SEHEMU YA PILI
Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema kabisa kama ni hivyo basi nijambo bora kumshukuru Mungu aliyenipa nafasi mimi na wewe kuwa salama lakini pia hata kama haujawa vizuri sana kiafya bado unayonafasi ya kumshukuru Mungu kwasababu hadi unaweza kusoma ujumbe huu basi ujue Mungu anaendelea kukupigania. Yote kwa yote napenda kukukaribisha sana katika mwendelezo huu wa masomo haya ya nguvu ya maarifa ambayo yanatupa nafasi kutafakari na kuchukua hatua sahihi kuelekea kwenye kilele cha mafanikio makubwa katika maisha yetu.
Kabla hatujaendelea mbele sana nikukumbushe kaulimbiu yetu kuu ya mwaka huu 2021 ni *kujifunza, kutafakari na chukua hatua* haya ni mambo matatu ambayo nimuhimu sana kuyazingatia kila siku ya maisha yetu, kwenye jambo lolote na hatua yeyote kabla haujafikia hatua ya kuchukua hatua jipe nafasi ya *kujifunza, kutafakari na kuchukua hatua* kwa kifupi maneno hayo tunayaita *KKK* hivyo baada ya kujifunza hapa katika somo hili jipe nafasi ya kutafakari ili kujua somo hili linawezaje kukusaidia katika kuboresha kazi/biashara yako, baada ya kutafakari basi nenda hatua ya tatu ya kuchukua hatua ambayo itakuwa na manufaa chanya kwenye kazi/biashara yako. Karibu sana twende pamoja.
Kwa siku ya jana tulijifunza njia kubwa mbili za kuongeza ufanisi kwenye kazi/biashara zetu na leo tutaenda kujifunza njia moja ya mwisho yakuongeza ufanisi kwenye kazi/biashara yetu.
3~JENGA UHODARI WA KUPINDUKIA KATIKA VIPAJI/TAALUMA YAKO.
Kujenga uhodari wakupindukia ni kuweza kujua kwa undani kuhusu kazi au biashara yako, kwakuweza kuijua biashara yako kwa undani basi unatakiwa kujenga ubobezi kwenye eneo hili lakazi au biashara ambayo unaifanya, katika kuhakikisha unakuwa bora zaidi katika eneo lako unatakiwa utumie vipaji vyako au taaluma yako kujifunza kwa undani zaidi ili uweze kuielewa zaidi biashara yako kwa undani zaidi.
Twende kwa mifano kidogo, wewe ambaye umeamua kuwa mfanyabiashara wa chakula basi kitendo cha kuamua kuwa mfanya biashara wa eneo ujue unajukumu kubwa kujifunza kwa undani ili uweze kuelewa zaidi nia sahihi zakuandaa chakula bora ambacho kitapendwa na wengi, sasa safari hii ya kuwa mbobezi (hodari kupindukia) katika eneo hili haiji mala moja bali nimchakato ambao mtu husika anaamua kuupitia ili kuweza kufanya biashara hiyo kwa ubora wa hali ya juu sana. Hapo ndipo mfanyabiashara huyu anahitaji kujifunza mbinu bora za kuandaa chakula bora, mbinu bora za jinsi ya kuhudumia wateja, mbinu bora zakuweka mazingira bora kwa wateja nakadhalika, hivi nivitu vyamsingi sana katika biashara yeyote ambayo mtu anaifanya, iwapo utashindwa kujenga uhodari kupindukia katika kile unachokifanya basi ujue utakuwa mtu wakubadilisha biashara mala kwa mala, rafiki unapoamua ufanya biashara fulani hakikisha unajifunza kwa wengine nakutengeneza uhodari mkubwa katika biashara yako. Kwasasa biashara nyingi zimekosa uhodari, kazi nyingi zimekuosa uhodari hali inayopelekea wafanyakazi na kwawafanyabiashara kusema hali ni mbaya na biashara hazitoki, rafiki napenda nikumbie kuwa tatizo siyo biashara uliyoichagua bali tatizo ni wewe haujaweka uhodari katika biashara yako.
Ngoja nikupe mfano hai kwangu mwenyewe, kipindi naingia kwenye secta ya ufugaji nikiwa na maarifa machache sana nilipata changamoto kubwa sana kwenye ufugaji kuku walikuwa wanaugua sana na pia kuku walikuwa wanakufa sana hali ili iliyopelekea kupata hasara kubwa katika ufugaji wangu, lakini sikukubali kukata tamaa bali nilitafuta tatizo ni nini mbona wengine wanafanya ufugaji na wanafanikiwa na mimi kwanini nafeli hapo nikaja kugundua kuwa wale wanaofanikiwa wanamaarifa ambayo mimi sina ndio maana wao wanafanikiwa na mimi ninafeli basi nikaondoka nalengo kuu kuwa nataka nijifunze ufugaji kwa undani ili niweze kuwa hodari kupindukia katika eneo hili ndio nilipotafuta maarifa kwa vitendo na kujifunza sana ilinichukua miaka mitano kuweza kujua ndani nje kuhusu ufugaji wa kuku hapo ndipo nilipoingia tena katika secta hii ya ufugaji nikiwa na nguvu kubwa ya kufanya mambo kwa ubora wa haki ya juu sana.
Nini nataka nikwambie wewe rafiki yangu? Wewe unaweza kufanya makubwa katika kazi/biashara yako kikubwa unachohitaji nikujua unataka uwe hodari kupitia nini nabaada ya kujua basi ingia ndani nenda kajifunze kweli kweli kupitia eneo ambalo unataka kuwa bora sana na inawezekana kabisa wewe kuwa hodari sana kwenye kazi/biashara. Najua uwenda unasema mimi nimeshakuwa mbobezi kwenye biashara yangu kwasababu nimefanya biashara/kazi kwa mda mrefu, hapana siyo kweli mda wakufanya kazi siyo kigezo chakuwa mbobezi kwenye eneo hilo bali kujifunza kwako nakuchukua hatua bora ndiko kutakako kupa ubobezi wa eneo lako.
Hatua ya kuchukua sasa, hebu tafakari katika biashara/kazi unayoifanya je umekuwa hodari kupindukia? Je ubora ulionao unadhani unatosha kukupa mafanikio makubwa? Je unadhani kuna haja ya wewe kujiboresha zaidi? Baada ya kupata majibu basi nenda kachukue hatua.
Ni mimi ninayejari mafanikio yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blospot.com
0758918243
0656918243
0621049901
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU
NGUVU YA MAARIFA
SOFTCOPY =10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
0 Comments