Ad Code

Responsive Advertisement

UNAJITAJI NGUVU ZA AINA GANI ILI KUWEZA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA~SEHEMU YA TATU



Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na zaidi sana unaendelea kuchukua hatua kila siku kuhakikisha unatimiza malengo makubwa uliyo nayo, kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanachukua hatua kila siku basi nakupa hongera sana, tabia ya kuchukua hatua kila siku inakuongezea nafasi kubwa ya wewe kuweza kufanikiwa katika ndoto zako,
kwa nafasi ya kipekee sana tumshukuru Mungu aliye Muumbaji wetu mkuu kwa wema na fadhili zake, kwasababu yeye ndiye aliye tupa kibali mimi nawewe kuweza kuwasiliana tena kwa siku ya leo, siyo kwamba sisi tumetenda wema sana hapana bali nikwaneema tu, Sasa tunapaswa kuitumia nafasi hii ya kipekee sana kuhakikisha tunafanya mambo yaliyo sahihi huku tukichukua hatua kuhakikisha tunaifanya dunia kuwa mahali sahihi pakuishi, hili ndilo jukumu letu namba moja ambalo nikufanya mambo sahihi kwa wakati sahihi natukitegemea matokeo bora sana. Hivyo haupaswi kuipoteza nafasi hii adimu sana ya leo, nenda kafanye yaliyo sahihi kufanywa ili kuleta matokeo yaliyo bora kwa wengine.

Bila kupoteza mda napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha sana wewe rafiki yangu tuweze kuendelea kujifunza nguvu tatu mihimu ambazo tunahitaji kuwa nazo ili tuweze kufikia mafanikio makubwa. Hizi ni ngubu muhimu sana ili tuweze kupata mafanikio, katika masomo yaliyopita tulijifunza nguvu hizo tatu na tukaziona, pia hatukuishia kuzijua tu bali tuliendelea kujifunza jinsi gani tunaweza kuzitumia nguvu hizo kuweza kutupa mafanikio makubwa maishani mwetu,  na leo tunaenda kujifunza *jinsi gani tunaweza kuwa na nguvu kubwa ya akili ambayo itataweza kutuletea ufanisi mkubwa katika maeneo ya kazi* hili nijambo muhimu sana katika kuleta mafanikio kwa mtu yeyote yule, sasa hivi kumekuwa na changamoto kubwa sana katika kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, watu wengi wamekuwa wakiingia kazi bila morali ya kufanya kazi hali inayopelekea ufanyaji wao wa kazi kutokuwa na ufanisi mkubwa,  hali hii inapelekea matokea mabaya ya kazi ambazo zinafanywa na mtu wa aina hii, huenda hata wewe hii hali huwa unakutana nayo pale unapofikiria kufanya kazi kuna hiasia hasi ambazo zinajitokeza mbele yako  kama vile hisia za woga, hisia za hofu,  hisia za wivu, hisia za chuki hizi nibaadhi ya hisia ambazo zinaondoa kabisa ufanisi wa kazi hali inayopelekea kazi kazi ambayo inafanywa na mtu wa namna hii kukosa ubora na matokeo yake huwa mabaya zaidi. Huenda nawewe umeshawahi kukutana na hali hii, au upo kwenye hali hii na unajiuliza ufanye nini kwasababu hisia hizi zinamaliza kabisa nguvu zakuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Kama wewe hii imekuwa moja ya shida yako basi twende pamoja tukachukua hatua ambazo zitaenda kutuondolea hisia mbaya tulizo nazo.

~FANYA TAJUHUDI
Tajuhudi ni mfumo wakisaikolojia ambao inamsaidia mtu kuweza kutuliza akilia na kuondoa hisia mbaya alizonazo katika akili yake.

Katika kuirejesha akili kuwa katika hali yake ya kawaida kuna njia mbalimbali za kufanya tajudi lakini mimi napenda nizungumze nawewe kuhusu aina hii moja ya tajuhudi (meditation).

Hivyo basi ili tuweze kuwa na akili iliyo tulia na kupata nguvu ya akili ambayo itatusaidia sana katika kukamilisha majukumu yetu kwa ukamilifu mzuri tunahitaji kufanya tajuhudi (meditation), sasa katika kujifunza kuhusu tajuhudu (meditation) tutajufunza kwa muundo wa maswali na majibu,  twende pamoja.

TAJUHUDI (MEDITATION) NI NINI?

Tajuhudi (meditation) ni mfumo wakisaikolojia ambao unalengo la kumsaidia mtu kuweza kuituliza akili na kuwa katika hali ya utulivu. Katika hali ya kawaida akili zetu zina mambo mengi  hali inayopelekea kupata msongo kutokana na msongamano wa mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi hivyo kusababisha akili kukosa utulivu. Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha akili kukosa utulivu baadhi ya sababu hizo nikupata taarifa ya mbaya, kuwa na mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa maamuzi ndani ya mda mfupi, uchovu pamoja mtazamo mbaya kuhusu mambo mbalimbali, hali hii inapelekea kupungua kwa nguvu ya akili ambayo ni injini muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu yeyote katika kuhakikisha mambo yanaenda sana, sasa mtu huyu ambeye amekosa utulivu wa akili kutokana na sababu mbalimbali kma nilivyo eleza hapo juu anahitaji kufanya tajuhudi (meditationi) ili kuweza kuirudisha akili yake katika mfumo wa kawaida. Kuna mwalimu wangu mmoja anaitwa docta Amani Makitira anamsemo wake maarufu anasema "akili yetu inaluka luka kama nyani hivyo tunatakiwa tuikamate na kuweza kuituliza" ndio nikweli mtu unapokuwa na msongo au unapokuwa umepokea taarifa mbaya kwakawaida akili yetu huwa inakosa utulivu na kama itashindwa kutulizwa kunahatari kubwa yakusababisha hatari kwa mtu hali itakayopelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Hivyo kufanya tajuhudi ni mbinu pekee ambayo itakusaidia kuweza kuituliza akili yako na kuweza kufanya maamuzi bora yaliyo sahihi.

KWANINI NI MUHIMU SANA KUFANYA TAJUHUDI (MEDITATION)
Kwakawaida kila mwanadamu kwasiku anafanya maamuzi mbalimbali hali inayopelekea akili kuchoka na akili inapochoka kuna hatari kubwa yakufanya maamuzi yasiyo sahihi. Siyo hivyo tu katika maisha ya mwanadamu kuna kuna changamoto nyingi hali inayopelekea akili kukosa utulivu na akili inapokosa utulivu hali inakuwa mbaya zaidi, sasa njia mojawapo ya kuponya akili zetu na kuziweka katika utulivu ulio sahihi nikufanya tajuhudi (meditation).

 Zifuatazo ni baadhi tu ya faida za kufanya tajuhudi (Meditation)
➡kuondoa msongo wa mawazo; ndio unapofana tajuhudi unaituliza akili yako na kupelekea kufanya maamuzi sahihi kwa kila jambo, hali hii inapelekea kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo unatokana na kuwa na msongamano wa maamuzi ambayo hayajafanyiwa kazi.

➡husaidia kuituliza akili; ndio hii nijambo nzuri ambalo linatokea kwa mtu anaye fanya tajuhudi, kwasababu tendo la kufanya tajuhudi nitendo ambalo linaifanya akili yako iweze kuwa katika utulivu  sahihi hali hii itapelekea wewe kufanya maamuzi sahihi na kwawakati sahihi pia akili inapokuwa katika utulivu sahihi inakusaidia sana katika kufanya maamuzi sahihi.

➡husaidia kuongeza umakini; ndio umakini wa mtu unaondoka kutokana na akili yake kukosa utulivu hali inayopelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi, sasa unapofanya tajuhudi na kuituliza akili yako sehemu moja itakusaidia sana kuongeza umakini mkubwa kwenye jambo fulani hii nikutokana na uwezo wako wa kuikama akili isiluke luke kama nyani.

➡Husaida kuponya magonjwa mengi ambayo chanzo chake ni mfumo wa akili; najua siyo ajabu kusikia mtu kupatwa na magonjwa ya akili lakini ukichunguza chanzo utakuja kugundua mtu huyo alikuwa na msongo wa mawazo hali iliyopelekea mtu huyo kupata magonjwa ya akili sasa wanasanya wamegundua kuwa kafanya tajuhudi mtu anaweza kupanya magonjwa hayo.

➡kuondoa mawazo hasi na kuongeza mawazo chanya; ndio unaweza kuondoa mawazo hasi kwakufanya tajuhudi nahapo ndipo unaweza kuingiza mawazo chanya ndani ya akili yako. Mtu huwezi kuwa na mawazo ya aina mbili ndani ya kichwa chako na mala nyingi mawazo hasi ndio yanayotawala katika akili za watu wengi sasa njia mojawapo yakuondoa mawazo hayo nikufanya tajuhudi (meditation).

➡Husaidia kuupa mwili nguvu; ndio tajuhudi inamsaada mkubwa katika kuupa mwili nguvu ya kanya kazi pamoja na maamuzi bora.

➡husaidia kuongeza ufanisi mkubwa wakazi; ndio hili halina upinzani kabisa unapofanya tajuhudi unakuwa na akili mpya au akili tulivu pia unakuwa na morali ya hali ya juu sana hivyo kupelekea kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

➡husaidia kuweza kuishi maisha ya sasa na siyo ya jana au yakesho.

Hizi ni baadhi tu yafaida za kufanya tajuhudi (meditation) hebu nawewe fanya alafu njoo  na ushuhuda wa jinsi ilivyo kusaidia.

Kwa leo naomba tuishie hapa wakati mwingine nitaeleza kwajinsi gani unaweza kufanya tajuhudi(meditation)

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243


KARIBU UJIPATIE VITABU BORA AMBAVYO VITAKUPA MAARIFA BORA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

KARIBU SANA RAFIKI.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu