habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema kabisa, naamini pia umefanikiwa kuuanza vyema mwaka huu 2021, naamini pia umeweka malengo makubwa na umezamilia kufanya makubwa kwa mwaka huu, sina shaka na hilo kwako na naamini unaouwezo mkubwa sana wakukamilisha yote uliyoyapanga kufanya kwa mwaka huu.
Ila ninawasiwasi kidogo kwako rafiki yangu mpendwa, wasiwasi huu unatokana na kawaida kuwa huwa unaweka malengo mengi na makubwa mwaka unapoanza lakini malengo hayo huwa hayatimii, lakini pia malanyingine unaweka malengo yanayokosa sifa yakuitwa malengo hii inaweza kuwa kwa kujua au kwakutokujua na mala nyingine huwa unakuwa na mawazo ambayo unadhani kuwa hayo ndio malengo na matokeo yake nikuwa inafika mda unasahau kuwa uliweka malengo gani na maisha yanaendelea kama kawaida na mwaka unakatika na kuanza mwaka mwingine kwa maneno yale yale kuwa mwaka mpya na mambo mapya.
Kutokana na changamoto hii mwaka jana niliandika kitabu kiitwacho *NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA* kwenye sura ya pili niliandika mambo mengi kuhusu kuweka malengo na njia sahihi yakuweka malengo na kuyafikia.
Kwa siku ya leo ninakuja kwako kutambulisha neno kuu lakwenda nalo mwaka huu 2021 nalo sio lingine ni hili JIFUNZE +TAFAKARI+ CHUKUA HATUA =MAFANIKIO
Ndio mwaka huu 2021 sio mwaka wakushanga shangaa kama miaka mingine iliyopita, wa sio mwaka wakuishi kawaida kama miaka mingine iliyopita bali nimwaka wakujifunza sana, tunaenda kujifunza maeneo yote muhimu ya maisha yetu na mimi rafiki yako nakuahidi nitakuwa kiongozi bora kuhakikisha mwaka huu natoa mafundisho mbalimbali kwa kadri Mungu atakavyo nijalia, nawewe rafikia yangu nakusii sana mwaka huu 2021 usipite bila kujifunza sana, usikubali siku yako iishe bila kujifunza, hakikisha kila siku unachukua mda kujifunza mambo mbalimbali kuhusu kila eneo la maisha yetu na kujifunza sio lazima uende shule hapana bali tafuta kitabu soma, tafuta makala yenye kukuelimisha soma, chua biblia soma na vitabu vinginevyo vyote soma, yani hakikisha kwa mwaka huu hauwi kama miaka iliyopita anza kwa kujifunza kila siku, kuna njia mbalimbali za kujifunza kama vile kusoma, kusikiliza, kuangalia na kuona kwa wengine pia kupitia changamoto zako mwenyewe.
TAFAKARI
Baada ya kujifunza kwenye kila eneo la maisha yako hebu chukua mda kutafakari kile ulicho jifunza, kutafakari kunakupa nafasi ya kutathmini juu ya kile ulichojifunza basi kwa mwaka huu nenda katafakari kwa kila kitu unatacho jifunza iwe kupitia kusikiliza basi baada ya kusikiliza nenda katafakari, baada ya kusoma vitabu na makala mbalimbali jipe nafasi yakutafakari, baada ya kupitia changamoto mbalimbali nenda katafakari kwenye kila kitu ulichojifunza kupitia changamoto hizo.
CHUKUA HATUA
Ndio baada kutafakari juu yale usiyojifunza jambo lamwisho unalopaswa kufanya nikuchukua hatua, nenda kachukue hatu kwa mwaka huu 2021 kujifunza pekee hakutakuwa na msaada kwako kama hauta chukua hatua, kutafakari pekee hakutakusaidia chochote bila kuchukua hatua, hivyo kuchukua hatua kwenye kila jambo ambalo utajifunza kwa mwaka huu.
Kwakufanya mambo hayo matatu kwa mwaka huu 2021 nakuhakikishia mwaka huu utakuwa nimwaka watofauti sana na miaka iliyopita, kwa kufanya mambo hayo matutu basi ninauhakika kuwa mwaka huu utaenda kuwa nimwaka wamafanikio nakubwa sana.
Twende pamoja kwa mwaka huu kwa kufanya mambo makubwa matatu ambayo KUJIFUNZA, KUTAFAKARI PAMOJA NA KUCHUKUA HATUA naamini mafanikio yatakuwa sehemu ya maisha yetu.
Ni mimi rafiki yako
FRANK MAPUNDA
www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243
Pia nitafute Facebook kwa jina la frank mapunda au like page ya nguvu ya maarifa (Facebook pamoja na blog ndio itakuwa sehemu kuu ya kuweka masomo kila siku)
JIPATIE NAKALA ZA VITABU
NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
SOFTCOPY =10000
PAMOJA NA
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY =7000/
0 Comments