ndio kipaji siyo kwaajiri yako bali Mungu amekupa kwaajiri ya kuleta matokeo bora kwa jamii sasa unapaswa kujua unakitumiaje kipaji chako Kuweza kuleta matokeo chanya na kwa jamii yako. Kadri unavyoleta matokeo makubwa kwa jamii ndivyo unavyoweza kufanikiwa zaidi.

~Je wewe unataka kujenga taaluma gani katika maisha yako ambayo itakuwa na msaada mkubwa kwa jamii? Kumbuka kuwa taaluma unayoijenga siyo kwaajiri yako bali kwa jamii kubwa ambayo utaihudumia hivyo nimuhimu sana kijenga taaluma ambayo itakuwa  na msaada mkubwa kwa jamii. Ni lazima taaluma yako ilete matokeo chanya kwa jamii inayokuzunguka na dunia kwa ujumla. Hiki nikitu ambacho kinawezekana kwa kila mwenye nia ya kuweza kufanikiwa na kuleta matokeo makubwa kwa jamii.

~Je unataka kuwa mzuri wa nini? Ndio unapotaka kuwa na mafanikio makubwa nilazima uwe mzuri kwenye jambo fulani ambalo ndilo litakalokutambulisha kwa jamii na kukupa mafanikio makubwa unayoyahitaji, hivyo unapaswa kujua kuwa ni taaluma/kipaji gani unatakiwa kukijenga ambacho kitakuwa na msaada mkubwa kwa jamii? Hili ni jambo muhimu sana hata ukichunguza kwa jamii utakuja kugundua kuwa kuna taaluma/kipaji fulani wamekijenga ambacho ndicho kinawafanya wawe na mafanikio makubwa waliyonayo. Sasa wewe kama unataka kuwa na mafaniko makubwa nimuhimu sana kujenga taaluma/kipaji ambacho kitakuwa namsaada mkubwa kwa jamii yako.

~Je ndani ya miaka kumi unataka uwe mzuri kuliko watu wote duniani kupitia taaluma/kipaji gani? Ndio nimuhimu kuwa na malengo ya kuwa nuru kwa jamii kuliko mtu yeyote na inawezekana ukiangalia watu wote unaowafahamu wamefanikiwa kupitia taaluma/vipaji vyoa haikuwa ndani ya siku moja bali wametumia mda mwingi Kuweza kuviboresha vipaji/taaluma zao hadi leo hii wewe unawafahamu,  hivyo nawewe unatakiwa kuweka malengo makubwa juu ya taaluma/kipaji ulicho nacho katika kuleta matokeo bora sana kwa jamii. Nilazima ujione mtu bora zaidi baada ya mda fulani na uchukue hatua kila siku kuhakikisha unafikia ubora huo unaouhitaji, hii itakusaidia sana kuweza kuwa na mafanikio makubwa maishani mwako.

~Je jamii unataka inufaike na nini kupitia wewe? Ndio kipaji au taaluma unayoijenga nilisema siyo kwaajiri yako bali nikwaajiri ya jamii yako sasa taaluma yako nilazima uwe na manufaa makubwa kwa jamii yako hapo ndipo utakapoweza kupata mafaniko makubwa unayoyahitaji. Hebu chunguza watu walio fanikiwa sana katika dunia hii utakuja kugundua kuwa taaluma na vipaji vyao vimekuwa na msaada mkubwa sana kwa jamii mbalimbali za watu.

~Unataka kuongeza/kuboresha taaluma/kipaji chako katika maeneo gani? Ndio kuwa na taaluma/kipaji tu haitoshi kukupa mafanikio makubwa nimuhimu sana kuweza kuboresha zaidi kipaji chako au taaluma yako sasa hapo ni muhimu sana kujua kuwa unataka kuboresha eneo gani la taaluma/kipaji chako ili uweze  kuhudumia jamii kubwa na kwaubora mkubwa zaidi.

~Unahitaji kujenga vipaji/taaluma gani ili ziweze kukusaidia zaidi katika kuisaidia jamii? Ndio nimuhimu sana kujenga taaluma fulani kama hauna ili kuweza kupata mafanikio makubwa. Mfano wa hili ni kama ifuatavyo
>Nahitaji kujifunza zaidi njia bora ambazo zitaniwezesha kunitambulisha kwa jamii kuhusu huduma ambazo ninatoa.
>Nahitaji kutengeneza mfumo bora zaidi ambao    ambao utanisaidia kuwafikia watu wengi zaidi waweze kunufaika na mimi.
>kujifunza njia sahihi ya kuweza kuwasiliana na watu vizuri.

Kwa leo naomba niishie hapa nimuhimu kuyafanyia kazi maarafa haya ili maisha yako na jamii yako iweze kunufaika na uwepo wako hapa duniani,  tukutane tena wakati ujao usipange kukosa mwendelezo wa somo hili ni muhimu sana.

Ni mimi rafiki yako.
Frank mapunda
Masomo haya unaweza kuyapata kwenye blogs hii www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu: 0758918243/0656918243/0786115129
E-mail: nguvyuyamaarifa1@gmail.com

PIA UNAWEZA KUJIPATIA VITABU NA UKANUFAIKA ZAIDI NA  MAARIFA MUHIMU KUHUSU MAFANIKO

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI MUNGU AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu