Ad Code

Responsive Advertisement

JE UNAWEZAJE KUONGEZA UFANISI KWENYE KAZI/BIASHARA?

 




SEHEMU YA KWANZA


Habari rafiki yangu mpendwa? Karibu sana kwenye mfululizo wa masomo yetu ya nguvu ya maarifa ambayo yanaenda kutupatia maarifa mbalimbali katika maisha yetu, maarifa haya niyamuhimu sana ili kuweza kutusaidia kupiga hatua kubwa katika kuzifikia ndoto zetu. Somo la leo na mfululizo wake nilamuhimu sana kwa maisha yetu kwasababu bila ufanisi katika kazi/biashara ningumu sana kuweza kupata mafanikio makubwa hivyo nikukaribe sana katika somo hili, ili uweze kuwa na ufanisi mkubwa katika kazi au biashara unahitaji mambo makubwa matato nayo nikama yafautayo.


1-FANYA KAZI ZA MSINGI NA ZENYE KUZAA MATUNDA.


Katika biashara au kazi kuna mambo mengi sana ambayo huwa tunayafanya lakini nimambo machache sana ndio yanayochangia mafanikio kwenye biashara/kazi. Sasa katika kuleta ufanisi mkubwa kwenye biashara/kazi yako unatakiwa kutafakari na kugundua ni mambo gani ya msingi sana kufanya ambayo yanachangia mafanikio kwenye kazi au biashara yako. Hili linahitaji umakini sana katika maisha yako ya kazi na biashara kwasababu kama utashindwa kugundua hili utajikuta unafanya kazi kubwa sana kwenye biashara/kazi yako lakini mambo yote hayo hayaleti ufanisi mkubwa katika eneo lako la kazi/biashara. 


Sasa ili kuzuia upotevu wa nguvu na mda ambao unautumia kwenye kazi au biashara yako basi unatakiwa ufanye tathmini ya mambo ambayo niyamsingi na yenye kuleta matunda chanya kwenye biashara yako.


Hili la kuchagua kazi ya msingi na yenye kuleta matunda kama litafanyiwa kazi kwenye biashara/kazi tutafanya kazi/biashara zetu kwa ufanisi mkubwa, hata kwa upande wa bidhaa katika biashara fanya tathmini kugundua ni bidhaa gani ambazo nizamuhimu na zenye uhitaji mkubwa kwa wateja wako hizi ndizo zakuziwekea kipaombele kikubwa katika biashara yako, hivyo hivyo kweye kazi kuna majukumu mengine ambayo niyamuhimu ambayo ukiyafanya yanaleta ufanisi mkubwa kwenye kazi yako hayo ndiyo unatakiwa uyape kipaombele kikubwa ili uweze kuongeza ufanisi kwenye kazi zao. Hili lipo kwenye kila eneo la maisha yako kuanzia kazi, biashara na maisha ya kawaida. 


Hivyo basi kwa siku ya leo kaa chini tafakari katika kazi/biashara yako ni kazi gani za msingi kufanya na ukifanya basi zinaleta ufanisi mkubwa basi focus kwenye eneo hili, wekeza nguvu zako kwenye eneo hilo, elekeza uwekezaji wako kwenye eneo hilo, kwakua hapo ndio kulipo nakii na mafanikio yako acha kupoteza mda kufanya kila kitu hata kama hakina umuhimu kwenye biashara yako na badala yake chagua mambo machache yamsingi kufanya na mambo hayo yawe niyale yenye kuleta matunda chanya kwenye biashara/kazi yako.


Pia katika kuchagua kazi ya msingi na yenye kuzaa matunda kwa ukuaji wa biashara yako unatakiwa kuzingatia pia mda sahihi wakufanya kazi hiyo, na hapo ndio utakapokuwa na jukumu la kufahamu wewe wakatika gani unakuwa katika ubora mkubwa wa kuzalisha matokeo chanya kwenye biashara yako na kuelekeza nguvu zako kufanya mambo hayo ya msingi na yamuhimu tu kwenye kazi/biashara yako kwa kufanya hivyo utaongeza ufanisi mkubwa kwenye kazi au biashara yako.


2-TENGENEZA RAMANI YA MALENGO YAKO ISIYOZIDI HATUA TANO.


Hapa unatakiwa uwe na malengo yaliyopangiliwa kukamilika katika mda fulani, hii nikwasababu kuwa kijambo ambalo limewekewa ukomo wa mda kutika kukamilisha linafanya kwa ufanisi mkubwa na kwawakati kuliko jambo ambalo halijawekewa ukomo wa mda, wewe unaweza ukawa shahidi mkuu katika hili chukulia mfano kazi bosi kaacha maagizo kuwa inapofika siku fulani basi kila mfanyakazi anatakiwa awe amekabidhi ripoti yake yakazi, baada ya kuweka siku ya mwisho yakukamilisha zoezi lakukusanya ripoti hapo ndipo utakuta watu wakobise zana kuhakikisha wanalitimiza hilo kwa wakati hivyo ndivyo ilivyo kwenye biashara na kazi ili uweze kuongeza ufanisi mkubwa katika kazi/biashara unatakiwa kutengeneza ramani  sahihi yenye malengo yasiyozidi hatua tano zakuchukua. 


Unaweza kujiuliza kuna umuhimu gani wa kutengeneza ramani kwenye biashara/kazi. Au ramani nikitu gani?  Ramani ya malengo yako nitaswira picha ya wapi unataka kufika, sasa kwenye biashara/kazi uanatakiwa utangeneze ramani ambayo itakupa picha sahihi ya nini unatakiwa kufanya na kwanamna gani unaweza kupata mafanikio juu ya jambo hilo, sasa unapokuwa na ramani yenye malengo yakukuonesha nimambo gani yakufanya/ nihatua gani zakuchukua kwenye majukumu yako ya kazi/biashara itakusaidia sana kuongeza ufanisi kwa kiwango kikubwa sana kwenye kazi au biashara yako.


Hapa unatakiwa uwe umejiweka malengo fulani ambayo unatakiwa uwe umeyatimiza ndani ya mda fulani kabla ya kuanza kufanya majukumu yako, malengo yako ndio yatakupa uelekeo sahihi wa hatua zakuchukua kuhakikisha unafanya kazi/biashara yako kwa ufanisi mkubwa.


Hivyo basi nikusii sana wewe rafiki yangu kuwa leo unapoelekea kazi hakikisha kabla ya kufanya kazi yeyote uwe tayari umetengeneza ramani ya malengo ambayo unatakiwa kuyatimiza ndani ya mda husika,  na hapo sasa unaweza kuweka malengo ya mwaka mmoja hadi miaka kumi lakini hautakiwi kuishia hapo bali unagawa malengo yako kwa vipindi mfano miezi sita, miezi mitatu, mwezi mmoja, wiki moja na siku moja. Hivyo kila siku unatakiwa kufahamu majukumu ambayo unatakiwa kuyatimiza ndani ya siku husika. Na unapofika katika sehemu husika kwa maana ya kazi/biashara acha kushughurika na majukumu ambayo hayapo ndani ya malengo bali fanya yale tu yaliyopo ndani ya ramani yako ya malengo ambayo ulijiwekea. Jambo la muhimu zaidi katika eneo hili nikuwa na mda wakufanya tathmini baada ya kumaliza majukumu yako yasiku husika na kupanga/kujikumbusha majukumu yako ya kesho. Hapa jambo la muhimu pia nikufanya majukumu yako kwa ubora wa hali ya juu zaidi kuliko jana, ndio kila siku dhamiria kwamba leo nitafanya kwa ubora wa hali ya juu kiliko jana hii itakusaidia sana kuwa na  ufanisi mkubwa kwenye biashara/kazi yako hali itakayopelekea kukupa mafanikio makubwa kwa maisha yako ya kazi/biashara.


Kwa leo nenda kayafanyie kazi mambo hayo mawili, na iwapo unachangamoto yeyote kuhusiana na mambo hayo basi usisite kunitafuta ili tuweze kuwekana sawa.


Ni mimi ninayejari mafanikio yako

Frank mapunda

Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com

0758918243/0621049901/0656918243


KARIBU UJIPATE NAKALA ZA VITABU VITAKAVYOKUPA  MAARIFA ZAIDI


NGUVU YA MAARIFA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu