Ad Code

Responsive Advertisement

UNAWEZAJE KUJENGA USHUJAA KATIKA MAFANIKIO UNAYOYATAKA?

 




*SEHEMU YA KWANZA*



Rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa upo salama sana, kama ni hivyo jipe dakika chache kumwambia Mungu asante kwa kunilinda na kuniweka salama hadi sasa, (Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea ikiwa na pamoja afya njema uliyopewa)

, baada ya kumaliza kumshukuru Mungu sasa tukumbushane kidogo kaulimbiu yetu kuu kwa mwaka huu 2021 nikwamba Mwaka huu ni mwaka wa KUJIFUNZA SANA, KUTAFAKARI KWA KILA TUNACHOJIFUNZA  NA MWISHO KUCHUKUA HATUA KUPITIA YALE TULIYOYAONA BAADA YA KUTAFAKARI, Haya ni maeneo machache na  ambayo nimuhimu sana kuyafanyia kazi katika kila siku ya maisha yako. Bila kupoteza mda sasa twende tukajifunze jinsi ya kujenga ushujaa katika mafanikio tunayoyataka.


Shujaa ni mtu mwenye moyo thabiti anayeweza kukabili mambo hata kama ni yahatari. Sasa katika kujenga ushujaa katika mafanikio tunahitaji kuwa na moyo thabiti. Moyo thabiti ni usio teteleka katika kuhakikisha unapambana katika hali yeyote hadi mafanikio yapatikane. Tunaweza kuliweka somo letu katika namelezo haya nikwajinsi gani tunaweza kujenga ushujaa katika kupata mafanikio tunayoyataka? Ili kujenga ushujaa katika kupata mafanikio tunahitaji tufanya mambo matatu muhimu kuzingatia ili kuweza kujenga ushujaa ambao utatusaidia kupata mafanikio makubwa.


1~KUHESHIMU MAPAMBANO

Mapambano ni makabiliano baina ya pande mbili au zaidi katika mashindano, vita au fikira; harakati. Sasa katika kujenga ushujaa mkubwa katika eneo la mafanikio tunahitaji kuheshimu sana mapambano hayo ambayo tunaenda kupambana nayo ili tuweze kupata mafanikio makubwa ambayo ndiyo tunayoyakusudia. Jambo la muhimu lakufahamu nikuwa mafanikio yeyote nimatokeo ya mapambano yeyote na matokea chanya  kuwa upande wampambanaji hapo ndipo mafanikio makubwa yanapoonekana. Hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana bila ya mapambano na kama yapo basi mafanikio hayo yanakuwa hayajajenga kwenye msingi imara hivyo tegemea kuanguka katika mafanikio hayo, kupata mafanikio nikama vile kujenga nyumba kwamba unahitaji msingi imara ndivyo ilivyo kwenye eneo la mafanikio unahitaji uweke umsingi imara na msingi imara ni mapatokea ya mapambano ambayo mtu anakabiliana nayo katika kuweza kupata mafanikio makubwa. Hivyo wewe kama mmoja wa wasafiri katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa unahitaji kujua kuwa katika safari hii unahitaji kupambana kweli kweli na kuheshimu mapambano hayo, kama ilivyo kwa wacheza masubwi moja yakanuni muhimu katika mapambano nimheshimu mpinzani wako ndivyo ilivyo kwetu mpinzani wetu nichangamoto ambazo tutakutana nazo katika kutafuta mafanikio kitu kikubwa tanachotakiwa kukifahamu nikwamba tuheshimu changamoto na tukubali kuwa changamoto hizo tunapaswa tuzitumie kama rasilimali ambazo zitaenda kutusaidia kuweza kupiga hatua zaidi.


Jambo lingine muhimu katika mapambano haya nikuwa tunahitajika kufurahia mapambano hayo, ndio tunahitaji kufahamu kuwa mapambano haya ambayo tumeyaingia siyo mateso wala hatujaingia kwasababu tumelazimishwa hapana bali mapambano haya ni sehemu ambayo tunaipenda hivyo katika mapambano haya tunapambana kwa sababu ya upendo wetu mkubwa kwa kile tunachokipambani, ukiangilia wale wote wanaoshinda mapambano utagundua jambo moja kwa washindi wote wanaoshindwa mashindano hawashindi kama ajari bali walitengeneza katika akili zao hali ya kuyapenda mashindano hayo hivyo walijituma sana katika mapamba hayo kuhakikisha wanatetea kile wanachokipenda,  hata wewe rafiki unaweza kuwa mshindi wa mapambano haya jambo kubwa la muhimu nikuwa unatakiwa kuyaheshimu mapambano, kukubali kupambana na mwisho kuyapenda mapambano haya kwa kufanya hivyo unakuwa umekaa njia sahihi kuelekea kwenye kujenga ushujaa katika kupata mafanikio  makubwa.


Ni mimi rafiki yako

Frank mapunda

Www.nguvuyamaarifa.blospot.com

0758918243

0656918243

0621049901


JIPATIE VITABU


NGUVU YA MAARIFA


SOFTCOPY 10000/=


TAJIRIKA KWA UFUGAJI KWA KUKU


SOFTCOPY  7000/=


Post a Comment

0 Comments

Close Menu