Ad Code

Responsive Advertisement

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUDHIBITI CHANGAMOTO HIZ


KONA YA UFUGAJI

SEHEMU YA KWANZA

Habari rafiki yangu mpendwa nimatumaini yangu kuwa upo salama kabisa huku ukiendelea kuchukua hatua mbalimbi kuhakikisha unafikia malengo makubwa uliyonayo katika maisha yako kama ni hivyo basi nakupa hongera sana lakini kama ni mgonjwa kiasi ambacho huwezi kuchukua hatua yeyote ya kimaendeleo kutokana na changamoto mbalimbali za kiafya basi nakupa pole sana nakuombea kwa Mungu akupenye ili upate nafasi ya kuendelea na shughuri zakuhakikisha maisha yako na yajamii yako yanakuwa bora sana
. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwakuweza kunipata nafasi hii yakipekee sana kuweza kuwa hai nanikiwa na afya njema sana kwa siku hii ya leo siyo kwamba nimetenda mema sana kuliko wengine bali ni kwaneema yake pekee,  nikuombe rafiki yangu chukua dakika chache kumshukuru Mungu kwakuwa ameruhusu mimi nawewe tuweze kuwa hai na afya njema lakini hata kama unachangamoto yeyote ya kiafya na nyingine yeyote mweleze yeye naye atatenda.

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUDHIBITI CHANGAMOTO HIZI.

Karibu sana rafiki yangu katika somo la leo, kwanza kabisa niwape pole sana ndugu zangu wafugaji wa kuku ambao wanakutana na changamoto mbalimbali ambazo zinakatisha tamaa sana katika ufugaji wa kuku, zipo changamoto nyingi katika ufugaji wa kuku lakini kwa siku ya leo nitaongelea changamoto moja ya magonjwa na siku zijazo nitaendelea kuelezea changamoto zingine na hatua za kuchukua. Katika ufugaji wa kuku kumekuwa na changamoto kubwa sana ya magonjwa hali inayopelekea wafugaji wengi wapete hasara katika ufugaji wako kutokana na kupoteza kuku wengi ambao wanakufa kwa magonjwa mbalimbali. Changamoto hii imekuwa ikiwaludisha nyuma wafugaji wengi kiasi vha kukata tamaa kabisa katika ufugaji wao. Kutona na ukubwa wa changamoto hii napenda niwape pole sana ndugu zangu wote ambao mmekutana na changamoto hii na mnaendelea kukutana nayo katika ufugaji wenu.

Kwanza nianze kwakusema kuwa kuku kuugua siyo jambo baya kabisa kwasababu kwa asili viumbe vyote vinaugua, hata sisi binadamu huwa tunaugua lakini ubaya ni kuchelewa kupata matibabu sahihi au kushindwa kupewa matibabu sahihi huu ndio ubaya wa kuugua, hii ipo kwa kuku na hata kwa binadamu pia. Mwanadamu anapougua maralia siyo kitu kibaya ila ubaya utakuja pale mwanadamu huyu akishindwa kupata matibabu sahihi ya ugonjwa ambao anaugua  hapo ndipo penye madhara makubwa. Hivyo ndivyo ilivyo kwa kuku, pale kuku anapougua na kucheleweshewa kupata tiba sahihi ndipo ilipo tatizo kubwa nakupelekea vifo vingi kwa kuku. Hivyo changamoto kubwa inayowapata wafugaji wa kuku nikushindwa kujua aina ya ugonjwa ambao kuku wanaugua kiasi kinachopelekea kuku kupewa dawa isiyo sahihi hii inawafanya kuku waendelee kuugua zaidi hadi kupelekea vifo vya kuku wengi bandani. Kuchelewa huku kuwapa tiba sahihi kunatokana na uelewa mdogo wa wafugaji napia changamoto kubwa inachagizwa na wauzaji wa madawa ya mifugo kutokuwa na dawa zenye ubora bao utasaidia kuku kuweza kupona.


NINI KIFANYIKE

Tumeona jinsi changamoto hii ilivyo kubwa, lakini kuona tatizo si ndio kusema tatizo limeisha hapana bali tunahitaji kutatua tatizi ambalo lipo ili tuweze kusonga mbele katika ufugaji wetu. Zifuatazo ni hatua za kuchukua ili kuweza kuondoka kwenye changamoto hii kubwa ambayo imekuwa chanzo cha sisi kushindwa kusonga mbele.

1)TAMBAUA DALILI ZA UGONJWA KABLA HAUJAWAATHIRI KWA KIWANGO KIKUBWA KUKU WAKO.

Kuku huwa wanakuwa na hatua kubwa tatu za ugonjwa wowote ule, hatua ya kwanza pale ugonjwa unapoingia/unapoanza kuwaathiri kuku wako. Hii  ni hatua ya awali kabisa ya ugonjwa kwa kuku hivyo nivema ukawa na utaratibu wa kuwachunguza kuku wako kila siku kujua hali zao zipoje hii itakusaidia sana kuja changamoto ambazo wanapitia hivyo kama utakuwa na utaratibu wa kuingia bandani mwa kuku na kukaa angalau dakika kumi (mda unaweza kuongezeka kulina na idadi ya kuku) kwaajiri ya kuwachunguza kuku wako itakusaidia sana kuweza kugundua hali zao hivyo kama kuna ugonjwa flani umeingia utaweza kuujua hivyo kuwahi kuwapa tiba sahihi, kwa kufanya hivi itakusaidia sana kupoteza kuku wako kwa ugonjwa kwasababu utakuwa umeuwahi ugonjwa. Kumbuka nimesema kuwapa tiba sahihi siyo kuwapa dawa,  nazungumza hivi kwasababu kama hauta wapa kuku wako dawa sahihi kulingana na ugonjwa ambao wanaugua ningumu sana kuweza kuwaponya kuku wako na matokeo yake wataingia kwenye kundi hatua ya pili ya ugonjwa. Hatua ya pili ya ugonjwa ni pale ambapo kuku wengi bandani wanaugua hapa utaona dalili za ugonjwa zimeenea kwa idadi kubwa ya kuku na pia kuku wanapoteza kabisa hali ya uchangamfu. Katika hatua hii mfugaji unatakiwa kujua aina ya ugonjwa ambao kuku wako wanaugua na kuwatafutia dawa sahihi ambayo inanguvu ya kupambana na magonjwa ambayo yameathiri kwa kuasi kikubwa. Kumbuka nimesema dawa sahihi ambayo inauwezo wakupambana na ugonjwa ambao umeathiri kuku kwa kiwango kikubwa hii nikutokana na kuwa na dawa nyingi ambazo zinatibu magonjwa kulingana na hatua ya ugonjwa hivyo naomba unielewe hapa siyo kila dawa inayouzwa dukani inatibu ugonjwa fulani wa kuku kwa usahihi hapana dawa hizi zinatibu kulingana na jinsi kuku wako walivyoathirika, hivyo tafuta dawa ambayo itakuwa na nguvu kubwa kuweza kutibu kiwango kikubwa cha ugonjwa. Na hatua ya tatu na yamwisho ni pale ambao kuku wako ugonjwa umewaathiri kwa kiwango kikubwa zaidi kiasi ambacho wameanza kufa hii ni hatua mbaya kwa kuku kwasababu katika hatua hii kuku wanakuwa wameathirika kwa kiwango kikubwa sana kutokana na kutopewa dawa sahihi za ugonjwa ambao kuku walikuwa wanaugua. Hivyo mfugaji unatakiwa kutafuta dawa sahihi ambayo itakuwa na msaada mkubwa wakupambana na aina ya ugonjwa ambao kuku wako wanaugua, hivyo unatakiwa kuwapa dawa sahihi, ila unachotakiwa kufahamu nikwamba siyo kwamba utakapoanza kuwapa dawa hiyo basi kuku wako watapona mala moja hapana bali wataendelea kufa kwa siku mbili hadi tatu na kuku ambao watakufa niwale ambao wilikuwa na hali mbaya zaidi ya ugonjwa kiasi ambacho cha kushindwa kusikia dawa.

Naomba niishie hapa kwa leo tutaendelea tena wakati mwingine katika mwendelezo wa masomo haya. Hivyo unaweza kujipatia nakala ya kitabu cha *Tajirika kwa ufugaji wa kuku* ili kunafaika zaidi na maarifa bora ya ufugaji wakuku. Pia mda si mterefu kuanzia sasa utaweza kupata masomo  haya kupita blog iitwayo *www.nguvuyamaarifa.blogspot.com* kwa maarifa mbalimbali kuhusu ufugaji wa kuku na mambo mbalimbali kuhusu maarifa yatakayo kupa ufahamu zaidi kuhusu mafanikio.

Ni mimi rafiki yako
Mwandishi na mwalimu wa ujasiliamali
Frank mapunda
0758918243
0656918243
0786115129

UNAWEZA KUJIPATIA VITABU AMBAVYO VITAKUPA MWONGOZO BORA WA MAFANIKIO

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*



HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

KAZI YANGU NI KUKUPA MAARIFA BORA YATAKAYO KUPA UFAHAMU MKUBWA KUELEKEA MAFANIKO MAKUBWA NA WEWE JUKUMU LAKO NIKUCHUKUA HATUA KWA YALE UNAYOJIFUNZA ILI MAISHA YAKO YAWE BORA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu