Habari rafiki yangu mpendwa, nimatuamini yangu kuwa ni mzima wa Afya njema basi sifa na utukufu umludie Mungu.
Bila kupoteza wakati napenda nikushirikishe jambo dogo lakini jambo lenye umuhimu mkubwa sana kwa maisha ya mwanadamu yeyote yule nalo sio lingine bali ni FURAHA. Furaha ni jambo muhimu sana kwa kila mmoja anayeishi hapa duniani lakini changamoto kubwa nikwamba watu wengi wanaishi kwakuosa furaha, najua unajiuli nikwanini unakosa furaha wakati furaha nikitu muhimu sana katika maisha yako?
Basi leo ninajibu fupi sana lakini jibu hili naomba ulitafakari kila siku ndani ya siku therasini kuanzia sasa naamini utaanza kuona furaha ikitawala ndani ya maisha yako.
Najua unajiuliza kwanini siku therasini? Basi jibu nikwamba siku therasini ndio siku ambazo mtu yeyote anao uwezo wakubadili tabia au yeyote na ikabadilika hivyo kwasiku hizo therasini naamini utakuwa na uwezo wakuifanya furaha iwe ndani yako kwasababu utajua njia sahihi yakuwa na furaha mda wote.
Oooh! Nisiwe na maneno mengi bali twende pamoja nikakupe msingi mkuu wa kuwa na furaha ya kudumu maishani mwako. Kabla hatujaenda kuona jinsi ya kuwa na furaha yakudumu maishani mwetu basi twende tukaone sababu kubwa ya kukosa furaha.
HII NDIO SABABU KUU YA KUKOSA FURAHA
~Sababu kubwa kwanini watu wengi wanakosa furaha nikwasababu watu wengi hawaishi maisha yao halisia badala yake wanaigiza maisha. Watu hao ambao wanakosa furaha hawajawahi kujiuliza kipi hasa wanachotaka kwenye maisha yao na kukifanyia kazi badala yake wamekuwa niwatu wanao angalia maisha ya wengine wanataka nini au wanafanya nini na wao kufanya hivyo. Hii ndio sababu kubwa ya watu wengi kukosa furaha maishani mwao.
HII NDIO SIRI YA KUWA NA FURAHA
~Kitu muhimu kufahamu kuhusu furaha nikwamba furaha haitoki inje bali furaha huanzia ndani yamtu hivyo ukitaka kuwa na furaha ya kudumu maishani mwako kitu chakwanza unapaswa kufahamu furaha haitoke nje ya wewe bali furaha inatoka ndani yako, wewe ndiye mwenye dhamana yakumiliki furaha bila kutegemea mazingira ya nje au watu wengine. Iwapo utampa mtu mamlaka ya yakukupa furaha basi tambua umechagua njia ya kukosa furaha yakudumu maishani mwako hii nikwasababu kuwa watu wengi wanatupa wanaweza kutupa furaha ya mda mchache tu lakini baada ya mda tukakosa furaha.
Naomba niishie hapa kwa leo nitaendelea siku nyingine kueleza kwa undani zaidi jinsi ya kuwa na furaha.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU
NGUVU YA MAARIFA
SOFTCOPY 10000/=
TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU
SOFTCOPY 7000/=
0 Comments