*SEHEMU YA MWISHO*
Habari rafiki yangu mpendwa? Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema kabisa, kama ni hivyo basi sifa na utukufu zimludie Muumbaji wetu kwakuwa ameendelea kutulinda na kututunza, yote haya si kwamba sisi tumetenda mema sana hapana bali tumepata yote kwa upendeleo tu,
Baada ya salama turejee moja kwa moja kwenye somo letu muhimu sana, na kabla hatuja ingia ndani kwenye somo letu la leo naomba tujikumbushe mambo muhimu ya kutembea nayo kwa mwaka huu 2021, Mwaka huu ni mwaka ambao tunategemea uwe ni mwaka wenye mafanikio makubwa sana kwa maisha yetu na mafanikio hayo hayatashuka tu wala kuibuka kama uyoga bali yatatokana na juhudi kubwa tunazoenda kuzitenda ndani ya mwaka huu na ili kufanikisha yote haya tunahitaji kutembea chini ya maneno haya matatu ambayo ni KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA, Ndio kwa mwaka huu tumechagua kujifunza mambo yote muhimu katika maisha yetu, mwaka huu tumechagua kujifunza kupitia kusoma vitabu, mwaka huu tumechagua kujifunza kupitia kufeli kwetu, mwaka huu tumechagua kujifunza kupitia changamoto zetu, mwaka huu tumechagua kujifunza kwa kwawalio fanikiwa zaidi yetu, huu nimwaka wa kujifunza sana na baada ya kujifunza tumeamua kuchukua mda kwaajiri ya kutafakari kwa yale tuliyojifunza ili kuweza kuchukua hatua iliyo bora, hivyo basi kwa mwaka huu tunaenda kutafakari kabla ya kuchukua hatua, kwa kila mafunzo tutakayo yapata kwa mwaka huu tunaingia hatua ya pili kutafakari na kuchuja yale ambayo tunauwezo nayo au yale ambayo yana msaada mkubwa kwa maisha yetu na baada ya kutafakari kwa kina tunaingia katika hatua ya tatu ya kuchukua hatua ndio kwa mwaka huu kila hatua ambayo tunaenda kuichukua nilazima imepitia katika maeneo makuu mawili la kwanza kujifunza na pili kutafakari na mwisho ndipo hatua huchukuliwa kwa kufanya mambo hayo tunaamini mwaka huu unaenda kuwa mwaka wa mafanikio makubwa.
Baada ya utangulizi huo naomba nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye somo letu la leo, leo tunaenda kuhitimisha somo hili somo ambayo kwa hakika tulijifunza mengi nikuombe wewe rafiki yangu ambaye tulikuwa pamoja toka mwanzo wa somo hili hadi mwisho wa somo hili najua umejufunza mambo mangi, umetafakari mambo mengi na mwisho kuna hatua umechukua katika somo hili, leo naomba ujibu maswali haya ya tathmini kwa somo lote karibu sana.
KAZI YA KUFANYA
~Jambo gani ambalo umekuwa ukipambana kulifanya kwenye maisha yako?
~jambo gani umekuwa ukihangaika kulifanya kwenye maisha yako?
~Je ni njia gani unazitumia/utazitumia kuhakikisha unalitimiza jambo hilo na unategemea kupata matokeo ya aina gani?
~Mambo gani unayotakiwa kufanya kwa mwaka huu lakini haujashea kwa mtu mwingine wa aina yeyote? Na unampango gani wa kushirikisha wengine.
~Je upo tayari kupambania ndoto zako kwaajiri ya nani?
Rafiki hayo ni nimaswali machache na muhimu sana kuyafanyia kazi kwa siku ya leo na baada ya kuyafanyia kazi yaweke kwenye mchakato kuhakikisha unachukua hatua halaka iwezekanavyo.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu:- 0758918243
0656918243
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU
NGUVU YA MAARIFA
SOFTCOPY 10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
JIFUNZE, TAFAKARI NA CHUKUA HATUA
0 Comments