SEHEMU YA PILI
Habari tafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa u mzima wa Afya njema kabisa, kama nihivyo basi niwajibu wetu kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuweza kutulinda hadi wakati huu tukiwa salama kiasi ambacho tumeweza kukutana tena kwenye somo la leo,
Napenda nichukue nafasi hii nzuri kukukaribisha sana kwenye somo la leo lakini kabla hatujazama ndani ya somo la leo naomba tujikumbushe kaulimbiu yetu ya mwaka huu wa 2021 mwaka wamafanikio makubwa kama tutachukua hatua, kauli kuu ambazo tunatembea nazo kwa mwaka huu ni KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA, ndio kwenye kila siku ya maisha yetu tunaenda kujifunza mambo mapya, na baada ya kujifunza tunaenda kutafakari kupitia mafunzo tunayoyapata na mwisho tunaenda kuchukua hatua juu ya yale tuliyojifunza na kutafakari, mambo haya matatu nimuhimu sana kudumu nayo katika maisha yetu kwasababu kama tutashindwa kujifunza mambo mapya maisha yetu hayatakuwa na utofauti na siku au miaka mingine iliyopita, hivyo ni wajibu wangu na niwajibu wako kila siku kujifunza mambo mapya, kwenye kila changamoto inayokukuta katika maisha yako kabla ya kuchukua hatua jipe nafasi yakujifunza baadae tafakari juu changamoto hiyo na aondoka na mafunzo ambayo umejifunza kutokana na changamoto hiyo na mwisho nenda kachukue hatua kulingana na tafakari njema uliyoipata.
Bila ya kupoteza mda sasa twende moja kwa moja kwenye mwendelezo wa somo letu lilopita ambalo tulikuwa tunajifunza njia sahihi zakujenga uongozi wenye ushawishi kwenye safari yetu yamafanikio makubwa, na katika somo hilo tulijifunza jambo kubwa moja ambalo lilikuwa linasema wafundishe namna bora yakufikiri tofauti na walivyokuwa wanafikiri, naamini katika somo lilopita ulipata nafasi ya kujifunza kwa kila lakini kama hukupata nafasi hiyo basi ingia www.nguvuyamaarifa.blogspot.com utakutana na sehemu ya kwanza ya somo hilo. Leo tuananda kujifunza mambo mawili muhimu ambayo yanakiwa kufanywa na kiongozi ili kuweza kuleta mafanikio bora kwa wale anayewaongoza.
2~WAPE CHANGAMOTO YA WAO KUKUA.
Hapa wewe kama kiongozi unapawa kuwapa nafasi wale unaowaongoza nafasi yakutumia ubunifu wako kuhakikisha wanafanya yaliyo bora zaidi kwenye biashara yako, hii nikutokana na ukweli kuwa kila mwanadamu anaubunifu wake katika jambo lolote hivyo wewe kama kiongozi unapaswa kujua ubora wa wa wafanyakazi wako na kuwapa nafasi kuonesha ubunifu wako ila wasitoke nje ya maadali ya kazi, pia wewe kama kiongozi wafundishe wale unaowaongoza maadili ya kazi zao, hili nijambo bora sana katika kuhakikisha unakuwa na wafanyakazi bora kwa biashara/taasisi yako, maadili yanamchango kubwa sana katika kuleta mafanikio makubwa katika biashara au kazi yeyote ile.
Wafundishe njia sahihi yakuwa wazungumzaji mbele zawatu, wewe kama kiongozi unawajibika kuwafundisha mala kwa mala wale unaowaongoza njia sahihi zakuwa wazungumzaji bora mbele za watu, hii nikutokana na ukweli usipingika kuwa mazungumzo bora kwenye biashara nikama roho ya biashara hivyo kama mteja atakuja kwenye biashara yako na akashindwa kupokelewa vizuri kwa mazungumzo mazuri nirahisi sana kupoteza wateja kwenye biashara yako.hivyo wewe kama kiongozi numuhimu kuhakikisha kuwa wale unaowaongoza wanakuwa bora zaidi katika majukumu yako ikiwa na pamoja na kuzalisha thamani zaidi katika kazi/biashara.
3~KUWA MFANO HAI KWAKO
Wewe kama kiongozi unapaswa kuwa kio kwa wafanyakazi/kwa wale unaowaongoza, hapa unapaswa kuwa makini sana na tabia zako hapa unapaswa wewe kama kiongozi kuwa mfano bora kwa wale unaowaongoza kwasababu nirahisi sana mtu kujifunza kupitia matendo kuliko kwanjia nyingine hivyo wewe kama kiongozi unapaswa kuwa mtu wa mfano katika kazi zako/biashara yako, kama unakemee uvivu basi hakikishe wewe siyo mvivu kama unataka wafanyakazi/wale unaowaongoza wawe na nidhamu bora hakikisha nawewe unakuwa na nidhamu bora, kama unataka wale unaowaongoza wawe wanajituma sana basi na wewe jitume sana, kama unataka wale unaowaongoza wawe waadilifu basi hakikisha wewe nimwadilifu hivyo kweli kila unachokihitaji wale unaowaongoza wakifanye basi hakikisha wewe unakuwa wakwanza kukifanya kwa kufanya hivyo utafanikiw sana kwenye uongozi wako na maisha yako ya uongozi yatakuwa bora sana.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243
0656918243
0621049901
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE NAKALA YA KITABU
NGUVU YA MAARIFA
SOFTCOPY 10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
0 Comments