Ad Code

Responsive Advertisement

UNAHITAJI NGUVU ZA AINA GANI ILI KUWEZA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA?~ SEHEMU YA NNE



Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza malengo yako makubwa uliyo nayo, hongera sana kwama ni hivyo lakini nina neno moja juu yako rafiki yangu "usikate tamaa pale unapoona haupati matokeo makubwa uliyoyakusudia au unapokutana na changamoto nyingi ambazo zinakufanya urudi nyuma baada ya kusonga mbele, sasa wewe unapokutana na hari yeyote ambayo ipo kinyume namalengo yako basi jifunze kupitia hilo na piga moyo konde endelea mbele,
najua kuna kipindi kigumu sana   ambacho sisi kama wanadamu tunakipitia hasa pale tunapokusudia kufanya mambo makubwa, leo usikubali kurudishwa nyuma na changamoto ya aina yeyote bali jifunze kupitia changamoto hiyo na endelea mbele kwa nguvu, kikubwa epuka kukata tamaa"

Bila kupoteza wakati tuendelee na somo letu ambalo tulilianza jana ambalo lilikuwa na kichwa kikuu kinachohusu *jinsi ya kuwa nguvu kubwa ya akili ambayo itatufanya tuweze kuwa na ufanisi bora kazini/kwenye biashara zetu ili kuweza kupata mafanikio makubwa* na katika siku ya jana tuliona kanuni moja wapo kubwa ya kuwa na nguvu ya kiakili ni kufanya tajuhudi(meditation) hii nikanuni moja kubwa ambayo inahusika kwa kiasi kikubwa sana katika koongeza nguvu ya akili iweze kuwa bora sana. Kwa siku ya jana tuliangalia mambo makubwa mawili moja maana ya tajuhudi pia tuliangalia faida ya kufanya tajuhudi  ni nini? Sasa leo tunaenda kujifunza ni nani anapaswa kufanya tajuhudi, jinsi ya kufanya tajuhudi na mwisho njia sahihi ya kutathmini mwenendo tajuhudi yako karibu sana twende pamoja.

NANI ANAPASWA KUFANYA TAJUHUDI?
Hili niswali muhumu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunaendelea na somo. Nani anapaswa kufanya tajuhudi (meditation)? Jibu nikwamba kila mmoja anapaswa kufanya meditation hii nikutokana na changamoto mbalimbali ambazo tunakutana nazo kila siku kwenye maisha yetu, changamoto hizo ndio zinazopunguza kwa kiasi kikubwa nguvu ya akili katika kufanya kazi na zaidi sana changamoto hizo zinaondoa utulivu wa akili kwa kiasi kikubwa sana, sasa wewe rafiki yangu ili kuongeze nguvu ya akili na utulivu wa akili yako basi kufanya tajuhudi ni njia bora zaidi ya kuongeza utulivu na nguvu yakufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Hivyo mtu yeyote mwenye nia ya kuishi maisha yenye uhuru wa kiakili na maisha bora basi tajuhudi ndio suruhisho ya yote.

NAWEZAJE KUFANYA TAJUHUDI (MEDITATION)

Baada ya utangulizi huo sasa twende kwenye mada kuu nawezaje kufanya Tajuhudi (meditation)? Kuna aina mbalimbali za tajuhudi na lakini mimi leo nitazungumza aina moja ya tajuhudi ambayo nirahisi kufanywa na mtu yeyote. Hizi ni hatua zakufuata ili uweze kufanya tajuhudi kwa mafanikio makubwa.

➡Tafuta eneo tulivu ambalo utapata utulivu mzuri bila ya kusumbuliwa  na kelele zozote au mtu yeyeto, mala nyingi mda mzuri ambao unakuwa tulivu nimda Asubuhi na mapema kuanzia saa kumi hadi saa kumi na moja huu nimda tulivu ambao mtu anakuwa na utulivu mkubwa.

➡kaa katika eneo hilo kwa nafasi/kujiachia hakikisha haujibani wala nguo unazovaa hazipaswi kuwa nguo za kujibana, hivyo kaa kwa uhuru wote.

#Baada ya hatua hizo mbili za maandalizi sasa tunaenda kuanza rasmi zoezi letu la kufanya tajuhudi (meditation)

➡katika eneo ulilokaa unaweza kufunga macho yako au kutazama mbele yote nisawa

➡katika mkao wako huko vuta punzi kuingia ndani kwa nguvu na zitoe kwakutumia mdomo wako kwa nguvu (hapo unapovuta pumzi Mmmh nakutoa Haaaaa!)

➡katika akili yako unapofanya zoezi hili la kuvuta pumzi kwa nguvu nakutoa kwa kwa nguvu ondoa na hisia hasi zilizopo kwenye akili yako na ziachie zitoke hivyo unapovuta pumvi Mmmmh! Kusanya hisia hasi zote kwenye akili yako na unapotoa Haaaa! Ondoa hisia hasi hizo kwenye akili yako.

➡Hakikisha mawazo mengine hayaingilii kwenye zoezi hili na pale yanapojaribu kuingilia wewe jikumbushe kuwa unaondoa hisia chafu na unaingiza hisia nzuri.

➡Ili kuleta ufanisi wa tajuhudi yako (meditation) yako kila unapovuta pumzi hesabu moja unapotoa hesabu mbili hapo unapaswa kuelekeza akili yako kwenye kuhesabu tu, najua inawezekana kipindi unafanya zoezi hili kuna mawazo mengi yatapita kwenye akili yako lakini wewe unayo mamlaka ya kuyakataa na kuendelea  na zoezi lako la kuhesabu hivyo wewe tembea na kuvuta pumvi mmmmh! Hesabu moja na ondoa Haaaa! Hesabu mbili vuta pumvi mmmmh! Moja na ondoa   haaaa! Mbili twende tena mmmmh! Moja na ondoa haaaaa! Mbili twende tena Mmmmmh! Moja ondoa Haaaaa! Mbili. Unaweza kufanya zoezi hili kwa dakika tano hadi saa kulingana na uwezo wako wakufanya tajuhudi,  kwa mwanzo unaweza kuanza na dakika tano lakini kadri siki zinavyozidi kwenda endelea kuongeza dakika moja moja hadi ufikie angalau dakika 20 hadi 30.
➡katika kuleta ufanisi wa zoezi hili unaweza kutega alamu ambayo itakukumbusha mda uliopanga kumaliza kwa mafano siku ya kwanza unapanga kufanya tajuhudi kwa dakika 5 basi tega alamu ikifika dakika tano ikukumbushe,  kila siku unaweza kuongeza dakika moja hadi mbili hadi ufikie lengo la kufanya kwa mda mregu zaidi.

➡Zoezi hili lakufanya tajuhudi  (meditation) ni zuri sana kwasababu baada ya kumaliza kufanya tajuhudi utajiona nimtu mwingine tofauti sasa mimi baada ya kumaliza kufanya Tajuhudi najiona kuna mzigo fulani nimeuondoa kichwani hivyo nakwa na morali ya hali ya juu sana hivyo naweza kufanya mambo yangu kwa utulivu mkubwa sana. Hebu nawewe jaribu alafu njoo nipe majibu.

BAADA YA KUFANYA TAJUHUDI UFANYE NINI?~ WASHIRIKISHE NA WENGINE

Hili niswali zuri sana, katika maisha kuna jamii kubwa ambayo tunashirikiana nayo katika kufanya kazi huenda wewe ni bosi wa ofis fulani hivyo unakutana  na wafanyakazi wako ambao kila mmoja anakuwa ametoka nyumbani akiwa na changoto zake hivyo ili kuwa na ufasi mkubwa wakazi kunahitaji utulivu mkubwa wa kiakili hivyo njia bora ya kuwafanya wafanyakazi wako wawe na nguvu kubwa ya akili iliyojaa utulivu bora nikufanya tajuhudi hivyo nivema kuwashirikisha na nawao waweze kufanya tajuhudi,  sasa hapa unaweza kufanya nao pamoja kwa mda wa dakika tano au zaidi. Kwakufanya zoezi hii litasaidia sana kuongeza ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wako kwasababu watafanya kazi huku akili yao ikiwa na utulivu mkubwa sana. Zoezi hili kama wewe nimwalimu shuleni basi unaweza kulifanya kwa wanafunzi wako hivyo litakuwa na msaada mkubwa sana. Baada ya kufanya zoezi hili watakie kazi njema kama niwafanya kazi wako/wenzako au wanafunzi wako watakie masomo mema. Natamani zoezi hili lifanywe na kila mwanadamu anayeishi katika sayari hii kwasabab nizoezi dogo lakini linanguvu kubwa sana katika kuleta utulivu  wakili na nakuponya magonjwa ya akili.

Mimi ni yule yule rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243

KARIBU UJIPATIE VITABU BORA VYA MAARIFA

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu