Habari rafiki yangu mpendwa, nimatumaini yangu kuwa umekuwa na wakati mzuri wa kuchukua hatua kuhakikisha maisha yako yako yanakuwa bora sana hongera kwa hilo, kila siku mpya nisiku nzuri ya kuchukua hatua kuelekea kutimiza ndoto zetu haijalishi ni hatua gani unachukua iwe ni kubwa au ndogo inamchango mkubwa sana katika maisha yako na mafanikio yako hivyo napenda nikukumbushe rafiki yangu mpendwa leo hii nisiku nzuri na bora sana ya wewe kuchukua hatua kuelekea maono/ndoto kubwa uliyonayo.
Kwa nafasi ya kipekee sana tumshukuru Mungu aliye Muumbaji wetu kwakutupa tena nafasi hii nzuri na yakipekee sana kuweza kuwa hai na afya njema hadi wakati huu wa mimi na wewe tunaweza kukutana tena kwanjia ya maandishi siyo kwa uwezo wetu wala kwa nguvu zetu ila nikwaneema tu kuwa hivi tulivyo, sisi siyo kwamba niwatakatifu sana kupata nafasi hii bali nikwaneema tu hivyo niwajibu wetu kutafakari ukuu wa Mungu wetu nakusema Asante Mungu kwa nafasi nzuri na yakipekee sana, rafiki kuwa hai hadi sasa siyo kwa bahati mbaya bali nikwasababu Mungu wetu aliye mkuu ameweka kusudi kubwa ndani yetu hivyo anahitaji tulifanyie kazi ili tuweze kuleta matokeo chanya kwenye ulimwengu huu hivyo leo ni moja ya siku muhimu sana yakuchukua hatua ambayo inaenda kutusogeza karibu zaidi nakutimiza ndoto zetu.
Bila kupoteza wakati sasa twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo, somo ambalo lipo katika muundo wa swali ambalo linauliza Kwanini wafugaji wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye ufugaji wa kuku? hili ni swali muhimu sana ambalo linatakiwa kupewa majibu sahihi. Nimekuwa kwenye secta hii ya ufugaji kwa mda sasa namoja ya jambo kubwa ambalo napenda kulifanya nikuwatembelea wafugaji mbalimbali ili kuweza kujifunza na kupeana ushauri kuhusu ufugaji wa kuku, katika kufanya kwangu hivi nimekutana na wafugaji wengi sana (wakongwe) wafugaji wa mda mrefu sana ambao wamekuwa wakifanya ufugaji lakini hawana mafanikio wamekuwa wanasifa ya kuitwa wafugaji wazoefu lakini ndani ya uzoefu wao hawana mafanikio. Baada ya kuchunguza kwanini wafugaji wengi hawana mafanikio makubwa zaidi sana wamekuwa na maisha tu ya kawaida nikaja kugundua mambo yafuatayo.
1~WANAFANYA UFUGAJI WAKO KWA MAZOEA
Wafugaji wengi wa kuku wamekuwa wakifanya ufugaji wao kwa mazoea hali inayowapelea wapate matokeo madogo kwenye ufugaji, ninapozungumza ufugaji wa mazoea nazungumzia ufugaji ule uliopitwa na wakati. Kwa sasa secta ya ufugaji inakuwa kwa kasi sana na kila siku kuna mbinu mpya ambazo zinaifanya secta ya ufugaji nayo ibadilike sasa ukiwa kama mfugaji ambaye haujaamua kuendana badilika na kujifunza mambo mapya kuhusu ufugaji wa kuku basi jua mafanikio katika ufugaji utaendelea kuyasikia kutoka kwa wengine. Ngoja niingie ndani kidogo, kipindi cha nyuma tulikuwa tunaaina tatu za kuku kama vile kuku waasili, kuku wamayai na kuku wa kienyeji lakini sasa mambo yamebadilika kidogo kuna kuku chotara naye ameongezeka, kuku huyu amekuja kuleta mapinduzi makubwa katika secta ya ufugaji kwa sasa hali inayowapelekea mafanikio makubwa kwa wafugaji, sasa wewe mfugaji ambaye unaishi kwa mazoe nakutegemea kuku waasili wanalipa bila kuangalia mahitaji ya soko kwasasa yapoje utaendelea kupitwa.
Pia kipindi cha nyuma kidogo wafugaji wengi wa kuku wa mayai na nyama walikuwa wanategemea kununua chakula dukani ambacho kimetengenezwa kabisi hali hii iliwafanya wafugaji wafanye ufugaji wao wakuku kwa gharama kubwa sana lakini sasa kutokana naukuaji wa secta hii ya ufugaji unaweza kutengeneza chakula mwenyewe nyumbani na nikawa na ubora mkubwa huku ukitumia nusu ya gharama, ndio nusu ya gharama yaani kama ulikuwa unanunua mfuko kwa shilingi 50,000/= chakula hicho hicho unaweza kukipata kwa 25000/= (kwenye kitabu changu kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku katika ukurasa wa 78 nimefundisha na kueleza jinsi yakutengeneza chakula cha kuku kwa gharama ndogo huku chakula kikiwa na ubora uleule unaotakiwa kwa mifugo yako, vile vile katika ukura wa 210 nimeeleza kwa undani lishe bora ya kuku ni ipi na kwanamna gani unaweza kuengeneza chakula chenye jumla ya lishe bora kwa kuku wako jipatie nakala yako ili unufaike zaidi na maarifa hayo),
Vile vile kutokana na ukuaji wa secta hii ya ufugaji kumekuja kugundulika vyakula vingine ambavyo nibora zaidi kwa ufugaji wa kuku huku vikitumia gharama ya chini zaidi kuweza kuviandaa vyakula hivyo kama vile Azolla, Hydroponic Fodder hivi ni vyakula ambavyo vinaongeza sana thamani ya kuku na kumrudisha katika hasiri yake, vyakula hivi viligundulika na wenzetu ambao wanaishi maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya chakula hivyo kutafuta mbinu mbalimbali zakuweza kupunguza gharama yachakula bila kupunguza ubora wa mifugo hapa ndio walipogundua sayansi kuzalisha majani ambayo nitiba na lishe bora kwa kuku wako (unaweza ukajifunza kwa undani zaidi somo hili katika ukurasa wa 229 nimefundisha kwa undani zaidi jinsi ya kutengeneza chakula hicho na pia jinsi ya kulisha mifugo yako vilevile nikwanamna gani utapunguza gharama ya chakula).
Sasa kwa wafugaji ambao wanafuga kwa mazoe ningumu kujua mbinu hizo namatokeo yake wamekuwa wakifanya ufugaji kwa mazoea yasiyo kuwa na tija. Yani huwezi kupata matokeo bora kwakutumia njia zile zilizo pita na wakati wakati wenzako wanatumia njia mpya zinye kuzaa matunda. Ngoja nikuoneshe kidogo kuku waasili anachuku miezi sita hadi kumi na moja kuanza kutaga na bei ya yai ni 500, lakini kuku chotara ambaye anawahi kutaga anachukua miezi minne na nusu hadi sita kuanza kuanza kutaga bei ya yai moja huunzwa 350-500/= kuku waasili hutaga mayai kati ya 30-70 kwa mwaka lakini kuku chotara hutaga mayai kati ya 150-240 kwa mwaka, kuku wa asili huuzwa akiwa na miezi mitano kati ya 6000-9000 lakini kuku chotara akiwa na umri huo huo huuzwa kati ya 12000-20000/= hebu ona mwenyewe alafu nipe majibu mazoe yako yanakupeleka wapi? Kuna mengi ya kujifunza katika eneo hili yani mda tu hautoshi.
2~KUKOSA MALENGO KATIKA UFUGAJI WA KUKU.
hii imekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi wakuku, watu wamekuwa wakifanya ufugaji wa kuku bila kuwa na malengo nayo makubwa ambayo yafanyiwa kazi, hauwezi kufanikiwa katika ufugaji wa kuku kama hauna malengo halisia hiyo haipo hata kidogo watu wengi wamekuwa wakifugaji bila ya malengo sahihi yani daaa! Inatia huruma unakuta mfugaji leo anakuku mia lakini baada ya miaka mitatu kupita ukienda kumtembelea bado anakuku mia vile vile yani unashindwa hata kujua kuwa huyu hapo ndio amefikaa! Au yani hakuwi yote hii nikutokana na kukosa malengo makubwa katika ufugaji wao. Hili somo nilisha litoa kwa siku za nyuma kidogo kama ukupata nafasi ya kusoma basi ingia www.nguvuyamaarifa.blogspot.com tafuta somo linalosema je nikweli ufugaji unaweza kunipa mafanikio makubwa (utajiri), ndani ya somo hilo utapata kujifunza aina yamalengo ninayoyahitaji uweke kwenye ufugaji wako.
3~KUTUMIA GHARAMA KUBWA YA UFUGAJI NA KUUZA MIFUGO YAO KWA GHARAMA YA CHINI.
Hii pia imekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji kushindwa kufanikiwa katika ufugaji wao wakuku kutokana na kutumia gharama kubwa za ufugaji lakini mwisho wa siku soko linawaamulia bei ndogo kulilo uhalisia wa gharama ambazo wanakuwa wamezitumia. Kwa njia hii hauwezi kukua hata kidogo yani kuku umemtunza kwa 7000/= nawewe unakuja kumuuza kwa 6000-7500 wewe unaweza kukua hapa, najua unashangaa unasema Frank unanidanganya! Oooh! Rafiki siandiki kwaajiri ya kukudanganya bali naandika kwaajiri ya kukwambia ukweli najua wafugaji watakuwa wananielewa vizuri sana hapa ngoja twende kwa mifano halisia kuku chotara unamnunua kwa 2000 kifaranga, na unanunua vifaranga 50 labda jumla unakuwa umetumia 100000/= alafu unaenda kununua madawa hadi kufikia miezi mitatu unakuwa umetumia 60000-80000/= chakula wanakuwa wametumia kilo 183 kwa wastani kilo moja huuzwa 1000 hii nikutokana na ukweli kwamba mfuko mmoja huuzwa 50000/= sasa kwa kilo 183 sawa na 183,000 hiki kiasi kwa mfugaji ambaye alikuwa makini kuwalisha kuku wake kwakipimo sahihi (ukweli nikwamba wafugaji wengi wanawalisha kuku wao bila kipimo hali inayopelekea kutumia gharama kubwa yachuakula kuliko kawaida), gharama ya chanzo cha joto ni 10000/= kwa umeme na 25000-35000/= kwa mkaa hapa itategemea bei ya mkaa ya malahali mfugaji alipo, mshahara wa mtunzaji ni 60,000 kwa miezi yote mitatu (nimeweka gharama ya 20000 tu kwa mwezi), gharama ya nauli 10000/= jumla ya gharama zote ni 423,000 hii ni kwa gharama za kawida kima cha chini utatumia hiyo, sasa tukija sokoni soko linahitaji kuku mmoja tuuze 7000-10000/= ngoja tuone . kama tutauza 7000 basi tutapata 350,000 tukitoa gharama tuliyotumia tutapata hasara ya 73000 lakin tukisema tuuze kwa 80000 tutapata 400000 hivyo kupata hasara ya 23000, lakini tuseme soko lipo vizuri sana umeuza kwa 9000 utapata faida ya 27000, je kwa stahili hiyo unaona mfugaji ananafasi ya kuweza kufanikiwa hapo? Ooooh! Naona ushaanza kuona ukweli eeeh! Tukutane kwenye somo lijalo.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Unaweza kujifunza zaidi kwa kutembelea ww.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu:0758918243/0656918243
E-mail: Nguvuyamaarifa1@gmail.com
PIA UNAWEZA KUJIPATIA VITABU AMBAVYO VITAKUPA MAARIFA ZAIDI KUHUSU MAFANIKIO
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
ASANTE KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO , MUNGU AKUBARIKI SANA.
0 Comments