Habari rafiki, nimatumaini yangu kuwa upo salama sana hivyo unachukua hatua sahihi kuelekea mafanikio makubwa ambayo unayahitaji, hakuna njia ya mkato kuelekea mafaniko zaidi ya kuchukua hatua kila siku hata kama kwa udogo lakini hizo hatua ndogo ndogo ndizo zinazokuja kuzalisha matokeo makubwa
hivyo nikusii sana wewe rafiki yangu mpendwa usiache kuchukua hatua kila siku zakuweza kukupeleka karibu zaidi na ndoto zako, sina shaka kuhusu kuwa wewe kuwa na ndoto kubwa naamini unayo. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii ya kipekee sana kumshukuru Mungu wetu aliye Muumbaji wa vyote kwa wema na fadhili zake juu yetu mimi kupata nafasi ya kuandika siku hii ya leo siyo kwa nguvu na uwezo wangu bali nikwaneema ya Mungu tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna wengi walitamani wawe na nafasi ya uzima kama hii ili waweze kuandika mambo mengi makubwa lakini sasa wapo kitandani na hawawezi hata kushika kifaa cha kuandika, kuna wengi walitamani leo wafanye mambo makubwa ya kuleta matokeo makubwa kwa dunia lakini sasa wamelala kaburini, hivyo mimi nawewe kupata nafasi hii siyo kwa juhudi zetu wala kwa uwezo wetu, wala siyo kwamba tumetenda wema sana kuliko wengine bali ni kwaneema tu, hivyo tunao wajibu wakiitendea haki siku hii nzuri ya leo, tunawajibu wakwenda kuchukua hatua sahihi ambazo zitaenda kutupeleka karibu zaidi na kusudi letu la kuwepo hapa duniani.
Bila ya kupeteza mda nichukue nafasi hii kukubaribisha kwenye somo letu la leo, somo la leo ni mwendelezo wa somo ambalo tulilianza siku zilizopita linekichwa kinachosema *umejiandaaje kwaajiri ya kupata mafanikio* katika somo lilopita tulijifunza kipengele cha pili kinachohusu maandaalizi ambayo yanatakiwa kuwekwa kwaajiri ya kupata mafanikio makubwa tunayoyahitaji sasa leo tutaenda kuangalia kipengele cha tatu na kuendelea ambavyo tunatakiwa kufikiri bayana kwaajiri ya kupata mafanikio.
3~KIPAJI/TAALUMA
Kipaji ni uwezo ambao amezaliwa nao ambao humwezesha kufanya jambo fulani vizuri. Na taaluma ni Elimu ambayo mtu anaupata kwa kufundishwa au kujifunza.(kwenye kitabu cha nguvu ya maarifa katika sura ya tatu nimefundisha kwa undani jinsi ya kugundua kipaji chako, jipatie nakaa ya kitabu hicho ujifunze na uweze kugundua uweo mkubwa ambao Mungu ameuweka ndani yako). Sasa katika kuweza kujiandaa vizuri ili kuweza kupata mafanikio makubwa ni muhimu sana kuwa na kipaji au taaluma ambayo utaifanyia kazi ili kuleta matokeo mazuri kwa jamii yako. Hivyo ni muhimu sana kujiuliza kuwa unataka kuwa na taaluma/kipaji gani ili uweze kupata mafanikio. Ukiangalia kwa undani utagundua watu wengi waliofanikiwa katika maisha wamefanikiwa kupitia taaluma fulani au kipaji fulani, mfano ukimwangalia Bwana samata amafanikiwa kupitia kipaji chake lakini ukimwangalia mtu mwingine utaona amefanikiwa kupitia taaluma fulani, hivi ni vitu muhimu sana kuwa navyo katika kuelekea mafanikio makubwa unayoyahitaji.
Yafuatayo ni maswali muhimu sana ya kujiuliza ambayo yatakusiadia kujenga taaluma/kipaji ambacho kitakusaidia kupata mafanikio makubwa.
~je wewe unakipaji gani ambacho unataka jamii inufaike sana kwa kipaji ulicho nacho? Ndio kipaji siyo kwaajiri yako bali Mungu amekupa kwaajiri ya kuleta matokeo bora kwa jamii sasa unapaswa kujua unakitumiaje kipaji chako Kuweza kuleta matokeo chanya na kwa jamii yako. Kadri unavyoleta matokeo makubwa kwa jamii ndivyo unavyoweza kufanikiwa zaidi.
~Je wewe unataka kujenga taaluma gani katika maisha yako ambayo itakuwa na msaada mkubwa kwa jamii? Kumbuka kuwa taaluma unayoijenga siyo kwaajiri yako bali kwa jamii kubwa ambayo utaihudumia hivyo nimuhimu sana kijenga taaluma ambayo itakuwa na msaada mkubwa kwa jamii. Ni lazima taaluma yako ilete matokeo chanya kwa jamii inayokuzunguka na dunia kwa ujumla. Hiki nikitu ambacho kinawezekana kwa kila mwenye nia ya kuweza kufanikiwa na kuleta matokeo makubwa kwa jamii.
~Je unataka kuwa mzuri wa nini? Ndio unapotaka kuwa na mafanikio makubwa nilazima uwe mzuri kwenye jambo fulani ambalo ndilo litakalokutambulisha kwa jamii na kukupa mafanikio makubwa unayoyahitaji, hivyo unapaswa kujua kuwa ni taaluma/kipaji gani unatakiwa kukijenga ambacho kitakuwa na msaada mkubwa kwa jamii? Hili ni jambo muhimu sana hata ukichunguza kwa jamii utakuja kugundua kuwa kuna taaluma/kipaji fulani wamekijenga ambacho ndicho kinawafanya wawe na mafanikio makubwa waliyonayo. Sasa wewe kama unataka kuwa na mafaniko makubwa nimuhimu sana kujenga taaluma/kipaji ambacho kitakuwa namsaada mkubwa kwa jamii yako.
~Je ndani ya miaka kumi unataka uwe mzuri kuliko watu wote duniani kupitia taaluma/kipaji gani? Ndio nimuhimu kuwa na malengo ya kuwa nuru kwa jamii kuliko mtu yeyote na inawezekana ukiangalia watu wote unaowafahamu wamefanikiwa kupitia taaluma/vipaji vyoa haikuwa ndani ya siku moja bali wametumia mda mwingi Kuweza kuviboresha vipaji/taaluma zao hadi leo hii wewe unawafahamu, hivyo nawewe unatakiwa kuweka malengo makubwa juu ya taaluma/kipaji ulicho nacho katika kuleta matokeo bora sana kwa jamii. Nilazima ujione mtu bora zaidi baada ya mda fulani na uchukue hatua kila siku kuhakikisha unafikia ubora huo unaouhitaji, hii itakusaidia sana kuweza kuwa na mafanikio makubwa maishani mwako.
~Je jamii unataka inufaike na nini kupitia wewe? Ndio kipaji au taaluma unayoijenga nilisema siyo kwaajiri yako bali nikwaajiri ya jamii yako sasa taaluma yako nilazima uwe na manufaa makubwa kwa jamii yako hapo ndipo utakapoweza kupata mafaniko makubwa unayoyahitaji. Hebu chunguza watu walio fanikiwa sana katika dunia hii utakuja kugundua kuwa taaluma na vipaji vyao vimekuwa na msaada mkubwa sana kwa jamii mbalimbali za watu.
~Unataka kuongeza/kuboresha taaluma/kipaji chako katika maeneo gani? Ndio kuwa na taaluma/kipaji tu haitoshi kukupa mafanikio makubwa nimuhimu sana kuweza kuboresha zaidi kipaji chako au taaluma yako sasa hapo ni muhimu sana kujua kuwa unataka kuboresha eneo gani la taaluma/kipaji chako ili uweze kuhudumia jamii kubwa na kwaubora mkubwa zaidi.
~Unahitaji kujenga vipaji/taaluma gani ili ziweze kukusaidia zaidi katika kuisaidia jamii? Ndio nimuhimu sana kujenga taaluma fulani kama hauna ili kuweza kupata mafanikio makubwa. Mfano wa hili ni kama ifuatavyo
>Nahitaji kujifunza zaidi njia bora ambazo zitaniwezesha kunitambulisha kwa jamii kuhusu huduma ambazo ninatoa.
>Nahitaji kutengeneza mfumo bora zaidi ambao ambao utanisaidia kuwafikia watu wengi zaidi waweze kunufaika na mimi.
>kujifunza njia sahihi ya kuweza kuwasiliana na watu
Hayo ndiyo mambo Muhimu sana kuyajenga kwaajiri ya kupata mafanikio hakuna mtu yeyote duniani ambaye amefanikiwa bila ya kutumua kipaji chake au taaluma yake, hivyo wewe rafiki yangu ambaye nimsafiri wa kwenda kwenye mafanikio leo hii kaachini na tafakari mwisho njoo na majibu sahihi kuhusu kipaji au taaluma ambayo unatakiwa kuwa nayo ambayo itakusaidia kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji.
4~HUDUMA
Ili uweze kupata mafanikio nimuhimu kutoa huduma kwa jamii ambayo ndiyo itakayo kupa mafanikio, hapa unatakiwa kuwa na majibu sahihi kuwa unataka kuwasaidia watu kupata nini? Ni huduma gani ambayo unakusudia kuitoa ambayo itakuwa na msaada kwa jamii. Hili nijambo muhimu sana kulifahamu kwasababu unaweza kuwa na taaluma/kipaji lakini ukashindwa kutumia taaluma yako au kipaji chako kwaajiri ya kuisaidia jamii, na iwapo hauta kuwa na huduma ambayo inamchango mzuri kwa jamii hauwezi kupata mafanikio makubwa hata kama unamaono makubwa kiasi gani?. Sasa katika kutoa huduma bora kwa wale ambao umewakusudia nimuhimu kujiuliza maswali yafuatayo.
~unataka kuwasaidia watu kupata nini na kivipi;
Hili niswali Muhimu sana ambalo unapaswa kujiuliza kupitia huduma ambayo unataka kuitoa, lazima uwe majibu ambayo yataonyesha jinsi huduma yako itakavyotatua matatizo ya jamii yako. Bila kuwa na utatuzi wa matatizo ya jamii yako ningumu sana kupata mafanikio na njia hiyo tunaita utapele siyo huduma.
~je watu unaowahudumia wanataka nini?;
Hili niswali Muhimu sana ambalo unatakiwa kuwa na majibu nayo. Hii nikutokana na ukweli kwamba bidhaa au huduma tunayoitoa siyo kwaajiri yetu bali nikwaajiri ya jamii hivyo nimuhimu kujua mahitaji ya wateja wako ili kule majibu kwa matatizo yao. Kumekuwa nakosa kubwa kwa baadhi ya watu kwamba wanapeleka huduma mahali ambapo jamii ya eneo hili walikuwa hawaitaji huduma hiyo matokeo yake wamepata hasara kubwa ambayo inawapelekea kushindwa kufikia mafanikio wanayoyahitaji, hivyo napenda nikusihii wewe rafiki yangu kuwa kabla ya kuleta huduma fulani sehemu yeyote basi hakikisha umefanya utafiti katika eneo hilo na kujua mahitaji ya jamii yao katika eneo husika.
~Je utawahudumia vipi ili waweze kunufaika na huduma yako?;
Hili ni swali muhimu sana kujiuliza kabla ya kuleta huduma kwa wateja wako hii nikutokana na ukweli kuwa huduma ambayo unata kuitoa kuna watu wengine walisha wahi kutoa au wanaendelea kutoa katika eneo hilo sasa wewe ambaye unataka kwenda kuanza kupeleka huduma yako kwa jamii hiyo nimuhimu sana kuja na majibu ambayo yataonesha njia ambayo utaitumia Kuweza kuleta huduma kwa jamii husika.
~je unataka kutoa hisia gani kwa wateja wako;
Hili niswali Muhimu sana katika kutoa huduma, biashara yeyote yenye mafanikio ukiichunguza kwa ndani utagundua wamili wa biashara hiyo wamewatengenezea wateja wao hisia fulani ambazo zinawafanya wateja wao waendelee kupata huduma katika eneo hilo. Hebu nikuulize swali hapo ulipo kuna maduka mengi sana ya simu lakini wewe ukihitaji kununua simu utaenda kununua duka gani (naamini kuwa duka utakaloenda utaeda kwasababu duka hilo limetengeneza hisia fulani ambayo inakuvutia kwenda duka hilo) hii ipo hata kwenye maji safi ya kunywa kuna wengine wakiyaona maji yakilimanjoro wanapata hisia ambazo zinawavutia sana kunywa maji hayo. Sasa wewe kama mtoa huduma nimuhimu sana kutengeneza hisia nzuri kwa biashara yako ambazo zitawafanya wateja wafikirie zaidi huduma yako baada ya kufikiria huduma ya mtu mwingine.
~je unataka kuwa na hisia gani mda mwingi kwenye huduma yako;
Hili ni swali muhimu sana ambalo unatakiwa ulipe majibu sahihi, ipo hivi rafiki katika kutoa huduma ambayo itakuwa na mafanikio makubwa nimuhimu sana wewe kama mto huduma kuwa na hisia fulani ambayo utaionesha kila siku bila kujari mazingira, hii itawasia sana wateja wako waweze kukujua vizuri na waweze kuendana na wewe, kuna hisia ambao ukiwa nazo zitawavutia zaidi wateja na hisia zingine ukiwa nazo zikawapoteza wateja wako hivyo nimuhimu sana kujua hisia sahihi yakuwa nayo ambayo itakuwa na mchango mzuri kwa huduma ambayo utaitoa baadhi ya hisia hizo nikama vile hisia za furaha, hisia za huzuni, hisia za chanya na hisia hasi.
Kwa leo naomba niishie hapa tukutane tena katika somo lijalo ambalo tutaendelea kujifunza mambo muhimu ambayo tunatakiwa kuwa nayo wakati ambao tunajiandaa kwaajiri ya kupata mafanikio makubwa tunayoyahitaji, mambo haya unatakiwa kuwanayo wakati wote wa maisha yako.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Blogs:Nguvuyamaarifa.blogspot.com
E-mail: Nguvuyamaarifa1@gmail.com
Simu: 0758918243/0656918243/0786115129
UNAWEZA KUJIPATIA VITABU AMBAVYO VITAKUPA ZAIDI MAARIFA AMBAYO YATAKUWA NA MSAADA MKUBWA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO YAKO.
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=
0 Comments