SEHEMU YA PILI
habari rafiki yangu mpendwa? Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwakuendelea kutulinda na kutuweka salama mimi na wewe, hii siyo kwa uwezo wetu wala kwa matendo yetu Bali nikwaneema tu.
Pili nikushukuru wewe rafiki yangu mpendwa ambaye ulikubali kuungana nami katika kusafiri pamoja katika safari hii nzuri ya miezi sita ya kuisoma Biblia, kuitafakari yale ambayo tunajifunza pamoja na kuchukua hatua, leo kwa Neema ya Mungu nimehitimisha kitabu cha 2Samweli na kesho kwaneema ya Mungu tutaanza kitabu cha 1Wafalme, najua safari itakuwa na changamoto nyingi lakini naomba nikutie moyo rafiki yangu safari tutaifikia na kuimaliza salama kabisa, najua safari shetani atajari kila namna kuhakikisha hatufikii mafanikio lakini tunaye Mungu aliyeupande wetu atatupigania, rafiki unajua kwanini napata ujasiri wakukwambia hii safari tutaimaliza salama na ndani ya miezi tunaimbaliza bila shida nikwasababu jambo tunaloenda kulifanya nijambo jema sana mbele za Mungu kwasababu tunaendelea kujifunza kupitia neno lake au tunaweza kusema tunaenda kujifunza kwake hivyo kwakuwa tumekubali kwenda kujifunza kwake basi atatupa nguvu ya kuendea.
Katika kuhitimisha katika kitabu hiki cha 2Samweli tunaweza kuwa tumejifunza mambo mengi makubwa kupitia kwa mpaka mafuta wa Bwana (mfalme daudi) kupitia mfalme huyu tumepata kujifunza hekima nyingi sana kupitia kwake na moja ya jambo kumbwa sana ambalo tunaweza kuondoka kutoka kwenye kitabu hiki nikumtanguliza Mungu.
Daudi katika kipindi chake chote cha maisha yake alipenda kuwa karibu na Mungu, na pale alipoona amemkosea Mungu alijinyenyekeza kwake na kumwomba msamaha, lakini hakuishia hapo tu daudi anasifa moja kubwa ya kumpa sifa na utukufu Mungu, mafanikio yote aliyapata katika kushinda vita vyote vigumu alijua siyo kwa uwezo wake bali ni kwanguvu za Mungu.
Kwakua daudi alimtegemea Mungu kwakila jambo Mungu alikuwa upande wake kwakila changamoto.
NI HATUA GANI TUNAENDA KUCHUKUA
Kuanzia dhamiria kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, iwe kwenye raha na taabu mwombe Mungu, mfanye Mungu awe kiongozi wako, kwenye Biashara zako Mfanye Mungu kuwa upande wako, kwenye Ndoto yako Mfanye Mungu kuwa kiongozi wako, kwenye changamoto zako Mwombe Mungu na akupiganie naye atakupigania kwenye kila eneo la Maisha yako Mtangulize Mungu.
Baada ya kumfanya Mungu kuwa wakwanza maishani mwako, kwenye kila ushindi Mpe sifa na utukufu yeye, unapopata mafanikio kwenye jambo lolote mtukuze Mungu, Asubuhi ukiamka Mshukuru Mungu, unapokuwa kwenye kazi zako Mshukuru Mungu , unapoludi nyumbani salama mshukuru Mungu, mdomo wako ujae shukrani, moyo wako ujae Shukrani, unapokuwa mtu washukrani unakuwa mtu wa furaha, unapokuwa mtu wa shukrani unakuwa mtu wa mafanikio hivyo kuanzia leo anza kuwa mtu wakushuku.
Ninapomalizia somo hili nikuombe tusome pamoja
2SAMWELI 22 huu ni wimbo wa Daudi baada ya Mungu kuwa pamoja naye katika kila hatua ya maisha yake
Biblia Habari Njema 2 Samueli 22:1,3-7 Daudi alimwimbia Mwenyezi-Mungu maneno ya wimbo ufuatao siku ile Mwenyezi-Mungu alipomkomboa mikononi mwa adui zake, na mkononi mwa Shauli. Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu. Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa adui zangu. “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; kamba za kuzimu zilinizinga, mitego ya kifo ilinikabili. “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu; nilimwita Mungu wangu. Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu, kilio changu kilimfikia masikioni mwake. (Huu ni baadhi ya utamu wa kitabu hiki kiitwacho Biblia mwone huyu mfalme alivyo na hekima kwakujua mafanikio yote hayajatokana na uwezo wake bali ni Nguvu za Mungu ndio zilizosababisha ushindi katika kila vita)
Nimimi rafiki yako
Frank mapunda
0758918243
0656918243
0621049901
Www.nguvuyamaarifa.blospot.com
USIKOSE KUSOMA BIBLIA KILA SIKU ANGALAU KURASA SABA KWA SIKU ILI INAPOFIKIA TAREHE 17/07/2021
0 Comments