Habari rafiki yangu mpendwa katika safari hii kuelekea mafanikio makubwa nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri sana huku ukihakikisha kila siku unachukua hatua ambazo zitakufikisha kwenye ndoto yako, ndio hakina njia yamkato ka habari ya kupata mafanikio bali mafanikio ni matokeo ya hatua sahihi ambazo mtu anazichukua kuelekea kutumiza lengo/ndoto aliyonayo mtu husika. Sasa katika mfululizo wa masomo yetu leo tunaendelea kujifunza somo muhimu sana kuhusu mafananikio ambalo linakichwa kikuu kinachosema unahitaji nguvu ya aina gani ili kuweza kupata mafanikio ndio mafanikio yeyote ambayo mtu anayapata yanatokana na kiwango cha nguvu alichonacho katika kafanya kazi ambayo italeta matokeo bora zaidi katika kazi zake.
Na katika kuhakikisha tunakuwa na nguvu imara katika maisha yetu nguvu ambayo inaenda kutupa morali ya kuendelea kafanyia kazi mipango yetu mikubwa basi mwanzo tulijifunza kwa kina kuhusu nguvu ya akili. Hii ni moja ya nguvu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu ambaye anahitaji kufanikiwa au kuwa na maisha bora sana, natumaini ulipata kujifunza mambo mengi muhimu ambayo kama utakuwa umeyafanyia kazi basi mafanikio yako yatakuwa makubwa sana, sasa leo tunaenda kujifunza aina ya pili ya nguvu ambayo kila msafiri wa kuelekea mafanikio makubwa anahitaji kuwa nayo. Nayo siyo nyingine bali ni nguvu ya mwili.
NGUVU YA MWILI
Mwili wa mwanadamu nikiungo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu huyu, kiungo hiki kinahitaji nguvu iliyo imara katika kuhakikisha mwanadamu anakuwa bora sana katika kazi au mambo mbalimbali ambayo anajihusisha nayo. Sasa katika kuhakikisha mwili huu unazalisha nguvu ambazo zitasaidia kuleta mafanikio makubwa kwa maisha ya mtu husika na jamii anayo ishi nayo au jamii kubwa ya watu ambao wanahitaji huduma kutoka kwa mtu huyo,
Sasa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa ufanisi mkubwa basi mtu husika anahitaji kupa mwili wake vitu ambavyo vitamfanya kuwa na Afya bora ambayo itampelekea kuwa na maamuzi sahihi katika maisha ya mtu husika, sasa katika eneo la mafanikio nikwamba mwanadamu anahitaji nguvu imara ya kimwili ambayo inatokana na kuwa na afya njema ambayo ndio msingi wa mafanikio yawamadamu yeyote. Kuna mambo kadhaa ambayo mtu aliyepanda gari kuelekea mafanikio makubwa anatakiwa kuyafanya ili kulinda afya yake ya mwili inakuwa imala zaidi mambo hayo nikama ifuatavyo.
#Pata mda mzuri wa kulala usingizi; ndio usingizi nikitu muhimu sana katika mwili wa binadamu yeyote, mwili wa binadamu unapopata wasaa mzuri wa kulala usinginzi huwa unapumzika na kukusanya nguvu mpya zakuweza kufanya kazi kwa wakati mwingine. Sasa katika kuhakikisha unakuwa na nguvu imara basi hakikisha unakuwa na mda au masaa kamili ambayo utayatumia kulala, hapa nimuhimu kuwa na mda maalumu wa kulala nikiwa na maana kwamba uwe na mda ambao utautumia kila siku kulala kwamfano wewe kila siku unalala saa nne na kuamka saa kumi na mmoja basi fanya hivyo kila siku hii itaifanya akila yako iweke alamu kwenye mda huo hali itakayopelekea kuwa na uzalishaji mzuri wa nguvu pale unapotoka kulala, katika kuhakikisha unakua na usingizi mzuri na bora kuna vitu unatakiwa kuviepuka kabla ya kwenda kulala baadhi ya vitu hivy nikama vile kutumia vitu vyenye mwanga mkali kama vile simu, computer, tv n.k nusu saa kabla ya kwenda kulala, pia epuka matumizi ya kahawa masaa mawili kabla ya kulala, epuka kufanya mazoezi mda mchache kabla ya kulala, epuka msongo wa mawazo, epuka kula kiwango kikubwa cha chakula kabla ya kwenda kulala, epuka kelele wakati wa kulala. Kwa kuzingatia mambo haya utapata usingizi mzuri ambao unakusaidia wewe kupata nguvu kubwa ya mwili ambao ndio msingi mkuu wa mafanikio ya mwanadamu yeyote katika kufanya kazi, niukweli usiopingika kwamba kama mtu hayupo vizuri kimwili ningumu sana kuweza kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa hivyo nimuhimu sana kuzingatia tunailinda miili yetu na changamoto mbalimbali ambazo zitaenda kuathiri miili yetu. Hukuo mbele nitakuwa na somo maalumu la kilinda afya zetu dhidi ya mangonjwa ambayo yanaenda kuathiri nguvu za mwili usiweze kufanya kazi kwa ufanisi namatokeo yake kuishia kwenye umaskini mkubwa.
Kwa leo naomba tuishie hapa tukutane tena wakati mwingine ambao tutaendelea kujifunza nguvu nyingine ambayo tunahitaji ili kuweza kuwa na mafanikio makubwa.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243
KARIBU UJIPATIE VITABU
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=
ASANTE SANA KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI.
0 Comments