Katika makala iliyopita niliitambulisha kauli mbiu ya mwaka huu 2021 ni mwaka wa KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA , jambo moja kubwa ninalopenda nikushilikishe wewe rafiki yangu nikuwa kwa mwaka huu 2021 ninajambo moja kubwa ambalo napenda twende wote pamoja, sipendi nikuache kwa mwaka huu naamini tutasafiri pamoja toka sasa hadi mwisho wa mwaka huu.
Jambo moja kubwa ambalo ninatamani tusafiri pamoja mimi na wewe rafiki yangu nikwenye upande wa KUJIFUNZA, KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA, na moja ya eneo ambalo natamani tujifunze pamoja, tutafajari pamoja na tuchukue hatua pamoja basi eneo la kusoma biblia hadi kuimaliza ndani ya miezi sita,
Ooooh! Najua haujanielewa nasema hivi kwamwaka huu 2021 NATAKA TWENDE PAMOJA MIMI NA WEWE KATIKA SAFARI YA KUSOMA BIBLIA HADI KUIMALIZA , Ndio kwakuwa mwaka huu nimwaka wakujifunza sana basi tusafiri pamoja katika kuisoma biblia toka mwanzo hadi mwisho, kwakua huu mwaka 2021 nimwaka wakutafakari basi twende pamoja tukatafari kupitia biblia, kwakua mwaka huu 2021 nimwaka wakuchukua hatua hatua basi tusafiri pamoja tukachukue hatua kwa yale ambayo tutajifunza na kutafakari kupitia biblia naamini na hii ninaimani kubwa sana tunaenda kulitimiza kwa mwaka huu 2021 ndani ya miezi sita pekee.
Ndio nimiezi sita ya kujifunza kupitia Biblia, ni miezi sita yakutafakari Kupitia Biblia na nimiezi sita ya kuchukua hatua kupitia Biblia twende pamoja.
Najua unajiuliza kwanini miezi sita na siyo miaka miwili au mwaka mmoja? Nikweli upo sahihi kwa swali hilo lakini umekuwa miezi sita kwasababu ambayo nimeona inafaa kwakawaida kwakaida Biblia zipo za aina nyingi lakini nyingi zipo za aina mbili kuna zile za vitabu 74 na zile za vitabu 66 sasa ndani ya miezi hii sita tutazama kujifunza, kutafakari na kuchukua hatua kupitia biblia yenye vitabu 66. Nimechagua Biblia hii kwasababu kubwa moja kwamba ni Biblia ambayo inatumika kwa makanisa mengi ya kikristo. Nimejaribu kufuatilia pia biblia nyingi zina kurasa 985 katika agano la kale na kurasa 273 katika agano jipya ukijumlisha vitabu vyote utapata jumla ya kurasa 1258 ukigawanya kwa miezi sita ambayo ni sawa na siku 180, sasa chukua kurasa 1258 gawanya kwa siku 180 utapata 6.98 sawa na kurasa 7 kwa siku hizi zinawezekana kabisa, kusoma, kutafakari na kuchukua hatua.
Twende pamoja rafiki yangu mpendwa katika safari hii nzuri ya kujifunza kupitia Biblia, kutafakari kupitia Biblia na kuchukua hatua kupitia yale tutakayo jifunza.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0621049901
JIPATIE NAKALA YA VITABU
NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
SOFTCOPY 10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
0 Comments