Ad Code

Responsive Advertisement

NIFANYE NINI ILI UFUGAJI WA KUKU UWEZE KUNIPA MAFANIKIO MAKUBWA?


Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuchukua hatua sahihi ambazo zinakupeleka karibu zaidi na ndoto zako, ndio nijua unayondoto kubwa yakufanya makubwa maisha mwako lakini ndoto hiyo haiwezi kutimia mala moja paaa! Hapana bali ni matokeo yako ya kuchukua hatua kidogo kidogo kila siku yanaenda kuongeza kasi zaidi ya mafanikio yako, hongera sana kama wewe ni mmoja ya hao wanaochuka hatua kila siku kuweza kusogea karibu zaidi na na ndoto zako.
Kwa nafasi ya kipekee sana Napenda kumshukuru Mungu kwa nafasi yakipekee sana anayoendelea kunipa ya mimi kuweza kuwasiliana na wewe siyo kwamba Mimi nawewe ni wema sana, siyo kwamba mimi na wewe niwatakatifu sana kuliko wale walio lala wakiuguza majeraha ya ajari au wakijiuguza magonjwa mbalimbali bali ni kwaneema yake tu mimi nawewe kupata nafasi hii yakipekee sana  hivyo tunapaswa kuitumia nafasi hii kwa juhudi na nidhamu kubwa kuhakikisha tunafanya yale yaliyo sahii tu kufanya hilo ndio kusudi la Mungu kuendelea kutupa uhai mimi na wewe.

Bila ya kupoteza wakati twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo linalouliza nifanye nini ili ufugaji wa kuku uweze kunipa mafanikio makubwa hili niswali ambalo limekuwa likiulizwa na watu wengi sana kwamba kuna mambo gani ninatakiwa nifanye ili niweze kupata mafanikio? Ukiona hadi mtu anajiuliza swali hili ujue kuna mambo mawili yapo lakwanza amefanya ufugaji lakini haujampa mafanikio au anataka kufanya ufugaji lakini hajui nikwanamna gani ufugaji unaweza kumpa mafanikio, hivyo baada ya kuwa na tafakari ya kina ndipo linapoibuka swali nzuri kama hili. Sasa leo napenda nilijibu swali ili wewe kama mfugaji uchukue hatua ambazo zitakupeleka kwenye kutimiza ndoto zako za kuwa na mafanikio makubwa kupitia ufugaji wa kuku.

1~TENGENEZA MAONO MAKUBWA.
 Maono ni picha ambayo mtu anakuwa nayo katika kufikia jambo fulani. Sasa kwenye ufugaji wa kuku wewe mfugaji kitu cha kwanza unachohitaji kufanya kabla kuanza ufugaji wa kuku nikutengeneza picha kubwa kuhusu ufugaji wa kuku. Kosa kubwa wanalofanya wafugaji wengi nikufanya ufugaji wa kuku bila ya kuwa na picha kubwa ndani yao hili nikosa ambalo linawafanya washindwe kufika mbali kwenye ufugaji wakuku. Sasa unapokuwa na ndoto kubwa ndoto yako unaindika. Ndio andika ndoto yako kwamba mimi Frank mapunda ndoto/maono yangu katika ufugaji wa kuku ni kumiliki kampuni kubwa ya ufugaji wa kuku yenye kuwa na kuku laki laki tano ambapo ndani yake nitakuwa na branchi kumi katika mikoa kumi ya tanzania. Baada ya kuwa na ndoto kubwa ambayo inaonesha wapi unataka kufika katika ufugaji wa kuku sasa nenda katika hatua ya pili.

2~WEKA MALENGO YA JINSI YA KUFIKIA NDOTO YAKO.
Katika somo lililopita nilieleza jinsi ya kuweka malengo sahihi ya ufugaji wa kuku kama ukupata somo hilo basi ingia www.nguvuyamaarifa.blogspot.com utakutana na somo hilo. Malengo unayoyaweka nimuhimu yakawa malengo ambalo yatakufikisha kwenye ndoto zako. Baada ya kuweka malengo hatua inayofuata ni

3~TAFUTA MAARIFA SAHIHI KUHUSIANA NA UFUGAJI WA KUKU.
Hili ni jambo la muhimu sana kabla ya kuchukua hatua kuanza kuufanya ufugaji wako, iwapo utaamua kuingia kwenye ufugaji wa kuku bila ya kutafuta maarifa sahihi hauwezi kufanikisha ndoto zako hata kidogo kwasababu ufugaji wa kuku unachangamoto zake nyingi na changamoto hizo tayari zinamajibu kwasababu kabla ya wewe haujakutana nazo sisi tulioanza ufugaji tulikutana nazo tayari hivyo tukatafuta maarifa ambayo yalitufanya tuodoke kwenye changamoto hizo, hivyo wewe kabla ya kuingia kwenye ufugaji na ukakutana na changamoto ndipo ujifunze bali unatakiwa ujifunze kwanza ndipo uingie kwenye huo ufugaji, hapo ndipo ulipo umuhimu mkubwa kwako kupata kitabu kiitwacho *Tajirika kwa ufugaji wakuku* ambapo ndini yake utajifunza nakupa maarifa yote muhimu kuhusu ufigaji wakuku, ndani ya kitabu hiki utajifunza mambo mengi ambayo hapo masikio yako hayakupata kuyasikia hivyo hii ni hatua muhimu sana kabla ya kuendelea na hatua nyingine. Hatua inayofuata baada ya kuwa na maarifa sahihi kuhusu ufugaji wa kuku  ni

4-ANZA NA ULICHONACHO.
Ndio anza na ulichonacho nikweli unamaaono makubwa lakini ndani yako unamtaji mdogo hautakiwi kuacha kuanza eti kisa unamtaji mdogo hapa bali unatakiwa kuanza kuchukua hatua kwa hicho ulichonacho hata kama malengo yako ni kufuga kuku laki tano lakini sasa unamtaji wa kufuga kuku wawili anza na hao wawili baada ya miezi nane hata kuwa wawili tena (kwenye kitabu cha Tajirika kwa ufugaji wa kuku sura ya kumi nimefundisha kwa kina kanuni ya kuanzia chini hadi mafanikio makubwa hapo nimeelza kwa undani nikwajinsi gani unaweza kuanza ufugaji wa kuku hata kama hauna mtaji wakutosha, vile vile kwenye ukurasa wa 115 nimefundisha kwa kina jinsi ya kutumia kanuni ya anza na ulicho nacho). Baada ya hatua hii hatua  inayofuata ni

5~USIKATE TAMAANA
Ndio napenda nikwambie hili mapema usije sema sikusema, mafanikio yeyote hayajawahi kuwa rahisi hata kidogo ndio maana wechache wamefanikiwa ila wengi hawajafanikiwa kinacho watofautisha wale walio fanikiwa na wale wasiofanikiwa ni kiwango chao cha kustahimili changamoto, katika ufagaji wa kuku utakutana na changamoto nyingi kama vile kuku kuibiwa au kufa kwa magonjwa kutokana na kukosa dawa sahihi, au kuyumba kwa uchumi hivyo kusababisha kushindwa kuwahudumia kuku wako, au kukosa soko la uhakika la kuweza kuuza mifugo yao au kukosa uaminifu kwa wafanyakazi wako au kutokea kwa maafa ambayo yatasababisha kupoteza kuku wako, changamoto yeyote utakayo kutana nayo unapaswa kuichukulia kama funzo kwako jifunze kupitia changamoto hiyo na chukua hatua sahihi kuweza kusonga mbele. Mimi unayeniona leo nilikutana na changamoto nyingi sana kipindi naanza ilifikia hatua nilihisi nimekosea kuchagua aina hii ya uwekezaji lakini sikukubali changamoto zinifanye nipoteze ndoto yangu sikukubali changamoto zinirudishe nyuma bali nilichukua hatua ambazo sasa ninazifurahia kiasi ambacho naona maono yangu yanaenda kutimia, hata wewe rafiki yangu nakwambia usikate tamaa.

Kwa leo naomba niishie hapa tukutane tena wakati ujao.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
E-mail:Nguvuyamaarifa1@gmail.com
Simu:0758918243/0656918243
Kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanapitia changamoto yeyote katika ufugaji wakuku basi usisite kuwasiliana nami.

KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAONGEZA ZAIDI MAARIFA YAKO KUHUSU MAFANIKIO YAKO

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI.

Post a Comment

1 Comments

  1. Habari Bwana Mapunda.
    Nawezaje kupata hicho kitabu cha NIFANYE NINI ILI UFUGAJI WA KUKU UWEZE KUNIPA MAFANIKIO MAKUBWA?

    Soft copy, lakini pia naomba discount

    ReplyDelete

Close Menu