HITIMISHO
Habari rafiki yangu mpendwa, nimatumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema kabisa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa neema ya uzima kwasababu siyo kwa juhudi zetu wala siyo kwa matendo yetu bali nikwaneema tu hivyo tumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, bila ya kupoteza mda twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo, na leo tunaenda kuhitimisha somo ambalo tulilianza siku chache zilizo pita karibu sana rafiki yangu mpendwa.
KAZI YA KUFANYA
~Nikazi gani za msingi ambazo unatakiwa kufanya ili ziweze kuleta mafanikio makubwa.
~Ni mambo gani ambayo unatakiwa uache kufanya ili mda wako mwingi uwekeze kwenye mambo ya msingi yenye kuleta mafanikio?
~je unalengo gani kubwa ambalo unalifanyia kazi miaka mitano, miaka mitatu, mwaka mmoja, miezi sita, mwezi, wiki na siku ya leo?
~Ni watu gani ambao wamefikia mafanikio makubwa katika eneo hilo ambalo wewe unalifanyia kazi?
~Ni mda gani unatakiwa uwe tayari umekamilisha (umetimiza malengo yako)
~je ni mambo gani ambayo ulikuwa unayafanya lakini kwasasa unatakiwa uyaache ili uweze kuwekeza nguvu zako zote kwenye eneo.
~je nimambo gani ambayo siyo sahihi na siyo muhimu ambayo ulikuwa unafanya na sasa unatakiwa uyaache?
~je unatakiwa ujenga uhodari katika eneo/taaluma gani?
~Ni hatua zipi unatakiwa kuzifuata ili uweze kujenga uhodari katika Taaluma yako?
~je ni nani unaoweza kuwafuata na wakakusaidia kuweza kuongoze ufanisi na uhodari katika kaz/taaluma yako?
Rafiki haya ni maswali muhimu sana yakukiuliza kabla hatujaingia katika somo lingine hivyo kaachini, chukua kidaftari chako na jiulize hayo maswali na kujipatia majibu.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blospot.com
0758918243
0656918243
0621049901
0 Comments