Ad Code

Responsive Advertisement

JE UNAWEZAJE KUJENGA UONGOZI WENYE USHAWISHI KWENYE SAFARI YA MAFANIKIO YAKO?

 SEHEMU YA KWANZA



Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema kama na kama nihivyo basi nijambo la kheri kumshukuru Mungu kwa mbaraka wake mkubwa wa uzima ambao anaendelea kutujalia sisi tulio watoto wake.


Napenda kuchukua nafasi hii nzuri kukukaribisha sana katika kuendelea kujifunza mafundisho mujimu sana katika safari yetu ya kuelekea mafanikio makubwa, kabla ya kuendelea mbele napenda nikukumbushe kauli mbiu yetu ya mwaka huu 2021 inayosema KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA (KKK), kauli mbiu hii inatukumbusha wajibu wetu mkubwa kwa mwaka huu 2021 nikujifunza sana kwenye kila eneo la maisha yetu, kwenye kila changamoto ambazo tutakutana nazo kwenye kila magumu tutakayo kutana nayo kuna mambo tutajifunza kupitia changamoto, magumu, mafanikio nakadhalika, pia hatuta ishia kujifunza tu bali tunaenda kutafakari kwa kila ambacho tutaenda kujifunza ili kupima nikwanamna gani tunaweza kuchukua hatua ambazo zitakuwa na manufaa, lakini hatutaishia kutafakari pekee bali tutaenda kuchukua hatua zinazohitajika kuchukuliwa baada ya kujifunza na kutafakari. Haya nimambo muhimu sana kufanya kwa mwaka huu 2021 ili mwaka unapomalizika basi tuwe tumepiga hatua kwa kiwango kikubwa sana na inawezekana. 


Kabla ya kupoteza mda naomba niende moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo imbayo inasema *je unawezaje kujenga uongozi wenye ushawishi kwenye safari yamafanikio yako?


Uongozi ni madaraka aliyopewa mtu kusimamia shughuri au asasi na kiongozi ni mtu anayesimamia au kuelekeza watu au kikundi cha cha watu wafanye kazi au shughuri  fulani. Sasa katika safari yakujenga uongozi wenye ushawishi ili kuleta mafanikio makubwa kuna mambo matatu kama kiongozi anatakiwa afanye ili kuweza kuleta mafaniko makubwa. Kumbuka kiongozi yeyote jukumu lake kuu nikusimamia na kuelekeza watu wafanya kile kilicho sahihi hivyo kama kiongozi utakosa njia sahihi ya kuweza kuwashawishi wale unaowaongoza ningumu sana kuweza kupata mafaniko makubwa katika uongozi wako.


MAMBO MATATU YANAYOTAKIWA KUFANYWA NA KIONGOZI ILI KUWEZA KULETA MAFANIKIO BORA KWA WALE ANAEWAONGOZA KATIKA ENEO LOLOTE.


1~WAFUNDISHE NAMNA BORA YA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALIVYOKUWA WANAFIKIRI.


Ndio kazi kubwa ya kuiongozi yeyote nikutengeneza mfumo bora kwa wale anao waongoza na moja ya jambo la muhimu na lakwanza kufanya kama kiongozi nikuhakikisha unawafundisha namna bora yakufikiri kuhusu kazi wanayoenda kuifanya. Jinsi ya kufikiri kunaathiri kwa kiwango kikubwa sana mafanikio ya biashara au taasisi yeyote hivyo wewe kama kiongozi unapopewa nafasi ya uongozi jukumu lako kuu na namba moja kufanya nikuwafundisha namna bora wanavyotakiwa kufikiri kuhusu kazi wanayoifanya.


Kwakawaida watu wengi wanapoingia kwenye kazi wanapunguza uwezo wao wakujiamini, watu wengi wamekuwa wanadhana tofauti sana kuhusu wao wwnyewe, hivyo jukumu lako kama kiongozi nikuhakikisha unawajengea wale unaowaongoza uwezo wa kujiamini zaidi. Wewe kama kiongozi unajukumu kubwa kuwasaida wale unaowaongoza kufikiri tofauti na wao walivyokuwa wanafikiri. Na moja ya njia nzuri yakuwasaidia wale unaowaongoza nikuonesha kuwa unawaamini na unaamini uwezo wao hivyo hata pale unapoitaji kutoa maelekezo unatakiwa kutumia lugha ambayo haitawaondolea wao uwezo wa kujiamini bali utawapa nafasi ya kufikiri kwanamna tofauti na walivyokuwa wanafiri. Mfano unaweza kutumia lugha kama hizi pale unapotaka kutoa maelekezo, Unaonaje kuhusiana na jambo fulani, hebu fikiria kwa namna hiyo unafikiri nini kitatokea? Hapa imemjengea yeye uwezo wa kujiamini zaidi kwasababu ameoneshwa anaweza tofauti kama ungeamua kutumia neno lingine. Pia unaweza kutumia lugha hii hebu fikiria kwa namna hii, unafikiri kitatokea kitu gani kama tutaamua kufanya jambo hili?, kulingana na jambo hili kwa eneo hili unadhani tufanye nini?, unaonaje kama jambo hili likafanyika kwa namna hii. 


Maswali kama hayo yanasidia sana kwa wale unaowaongoza wewe kujenga kujiamini zaidi tofauti na ungekuwa unatumia lugha yakutothamini uwezo wako. Hivyo wewe kama kiongozi nimuhimu kuwaongezea uwezo wakujiamini sana nakuwaondolea hofu katika majukumu yao. Mfano mzuri nipale wachini yako unapoona wamefanya makosa ambayo yanagharimu biashara yako haupaswi kuwakaribia bali jaribu kuwafanya wafikiri tofauti na makosa waliyoyafanya. Hivyo basi wewe kama kiongozi wale wachini yako unapogundua wamefanya makosa unatakiwa wewe kama kiongozi kuwasaidia kwa kuwafundisha njia sahihi yakufanya ili wasiweze kufanya makosa tena. Kitendo hiki nikidogo sana lakini kinathamani kubwa sana katika kuongeza ufanisi wa wafanyakazi wako.


Mfano mwingine nipale mfanyakazi wako anapofanya maamuzi ambayo yameigharimu biashara yako, hapa wewe kama kiongozi haupaswi kuwakalipia kwasababu kwakufanya hivyo hautaweza kusuluhisha tatizo lisiweze kujiludia tena na badala yake unaweza kutumia mbinu hii ya kumwonesha jinsi makosa ambayo yameigharimu biashara na nini wameweza kujifunza kupitia tatizo ambalo limetokea. Unaweza kujifunza zaidi kupitia funzo hili "Siku moja mwanafunzi aliludi nyumbani kutoka shule na mtihani wa hesabu ambao alikuwa amefeli, kutokana na kufeli kwake mtihani ule mwanafunzi huyu aliumia sana, hivyo njia nzima alikuwa anatafakari adhabu ambayo atapewa na baba yake kama adhabu ya kufeli kwake, lakini kitu chatofauti sana alichokikuta mwanafunzi huyu nibaada ya kumpa Baba yake mthiani ule  alishangaa kuona uso watabasamu kwababa yake, mtoto alifikiri adhabu inafuata baada ya kufeli kwake mthiani ule lakini kwa upande wa Baba hali ilikuwa tofauti hakuwa katika hali ya hasira na wala hakuonesha hasira zake badala yake alionesha furaha yake baada ya kupokea matokea yake jambo ambalo lilimstaabisha sana mwanafunzi yule, kitendo kila cha Baba yake kuonekana kutokuwa na hasira wala nia yakumpa adhabu kilimpa funzo kubwa sana yule mwanafunzi, Baba yake anamwita mwanafunzi yule (ambaye ni mtoto wake) nakumweleza nimefulahi sana kuona matokeo haya ukiwa umefeli naamini kupita kufeli huku utakuwa umejifunza mafunzo makubwa sana juu ya masomo yako hivyo unapaswa ufikiri tifauti na ulivyo kuwa unafikiri kwamba masomo nimepesi kiasi kile, unapaswa ujue kwamba unapaswa kuongeza juhudi kubwa ili kuweza kupata matokea makubwa kwa siku zabaadae, unapaswa ufikiri nikitugani kimekufanya ufeli, hivyo chukulia kufeli kwako leo nifursa ya wewe kujijua vizuri na kujua udhaifu wako ulipo nakuufanyia kazi mapema iwezekanavyo, hivyo mwanangu usiumie kwakufeli kwako leo bali uumie kwa kufeli kwako tena (kama utafaeli kwa mala ya pili ndio uumie) hivyo kupita kufeli kwako leo unapata kujifunza mambo mengi yatofauti na yamuhimu sana tofautu na ulivyokuwa unafikiria. Hivyo mwanangu kila siku kuanzia sasa anza kufikiria matokeo mazuri kwa mithiani mingine iliyo mbele yako, kufeli kwako leo kuwe funzo na chachu ya kufauli kwa siku zijazo" maneno hayo ya Baba kwamwanafunzi huyo yalikuwa na msaada mkubwa sana ali iyoyepelea mwanafunzi huyu kufanya vizuri sana kwenye masomo yake ya mbele.


Mfano huu unakuhusu na wewe kama kiongozi pale watu wachini yako unapowaona wamefanya makosa haupaswi kuwakaripia badala yake unapaswa ukae nao nakuwapanafasi yakujifunza kupitia makosa ambayo wameyafanya.


Katika uongozi unapaswa kuwafikiria wengine (wale unaowaongoza) vizuri, hivyo achana na fikra kwamba wewe nibora kuliko wengine au achana na fikra kwamba hao unaowaongoza hawawezi kuelewa,  kwakuwa na fikra za aina hiyo zitakufanya ushindwe kuwa na mawasiliano/mahusiano  mazuri na hao unaowaongoza kwasababu unawafikiria vibaya. Hivyo jukumu lako kubwa kama kiongozi nikuwafikiria vizuri wale unaowaongoza, hivyo fikiri kuwa mtu yeyote anaweza kufanya vizuri kuliko wewe na hiyo nafasi umeipata wewe siyo kwamba wewe nibora sana kuliko wengine bali umeipata wewe kwasababu ilitakiwa apatikane mtu mmoja kati ya wengi. Hii itakusaidia sana kama kiongozi kuwafundisha wale unaowaongoza njia bora yakutimiza majukumu yao kwa ubora zaidi.


Mimi rafiki yako katika safari ya mafanikio

Frank mapunda

Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com

0758918243

0656918243

0621049901


KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU


NGUVU YA MAARIFA

SOFTCOPY 10000/=


TAJIRIKA KWA UFUGAJI WAKUKU

SOFTCOPY 7000/=


Post a Comment

0 Comments

Close Menu