Ad Code

Responsive Advertisement

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YAKO


FUNGU KUU:KUMBUKUMBU YA TORATI 4:40

Neno la Mungu linasema " Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele."


Katika sura tunamwona Musa akizungumza na wana wa israeli kanuni Muhimu ya mafanikio katika maisha yao kwamba wanapaswa kuzishika sheria za Mungu na amri zake. sasa tuondoke kidogo katika muktadha wa Biblia na tuje katika maisha yetu ya sasa ambayo tunaishi mimi na wewe.

Mafanikio ni mchakato ambao unaendeshwa na kanuni ambapo kama mtu atazifuata kanuni za mafanikio basi mafanikio yatakuwa upande wake, kuna  kanuni nyingi juu ya mafanikio lakini leo nitazungumza na wewe juu ya kanuni moja kati ya saba ambazo nimezieleza kwa undani zaidi katika kitabu kile cha NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA, Kanuni yakwanza inasema

WEKA AKIBA/JILIPE MWENYEWE KWANZA
Hii nikanuni moja muhimu sana ambayo Ukiifahamu na kuifanya kuwa sehemu ya maisha yako basi maisha yako yatakuwa na mafaniko makubwa sana, kanuni hii inahimiza jambo moja kubwa kwamba kila fedha unayoipata Asilimia kumi unapaswa ujilipe mwenyewe kama sehemu ya mshahara wako baada ya kazi, najua hatujaelewana hapa naomba twende mbele kidogo ili tuelewane vizuri leo hii mimi nimefanya kazi nakulipwa elfu kumi baada ya kumaliza kazi sasa kinachofanyika naichukua elfu kumi naenda kununua chakula cha elfu moja, baada ya hapo nachukua elfu moja nalipa nauli, baada ya hapo nachukua elfu  tano nanunua mahitaji ya nyumbani na baada ya hapo nachukua elfu moja nanunu vocha inabaki elfu mbili nalipa bili ya umeme nakuwa nimemaliza fedha yote. Swali kuna fedha yeyote ambayo mimi nimebaki nayo? Jibu hakuna je dakika chache zilizo pita sikuwa na fedha? Jibu nilikuwa nazo, swali pesa zangu zimeenda wapi? Jibu kwenye matumizi. Nini nataka unielewe hapa? Nikwamba fedha inapofika mikononi tunapaswa kujua siyo yetu na haita kuwa yetu kama hatutachukua hatua ya kujilipa sisi wenyewe kwanza najua unajiuliza kwanini nasema hivyo? Namaanisha kwamba fedha inapoingia mfukoni mwako haiwi yako bali inakuwa ya watu wengine ambao unaenda kuwapa kwaajili ya kukupa kile unachohitaji kama tulivyoona mfano wa matumizi hapo juu, hivyo fedha itakuwa yako hadi uchukue uamuzi wa wewe kujilipa kwanza, Ooooh! Najua bado hatujaelewana vizuri hapa ninachomaanisha nikwamba tuliona nilipata elfu kumi baada ya kupata ile nilienda kulipa kwa watu ili wanipe kile nilichokihitaji na mwisho nikabaki sina kitu kwasababu pesa yote iliisha kwenye matumizi. Hapa sasa naona umenielewa vizuri,  sasa kanuni hii inatuambia kwamba fedha yeyote tunayoipata tunatakiwa kujilipa wenyewe kanza kabla ya kwenda kuwalipa wengine hapa inachotakiwa kufanyika nikuchukua asilimia kumi ya elfu kumi ambayo tunapata elfu moja na kwenda kuiweka kwenye gereza langu na elfu tisa inayobaki ndio natakiwa kuifanyia natumizi (Hapa najua nimekuacha kidogo pale niliposema kuiweka kwenye gereza nilichokuwa namaanisha nikwamba natakiwa kuwa na akaunti ambayo natunza mshahara wangu inaweza kuwa laini au akaunti ya benki huko mbele nitaeleza hili fedha baada ya kuweka nitaifanyia nini, kumbuka hii nifedha kwaajili yangu hivyo sitampa wala kulipia kitu chochote).

Hii kanuni inatakiwa iwe sheri na amri hivyo  inatakiwa ifanywe kwa kila fedha ambayo inaingia mikononi mwangu hapo ndipo palipo na siri ya mafanikio yako. Ngoja nikuchokoze kidogo "toka umeanza kuingiza/kutafuta fedha hadi leo umejilipa mwenyewe kiasi gani? Hadi leo unafedha kiasi gani ambacho umekiweka gerezani? Najua jibu lako hakuna na hii inatokana na wewe kuto kuijua siri hii muhimu maishani mwako hivyo kilichokuwa kinafanyika niwewe kujinyima mshahara kwa miaka yote uliyoishi. Sasa napenda nikuambie sasa Acha kujidhurumu wewe mwenyewe anza sasa kujilipa mshahara wako, kuanzia sasa dhamilia kuishika sheria hii ya kwanza ya mafanikio makubwa na endelea kujifunza sheria zingine saba na mafanikio makubwa yatakuwa upande wako.

Fungu letu kuu linasema " Basi zishikeni sheria zake, na amri zake ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako,  nasiku zako ziwe nyingi katika nchi ilie akupayo BWANA,  Mungu wako." Sasa ukitafakari kwa umakini fungu hili utagundua kuna siri kubwa katika kuzishika sheria na amri ndivyo ilivyo kwenye maisha ulimwengu wa maisha tunayoishi sasa ili ufanikiwe unatakiwa uzijue Sheria saba za mafanikio makubwa na uzishike kwa maana uziishi kama amri ya maisha yako ili upate mafanikio yako na yawatoto wa watoto wako kwa maana wajukuu wako katika nchi hii akupayo Bwana.

Naomba kwa leo niishie kanuni hii ya kwanza kutokana na mda tutaendelea siku nyingine kanuni ya pili na kuendelea.

WITO; nimuhimu sana kuzijua kanuni za mafaniko kwaajili yamafaniko yako na kanuni hizi nimezieleza kwa undani sana kwenye kitabu kiitwacho NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA ili uweze kupata mafanikio makubwa kwaajiri yako na wajukuu zako ili siku zako ziweze kuwa nyingi na zenye furaha na amani katika nchi hii akupayo Bwana.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243


KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU

NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

SOFTCOPY 10000/=

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU

SOFTCOPY 7000/=

WOTE MNAKARIBISHWA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu