Ad Code

Responsive Advertisement

USIKATE TAMAA ULIUMBWA KWA KUSUDI MAALUMU



Habari rafiki yangu, nisiku nyingine tena tumepata kibali na Mungu mimi nawewe kuiona siku hii nzuri ya leo, wala siyo kwa juhudi zetu wa matedo yetu bali nineema pekee ya Mungu kutupa kibali kuiona siku hii ya leo, chukua dakika chache kumshukuru Mungu kwa wema na Fadhila zake juu yetu. Rafiki karibu sana katika somo la leo tujifunze mambo muhimu katika maisha yetu ambayo yatatusogeza karibu zaidi na mafanikio makubwa ambayo tunayahitaji, kusudi la kila mwanadamu anayeishi hapa duniani ni kuifanya dunia kuwa mahali pazuri kwa watu kuishi hilo ndilo kusudi kuu la maisha ya mwanadamu, unafanyaje ? Ni nijinsi unavyochukua hatua sahihi kuhakikisha unatimiza kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani kwa kulifanya lililo sahihi mbele za Mungu.

USIKATE TAMAA ULIUMBWA KWA KUSUDI MAALUMU


Rafiki katika maisha ya mwanadamu kuna vipindi fulani ambavyo kama wanadamu tunapitia, kuna vipindi vingine vinakuwa vigumu sana kiasi ambacho tunatamani hata kujiondoa hapa duniania hii haimaanishi kuwa Mungu ametuacha wala haimanishi kwamba tulizaliwa kwa bahati mbaya, kila mwanadamu aliye pata nafasi ya kuzaliwa hapa duniani Mungu aliweka kusudi kubwa ndani yake, hivyo licha ya kupitia katika vipindi vigumu maishani bado tunayo nafasi yakuishi maisha yale ambayo Mungu alikusudia tuje tuishi hapa duniani. Kitu kikubwa tunachotakiwa kufafanya ni kujua kwa ni ni tupo hapa duniani kwa kulijua hilo basi hata changamoto na magumu yeyote yakitujia bado tutaona tunanafasi ya kuondoka katika magumu hayo, hivyo nijukumu lako namba moja katika maisha kujua kwanini upo hapa duniani kwakulijua hilo nakuishi maisha yanayoendana na kusudi lako kutakufanya uishi maisha yenye maana.

Kulijua kusudi la kuzaliwa kwako nijambo moja hivyo usizani kwamba wewe kwakulijua kusudi la kizaliwa kwako basi hauta kutana na magumu hapana, magumu utakutana nayo mengi sana kiasi ambacho yatakukatisha tamaa ya kuendelea mbale, basi unapokutana na hali kama hiyo hautakiwi kukata tamaa bali endelea mbele kwa nguvu, angalia mbele yako kuliko magumu yako, angalia faida ya kutimiza kusudi la kuja kwako hapa duniani kwakufanya kwa juhudi kubwa huku ukijifunza kwa kila hatua ya magumu yako basi maisha yatakuwa bora sana, ukisoma katika biblia utagundua kuwa watu wote ambao tunawaona leo kama mashujaa wakubwa hawakuupata ushujaa wao kwa wepisi bali walipitia katika magumu mengi na yakukatisha tamaa sana lakini hawakukata tamaa bali waliendelea mbele, waliangalia kusudi la wao kuletwa duniani hivyo licha ya magumu yote lakini hawakukata tamaa, ukimtazama Ibrahimu Baba wa imani ataona alipitia vipindi vigumu sana katika maisha yake lakini hakukata tamaa aliendelea kumwamini Mungu licha ya magumu yote aliyopitia,  vile vile kwa Yakobo huyu jamaa alipitia maisha magumu sana lakini hakukata tamaa bali aliendelea mbele, huku akijifunza kwa kila gumu analopitia hatimaye maisha yake yakaja kuwa bora sana, siyo hao tu kuna kijana mmoja anaitwa Yusuph huyu kijana alikuwa mpambanaji sana licha ya kutokupendwa na ndugu zake, licha ya kuuzwa utumwani licha ya kuwekwa gerezani lakini hakuwahi kukata tamaa kamwe aliamini ipo siku atafanikiwa na hatimaye akiwa ndani ya gereza anaitwa na mfalme na anaenda kupewa cheo kikubwa na maisha yake yanakuwa bora sana, sasa unaweza ukajiuliza je kama angekata tamaa maisha yake yangekuwaje, jibu ni rahisi tu katika hilo kwamba maisha yake yangekuwa magumu sana. Lakini kutokana na kutokukata tamaa licha ya magumu yote aliyopitia alikuja kuwa na cheo kikubwa sana cha uwaziri mkuu wa taifa la Misri.

Rafiki najua unapitia kipindi kigumu sana maishani mwako napenda kukwambia jambo moja usikate tamaa kiwango cha changamoto unachopitia nikutokana na ukubwa wa kusudi ambalo Mungu aliliweka ndani yako hebu leo kaa chini tafakari upendo Mkubwa wa Mungu ndani yako, anza kutazama toka ukiwa mdogo mambo mangapi ambayo wazazi wako walipitia katika kukulea kwako utakuja kugundua kuwa kuna wengi walizaliwa siku moja na wewe lakini leo hawapo hai tena, hivi wewe ni nani hadi upo hai hadi leo utakuja kugundua kuwa Mungu anakusudi na wewe hivyo  anakupigania kwa kila hatua ili uweze kuishi kutimiza kusudi la Mungu. Rafiki huenda biashara zako zimefeli, huenda familia yako imekutenga, huenda jamii yako wanakunyima nafasi ya wewe kuwa vile upendavyo, uenda kuna ugonjwa fulani unakutesa,  napenda nikwambie kuwa usikate tamaa mtazame Mungu naye atakuonyesha njia, wewe siyo wakwanza kupitia katika magumu hayo alikuwa Ayubu alipitia kipindi kigumu sana lakini hakukata tamaa licha utajiri wake wote kupotea lakini hakukata tamaa, licha ya familia yake yote kuangamia lakini hakutakata tamaa, licha ya mke wake kupoteza imani na Mungu lakini Ayubu hakata tamaa, licha ya kuugua kwa mda mrefu kwa zaidi miaka kumi na nne lakini bado hakukata tamaa, wewe ni gumu gani unapitia? Rafiki napenda nikwabie kuwa usikate tamaa ugumu unaopitia unapitia kwasababu ya ukubwa wa kusudi la Mungu kwako hivyo tumia kama daraja lakukufundisha ili uweze kufika kule ukupendako.

Rafiki tumia magumu unayopitia ili kuwa daraja la wewe kufika kule ambako unataka kufika, ipo hivi rafiki usipojifunza kwa magumu unayopitia magumu hayo yatakuwa adhabu kwako lakini ukiamua kujifunza kwa kila gumu unalopitia basi yatakuwa daraja zuri kwako kufika katika viwango vya juu vya mafanikio yako. Najua unasema "frank hujua ugumu ninao pitia mimi" nikweli sijui lakini ninauhakika magumu unayopitia ni daraja lakukupeleka viwango vingine bora sana vya maisha yako kikubwa usikate tamaa jifunze kwa kila gumu unalopitia kwa kufanya hivi na maisha yako yatakuwa bora sana siku si nyingi. Mimi mwenyewe kunakipindi nilipitia kipindi kigumu sana katika maisha yangu ya biashara niliwahi kuvamiwa na kuporwa kila kitu cha ofisi yangu kuanzia mtaji hadi afya yangu ilinilazimu nijiuguze kwa fedha za mkopo pia biashara ikashindwa kuendelea kwasababu mtaji wote nilikuwa nimeibiwa lakini sikutaka kuruhusi kukata tamaa, kila aliye niona alinionea huruma sana lakini sikukubali kuendela kubaki chini nilimwamini Mungu kuwa mimi siyo wakubaki chini nilijua kuwa hilo lilikuwa daraja lakufika kule ninakotaka kwenda na Mungu wetu ni mwaminifu sana aliendelea kuwa pamoja nami hadi nikasimama tena, jambo moja lilo nisaidia mimi nikuto kukubali kukata tamaa na kuendelea mbele, rafiki napenda nikwambie kwamba hukuzaliwa kwa bahati mbaya Mungu anafanya kazi kubwa kuhakikisha wewe unakuwa hai kwasababu kuna kusudi kubwa ambalo ameliweka ndani yako, hebu mtazame Yesu yeye alipitia vipindi vigumu sana katika maisha yako toka kuzaliwa kwake hadi kukua kwake lakini hakukubali kukata tamaa aliendelea mbele na kuangalia kusudi kubwa la yeye kuletwa duniani, hakukubali kupingwa na watu kushindwe kulimiza kusudi la Mungu kumleta duniani, hakukubali changamoto yeyote imzuie yeye kutimiza kusudi la Mungu kwake bali alipambana kuhakikisha analitimiza kusudi la Mungu. Hata wewe usiangalie idadi ya watu wanao kupinga ila jifunze kupitia hilo, hata wewe usikubali magumu unayopitia yakukatishe tamaa ya kuendelea mbele, hata kama umeibiwa mtaji wako wote wewe usikate tamaa endelea mbele na Mungu wetu  nimwaminifu sana naye atakuwa pamoja nawe hadi mwisho wa maisha yako. Rafiki leo hii nenda kuchukue hatua mpya ya maisha yako, leo hii azimia kutokukata katamaa na magumu yote utakayo kutana nayo chukua kama daraja kwako kukupeleka katika vilele vya mafanikio yako.

Ni mimi rafiki yako
Mwandishi na mwalimu wa ujasiriamali
Frank mapunda
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kwa namba
0758918243
0656918243
0786115129

KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU VITAKAVYO INUA ZAIDI MAFANIKIO YAKO

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

HARDCOPY 15000/=
SOTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE SANA KWAKUWA PAMOJA NAMI.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu