Habari rafiki yangu mpenda? Nimatumaini yangu makubwa kwamba umekuwa na siku nzuri huku ukihakikisha unachukua hatua kuhakikisha unafikia ndoto kubwa ulizonazo kama wewe ni mmoja ya watu wa aina hiyo nikupongeze sana kwani mafanikio kwako hayawezi kukosekana.
Kwa heshima ya kipekee sana tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema yake yakipekee sana kwetu kuweza kutupa sisi nafasi ya kuiona siku hii ya leo siyo kwa juhudi zetu wala kwa nguvu zetu bali nineema tu hivyo tuchukue dakika chache kuweza kumshukuru Mungu kwa Neema hii yakipekee sana.
Bila ya kupoteza mda napenda sasa twende moja kwa moja kwenye somo la siku hii ya leo na katika siku hii ya leo tutakuwa tunahitimisha masomo yetu yaliyokuwa na kichwa kikuu kilichokuwa kinasema *unahitaji nguvu za aina gani ili kuweza kupata mafanikio makubwa* nimatumaini yangu kuwa umepata nafasi ya kujifunza mengi muhimu katika mfululizo wa masomo haya, leo katika kuhitimisha somo hili tutaenda kufanya zoezi la kujibu maswali ambayo yanatoka kwenye masomo ambayo tayari tumejifunza, nikuombe jambo moja rafiki yangu, hakikisha unakuwa na daftari na kalamu ambayo utaitumia kujifanyia tathmini juu ya masomo ambayo tunakuwa tunajifunza ili uweze kuyatumia katika kuleta matokeo maishani mwako, naamini kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa masomo haya na utakuwa mtu wakufanyia kazi mazoezi ambayo nayatoa mwishoni mwa somo husika basi maisha yako hayatabaki kama yalivyo bali yatakuwa bora zaidi. Na bila kupoteza wakati nikupeleke moja kwa moja kwenye zoezi letu la kuhitimisha somo letu.
KAZI YA KUFANYA
1~Unafanya nini kuhakikisha unaondokana na stres kabla ya kufanya kazi?
~Unawasaidia vipi wafanyakazi wako kuondoa stres kabla ya kuanza kazi?
~Je ufanye nini ili uweze kuongeza ufanisi kazini?
~je unafanya mambo gani kuhakikisha unafanya kazi yako kwa furaha na amani?
~je vyakula na vinywaji unavyotumia vinakuongezea ufanisi kwa kiasi gani?
~je unafanya nini kuhakikisha unakuwa na afya njema?
~je unafanya mazoezi ya mwili mala ngapi kwa wiki?
~je unahitaji kula vyakula gani ambavyo vitakufanya uwe na afya njema na kukupa nguvu zaidi ya mwili?
~je unahitaji kunywa maji kuasi gani kwa siku na unafanya nini kuhakikisha unakunywa maji yakutosha kwa siku?
~je unafanya nini kuhakikisha unaboresha nguvu ya kiroho maishani mwako?
Rafiki haya nimwasali muhimu sana kuyajibu kabla hatujaendelea na masomo mengine. Uzuri wa maswali haya yote tumejifunza tayari kwenye masomo yetu haya, hivyo jitahidi kuyajibu maswali haya na fanyia kazi kwa vitendo ili uweze kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa maishani mwako.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
0758918243
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE NAKALA YA VITABU ILI UWEZE KUONGEZA MAARIFA ZAIDI AMBAYO YATAKUPELEKA KWENYE MAFANIKIO MAKUBWA
*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*
SOFTCOPY 10000/=
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
SOFTCOPY 7000/=
ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI
0 Comments