Ad Code

Responsive Advertisement

UNAHITAJI KUWA NA NGUVU ZA AINA GANI ILI KUWEZA KUPATA MAFANIKIO?~ SEHEMU YA PILI




Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako,
kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake,  siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanyua  mguu hata mmoja tu, mimi na wewe nani hadi Mungu ametutetea kiasi hiki hakuna kubwa tulilo litenda  bali ni kwaupendeleo tu,  hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha *nguvu ya maarifa* sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).

Bila ya kupoteza mda nichukue nafasi hii  kukukaribisha sana kwenye mwendelezo wa somo letu muhimu sana kwa habari ya kupata mafanikio makubwa na leo tutaizungumzia jinsi ya kuwa na nguvu ya akili (mtazamo chanya) ambayo ni moja kati ya nguvu muhimu sana katika kuamua mafanikio yamwanadamu yeyote.

Tunapozungumza nguvu ya akili tunamaanisha kuwa na akili yenye kufikiri vitu kwa upande chanya wa kuwezekana bila kujari changamoto au magumu anayopitia mtu katika kufanya jambo fulani, ipo hivi rafiki haiwezekani kwa mtu yeyote kuweza kufanikiwa katika jambo lolote ikiwa ndani ya akili yake kumejaa hisia hasi/ hisia zakutowezekana, ndani yake kumejaa hisia za hofu,  ndani yake kumejaa woga, ndani yake kumejaa hisia mbaya za kushindwa, mawazo ya chuki pamoja na wivu kwa watu wengine walio fanikiwa. Hizi ni baadhi tu ya  hisia mbaya ambazo zinaua nguvu yako ya akili katika kuweza kukupa mafanikio makubwa,  najua unajiuliza unawezaje kuondoa aina hizi za hisia ambazo zinauwa kwa kiasi kikubwa ufanisi wako wa kazi na nguvu yako ya akili ambayo ndio nguvu muhimu sana katika kukupa mafanikio makubwa. Kwenye kitabu cha *nguvu ya maarifa* kuna sura nzima ambayo nimezungumzia kwa habari ya kuwa na mtazamo chanya ambao utakusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupata mafanikio makubwa.

Katika kuhakikisha unaipatia akili yako tiba/nguvu yakufikiri chanya unatakiwa kufanya mambo makubwa mawili . moja nikuondoa mawazo yote mabaya ndani yako kwa kufanya tajuhudi na mbili kubadili aina ya marafiki, kubadili aina ya vitu unavyovitazama, kubadili aina ya vitabu unavyosoma  pamoja na kubadili aina ya marafiki/watu unaoambatana nao  kila siku. Kwakufanya hivyo utaweza kuipa akili yako nguvu muhimu sana ambayo itakusaidoa sana katika kupata mafanikio makubwa. Katika somo lijalo tutaenda kuangalia nikwajinsi gani tunaweza  kuitumia tajuhudi katika kuipa akili zetu nguvu za kufanya mambo makubwa maishani mwetu, usipange kukosa mwendelezo huo.

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu:0758918243/0656918243/0786115129

KWA MAARIFA ZAIDI KARIBU UJIPATIE VITABU AMBAVYO VITAENDA KUKUPA MAARIFA KUHUSU MAFANIKIO

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI NA MUNGU AKUBARIKI SANA.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu