Ad Code

Responsive Advertisement

*NGUVU YA MWANAMKE* JE UNATAMBUA KUWA MWANAMKE ANANGUVU KUBWA YA USHAWISHI?


Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu makubwa kuwa u mzima sana,  kama nihivyo sina shaka kuwa unaendelea vizuri sana kuhakikisha unachukua hatua kuelekea kutimizi malengo makubwa uliyonayo. Ndio najua unayo malengo makubwa lakini umekubali kuanza kuyafanyia kazi kwa kuchukua hatua kidogo kidogo. Bila yakupoteza mda naomba nikupeleke moja kwa moja kwenye somo letu la leo ambalo nitaenda kuzungumza mambo machache kuhusu nguvu kubwa aliyopewa mwanamke na  Mungu. Mwanamke amepewa nguvu kubwa ya kufanya mambo makubwa sana kwakutumia akili yake siyo nguvu zake za mwili,   ndio maana mwanamke akiamua kutambua uwezo wake mkubwa alio nao anaweza kufanya mambo makubwa sana bila hata yakutumia nguvu ya mwili. Unaweza kuona hili katika Biblia kuwa kuna mwanamke mmoja aliweza kumshawishi SAMSON kumpa siri ya kitendawili chake ambacho hakuna yeyote aliyewahi kumwambia ila yeye alimwambia, pia hapo hapo unaweza kuona nguvu ya mwanamke ilivyoweza kumpa DELILA siri ya nguvu za SAMSONI vipindi vyote hivyo utaona SAMSONI anakubali kutoa siri ya nguvu zake ambazo hakuwahi kutoa sehemu yeyote ile.


Ukitambua kuwa mwanamke ananguvu kubwa ya ushawishi hebu jaribu kuandaa tukio alafu mpe mwanamke nafasi ya kuwaalika wageni na tukio lingine mpe mwanamme nafasi ya kuawaalika wageni hapo ndipo utakapoona jinsi watu hawa walivyobalikiwa kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi.  Siyo hivyo tu kuna msemo mmoja maarufu sana unasema *kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake* je umeshawahi kutafakari msemo huu,  ukiutafakari kwa kina utakuja kugundua unaukweli kwa Asilimia mia moja, lakini namimi nimekuja namsemo wangu hapa kuwa kila kufeli kwa mwanaume kuna mwanamke nyuma yake, hivi nikweli nipo sahihi hapa? Hebu nawewe tafakari alafu utapata majibu.


Kitu nilichojifunza mimi kuhusu mwanamke kuwa kipindi Mungu anamuumba mwanamke alimpa uwezo mkubwa wa akili kuliko uwezo wa nguvu za mwili hivyo iwapo mwanamke yeyote ataamua kutumia uwezo wake mkubwa naami dunia itakuwa na mafanikio makubwa sana. Hebu nawewe tafari hili mwanamke pekee anaweza kumfanya mwanaume atumie sehemu ya mshara wake wate kwa mwanamke, ni mwanamke pekee ndio mwenye uwezo wakuachanisha ndoa za watu wengi sikuhizi. Mmmh najua unajiuliza hivi ninamaanisha nini ninavyosema hivi, hebu tafakari nikwanini wafilisti waliamua kutumia DELILA katika kumtia katika mateka SAMSONI? 


Ewe mwanamke inuka sasa tambua uwezo wako mkubwa ulionao na ufanyie kazi maisha yako yatakuwa bora sana. Ukiniuliza mimi kwanini ndoa nyingi kwasasa zina shida nitakwambia kwasababu wanawake wengi hawajakubali kutumia uwezo wao mkubwa kwenye ndoa zao, hebu tafakari inakuwaje mwanaume anakuacha wewe na anaenda kumfuata mwanamke mwingine kama wewe? Mmmh! Najua utanijibu kuwa tamaa ya mwanaume lakini ukichunguza kwa undani utakuja kugundua kuwa kuna mahali mwanamke hakutumia uwezo wake ipasavyo, hebu tafakari kitu gani chaziada ambacho anafanya mwanamke mwingine kiasi cha kujengewa nyumba na wewe hununuliwi hata pikipiki? Najua utasema shida ni wanaume wenyewe tabia zao mbaya lakini hilo siyo kweli bali huyo mwanamke amegundua uwezo wake waushawishi na akamua kuutumia hali iliyopelekea kumteka mwanaume na kumfanyia mambo yote anayo fanyiwa? 


Hebu tafakari inakuwa kwenye mitandao yote ya simu wamempa mwanamke nafasi ya kujibu mteja kwamba namba unayopiga haipatimani n.k nasiyo mwanaume? 


Hebu tafakari vitu ambavyo vinaweza kumfanikisha mwanaume na mwanamke utakuja kugundua kuwa mwanamke anaweza akafanya vitu bila ya kutumia nguvu kubwa ya mwili na akafanikiwa kwa haraka zaidi kuli vitu anavyofanya mwanaume! Shida iko wapo sasa?


Shida wanawake wengi leo hajaamua kutumia uwezo wao mkubwa waliopewa na Mungu. Hebu leo ewe mwanamke tafakari umeuacha wapi uwezo wapo mkubwa ulionao?


Chukua hatua ya kufufua uwezo wako hapo ndipo yalipo mafanikio yako. Nikipata nafasi nitakuwa naeleza jinsi ya kufufua uwezo wa mwanamke ulio jificha nakuweza kufanya mambo makubwa sana.


Naomba nikuache na tafakari hii "kwasasa kuna wingi kubwa la watu wengi kupenda kuangalia season mbalimbali na season hizo zimetafsiliwa kwa kiswahi na wanaume je unadhani nini kitatokea iwapo wanawake wakiamua kutafsiri kwa kiswahili? Najiuliza nikwajinsi gani zitakavyowapiku kwa kiasi kikubwa kwa mauzo kuliko za zili zilizotafsiliwa na wanaume" najua unashangaa ndio wanawake wamebalikiwa sauti nzuri ya ushawishi sasa sauti hiyo wangeamua kuitumia katika kutafsi move je hali ingekuwaje? Mimi sijuwi ila ninachotambua zingependwa saana. 


Nimimi rafiki yako

Frank mapunda

0758918243

Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com


Post a Comment

0 Comments

Close Menu