SEHEMU YA PILI
Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu u mzima wa afya njema kabisa, kama nihivyo basi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, kabla hatuajaendelea mbele tuchukie nafasi hii kijikumbuka kaulimbiu yatu kuu ya mwaka wetu huu wa mafanikio makubwa ambayo inasema KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA (KKK), Haya ni maneno muhimu sana ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi kila siku ya maisha yetu, kila siku niwajibu wetu mkuu kujifunza na tunaenda kujifunza kupitia eneo ambalo tunalifanyia kazi, tunaenda kujifunza kupitia changamoto tunazokutana nazo, tunaenda kujifunza kupitia kusoma vitabu hivyo kujifunza, kujifunza na kujifunza ndio msingi wetu wa kila siku ya maisha yetu, baada kujifunza tunaingia hatua ya pili nikutafakari yale tuliyojifunza na baada ya kutafakari tunaenda kuchukua hatua, mambo hayo matatu ndio mambo ambayo yatafanya mwaka wetu huu uwe ni mwaka wa tofauti sana katika maisha yetu ndio mwaka ambao tunaenda kufanya mambo makubwa sana kuliko mwaka wowote ambao tumepata nafasi ya kuuishi duniani hapa hii ndio maana ya kusema huu ni mwaka wetu wamafanikio makubwa.
Oooooh! Kabla hatujapoteza mda sasa twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo somo ambalo tulilianza siku ya jana ambapo tunajifunza mambo muhimu yakuzingatia katika kujenga ushujaa ambao utatusaidia kuweza kupata mafanikio makubwa, katika siku ya jana tulijifunza jambo moja muhimu la kuzingatia ili kuweza kujenga ushujaa ambao utakuwa na msaada katika kupata mafanikio, sasa leo twende tukajifunze mambo jambo la pili muhimu kuzingatia katika kujenga ushujaa.
2~SAMBAZA UKWELI NA MALENGO YAKO.
Hili nijambo la muhimu sana katika kujenga ushujaa katika mafanikio yako. Hivyo kila mmoja katika eneo hili anapaswa kusambaza ukweli na malengo yako kwa wengine. Najua bado hauja nielewa, ninaposema kusambaza ukweli na malengo yako kwa wengine namaanisha kuwa unapaswa kuwa na watu muhimu ambao utawaambia malengo yako makubwa ambayo unayafanyia kazi kwa miaka kadhaa, kwa mwaka, mwezi na hata siku. Ngoja nizame kidogo hapa ninachomaanisha kuwa katika kujenga ushujaa nimuhimu sana kuwa na malengo makubwa ambayo ndio tageti yako katika kufikia mafanikio makubwa, sasa ili kuweza kutimiza malengo hayo unatakiwa uyagawe katika makundi kadhaa au tunasema inabidi uyagawe katika vipindi kadhaa kama vile lengo la miaka kumi katika lengo hilo unaligawa tena kwa miaka mitano na baada ya hapo unaligawa tena kwa mwaka mmoja na baada ya hapo unaligawa katika mfumo wa mwezi mmoja mmoja na unaendelea kuligawa katika kipindi cha wiki hadi unafika kipindi cha siku, sasa ili kuhakikisha malengo hayo unayafikia ndani ya mda hapo ndipo unapotafuta watu wako wakaribu na kuwashirikisha malengo yako kitendo hicho ndicho tunakiita kusambaza ukweli na malengo yako.
Watu hao ambao unaenda kuwashirikisha malengo yako anaweza kuwa kocha wako au wazazi wako au familia yako , hapa unatakiwa uwaambie ukweli kuwa kwa miaka hii kumi mimi nataka niwe nimefikia malengo fulani na kila mwaka nitakuwa napiga hatua fulani, pia kila mwezi nataka niwe nimefikia hatua fulani na kila siku nataka niwe nimetimiza lengo hili, jambo hili linamsaada mkubwa sana katika kuhakikisha wewe hausahau malengo yako lakini pia kutopenda kuwaangusha wale ambao wanakufatilia, pia pale unapotaka kukata tamaa ukiangalia kundi kubwa la watu ambao uliwahakikishia kuwa wewe utatimiza jambo hilo basi unapata nguvu ya kuendelea mbele, kitendo cha wewe kutopenda kuwaangusha wengine kwa kushindwa kwako kunakufanya ushindwe kukataa tamaa na kuendelea mbele kwa nguvu.
Ngoja twende na mfano kidogo hapa. Huenda wewe umekuwa ukiishi nyumba ya kupanga kwa mda mrefu na matamanio yako siku zote kuwa na nyumba yako mwenyewe, katika kuhakikisha unakuwa na nyumba yako mwenyewe umejaribu kila njia na ukashindwa? Naomba tumia kanuni hii namba mbili ya kujenga ushujaa katika mafanikio yako. Fanya hivi kaa chini na fikiria nyumba unayoihitaji ni nyumba ya aina gani? Pia fikiria nyumba hiyo unataka iwe maeneo gani, pia fikiria nyumba hiyo unataka uwe tayari unayo kwa kipindi gani? Na mwisho nyumba hiyo unataka iwe na vyumba vingapi? Baada ya kufikiria mambo hayo kwa kina unatakiwa kumtafuta fundi ramani mpe mwongozo wa ramani ya nyumba unayohitaji mwambie akuchoree ramani ya nyumba unayohitaji na baada ya kukuchorea ramani mwombe akusaidie akupe makadirio ya jengo unalohitaji litagharimu fedha kiasi gani, baada ya kufanya zoezi hili najua utakuwa tayari umepata picha halisi ya nyumba unayoihitaji kuwa nayo, piga hesabu kwamba gharama hizo unauwezo wa kuzimudu kwa mda gani? Huenda makadirio ya gharama ni milioni therasini au milioni ishirini au milioni kumi vyovyote iwavyo unapaswa utenge mda maalumu wa wewe kumiliki nyumba yako, panga kwawa iwayo na iwe lakini baada ya miaka mitano nataka kuwa na nyumba yangu mwenyewe, chukua rama ni yako nenda kapige picha ya nje jinsi jengo litakavyokuwa linaonekana baada ya hapo nenda kawaoneshe watu wako wa karibu inaweza kuwa familia yako au kocha wako na waambie mimi Frank mapunda kuanzia leo hadi kufikia siku fulani ya mwaka fulani nataka nitakuwa nimehamia tayari kwenye nyumba hii, na ili kuhakikisha nalitimiza hili kila mwezi nitakuwa na fanya jambo hili hapa unaandika huenda kununua bati moja kwa kila mwezi au bati moja kwa kila wiki unaandika, hivyo kila siku hakikisha unakuwa na jukumu lolote ambalo litafanya uongeze kitu katika kukamilisha lengo lako, mipango yote hiyo unapaswa kukabidhi nakala kwa kocha wako, na familia yako na kila mwezi pango siku yakuwaita pamoja na kufanyia tathmini. Rafiki nakuhakikishia hakuna lengo litakalofeli katika mfumo huu na hapo ndipo ilipo siri ya mafanikio yako.
Hivyo basi kuanzia leo panga na dhamiria kuwa unakuwa na tabia ya kusambaza ukweli na malengo yako ili uweze kupiga hataua kubwa kuelekea mafanikio makubwa.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blospot.com
0758918243
0656918243
0621049901
KWA MAARIFA ZAIDI KARIBU UJIPATIE VITABU
NGUVU YA MAARIFA
SOFTCOPY 10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
JIFUNZE , TAFAKARI CHUKUA HATUA 2021 NI MWAKA WANGU WAMAFANIKO MAKUBWA
0 Comments