Ad Code

Responsive Advertisement

UNAHITAJI NGUVU ZA AINA GANI ILI UWEZE KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA~SEHEMU YA SITA




Habari rafiki yangu mpenda? Nimatumaini yangu makubwa kwamba umekuwa na siku nzuri huku ukihakikisha unachukua hatua kuhakikisha unafikia ndoto kubwa ulizonazo kama wewe ni mmoja ya watu wa aina hiyo nikupongeze sana kwani mafanikio kwako hayawezi kukosekana
. Kwa heshima ya kipekee sana tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema yake yakipekee sana kwetu kuweza kutupa sisi nafasi ya kuiona siku hii ya leo siyo kwa juhudi zetu wala kwa nguvu zetu bali nineema tu hivyo tuchukue dakika chache kuweza kumshukuru Mungu kwa Neema hii yakipekee sana.

Bila ya kupoteza mda napenda sasa twende moja kwa moja kwenye somo la siku hii ya leo na somo letu la leo linasema *unahitaji nguvu ya kiroho ili uweze kupata mafanikio makubwa*

NGUVU ZA KIROHO

Tunapozungumzia unahitaji nguvu za kiroho ili uweze kuwa na mafanikio makubwa tunamaanisha kuwa unahitaji kujifungamanisha na Mungu wako ambaye ndiye anayekupa nguvu ya kuupata utajiri, nikinukuu kwenye maandiko matakatifu katika kile kitabu cha kumbukumbu la torati 8:17-19 Biblia inasema "17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
18 Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
19 Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka." Mwisho wakunukuu. Hapa tunaona Mungu mwenyewe anajitambulisha kwetu kuwa yeye ndiye anayetupa nguvu ya kuupaa utajiri (mafanikio makubwa tunayoyahitaji), sasa kama ni Mungu anayetupa nguvu ya sisi kuupata utajiri tunahitaji kujifungamanisha kwake ili tuweze kupata hiyo nguvu ambayo itatupa mafanikio makubwa.

Katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na nguvu yakiroho ambayo ndiyo inayotupa Nguvu ya sisi kupata mafaniko makubwa hapa tunahitajika kufanya mambo kadhaa ambayo yatatufanya tuwe na nguvu ya kiroho ambayo ndio nguvu Muhimu katika kutupatia mafanikio makubwa.

1:UNAHITAJIKA KUFANYA IBADA KWA MUNGU;
 Hili ni jambo la muhimu sana kwa kila mtu ambaye anahitaji kukua kiroho kwasababu ibada ndiyo inayotuunganisha na Mungu wetu hivyo swala la ibada ni jambo la muhimu sana na ikiwezekani linapaswa kuwa jambo la kwanza kuliko mambo yote maishani mwako. Ndani ya ibada kuna mambo kadha wa kadha ambayo ndiyo yanayoifanya ibada iwe na maana Mbele za Mungu baadhi ya mambo hayo nikama kusoma Neno la Mungu, kuomba, kumshukuru Mungu, kuomba msamaha pamoja na kutoa shukrani kwa Mungu. Haya nimambo muhimu sana ambayo yatakufanya uwe na nguvu kubwa ya kiroho ambayo itakupa nguvu kubwa yakuweza kupata mafanikio makubwa.

Muhimu:- Hakuna mwanadamu yeyote duniani ambaye amepata mafanikio makubwa bila kuwa na hii nguvu ya kiroho hivyo nivema nawewe kama unahitaji mafanikio makubwa basi hakikisha unakuwa na Nguvu imari ya kiroho ambayo itakufanya kuweza kumiliki utajiri na mafanikio makubwa. Katika eneo hili kuna nguvu kuu mbili ambazo zinaongoza watu kuwa na mafanikio makubwa njia ya kwanza inamwongoza mtu kuwa na mafanikio makubwa lakini niyamda lakini nguvu ya pili inamwongoza mwanadamu kuwa na mafanikio makubwa na yakudumu na iwapo mwanadamu yeyote ambaye atakosa kuwa na nguvu hii ya kiroho basi mafanikio kwake inakuwa nichangamoto kubwa. Na baadhi ya nguvu hizo ni Nguvu za kiroho kutoka kwa Mungu na pili ni nguvu za kiroho kutoka kwa shetani hivyo nikusihii wewe rafiki yangu chagua kuwa na nguvu yakiroho kutoka kwa Mungu ili uweze kupata mafanikio yakudumu.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243


KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUONGEZEA MAARIFA ZAIDI YA KUKUPA MAFANIKIO MAKUBWA

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

SOFT COPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

SOFT COPY 7000/=

KARIBU SANA TUENDELEE KUWA PAMOJA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu