Ad Code

Responsive Advertisement



UMEJIANDAAJE KWAAJIRI YA KUPATA MAFANIKIO?~ SEHEMU YA NNE

Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kwama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana.
Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanya hata mguu mmoja, mimi ni nani hadi Mungu amenitetea hivyo hakuna kubwa nililolitenda bali ni kwaupendeleo tu hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha *nguvu ya maarifa* sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).

Bila ya kupoteza mda nipenda kukukaribisha sana kwenye somo la leo ambalo nimwendelezo wa masomo yaliyotangulia ambalo linauliza *umejiandaaje kwaajiri ya kupata mafanikio?* na katika somo lilopita tuliitimisha kipengele cha nne ambacho kilikuwa kinahusu kufikiri bayana ili kuweza kupata mafanikio makubwa tunayoyahitaji,  sasa leo tunaendelea na jambo la tatu ambalo nimuhimu sana kuwa nalo kwaajiri yakuja kupata mafanikio makubwa tunayoyahitaji,

3~JE UNATAKA KUTOA HISIA GANI?
Hili ni swali muhimu sana katika kujiandaa kupata mafanikio makubwa, nimuhimu sana kujia aina ya hisia ambazo unatakiwa kuzitoa pindi unapoendea mchakato mzima wa mafanikio makubwa. Katika kupata mafanikio kuna hisia mbalimbali ambazo mwanadamu anakuwa nazo sasa wewe kama msafiri wa kuelekea kwenye  mafanikio makubwa je nihisia za aina gani unatapenda kuwa nazo.hapa unatakiwa ujiulize je nikitu gani ambacho kimekuvutia wewe kutaka kupata mafanikio unayoyataka. Unapokuwa na majibu ambayo yanaonesha ainaya hisia unayotaka kuwa nayo pale unapopata mafanikio makubwa basi hisia hizo zitakusukuma zaidi katika kuongeza bidii kubwa ya wewe kupata mafanikio unayoyahitaji. Zifuatazo ni baadhi ya hisia ambazo watu wanakuwa nazo wanapohitaji kupata mafanikio.

~kutaka kuwa na mambo yako kwenyewe ili uweze kuwa na furaha. Hii nisehemu ya hisia ambayo mtu anakuwa anayo anapokuwa katika mchakato wa kupata mafaniko na hata baada ya kupata mafanikio. Unapokuwa na hisia ya namna hii inakusukuma kuweka juhudi kubwa katika kuhakikisha unakuwa na biashara au uwekezaji ambao unakuwa wakwako binafsi, lengo kubwa la kuwa na biashara na uwekezaji wako nikuhakikisha unafanya mambo yako bila ya kusimamiwa na mtu yeyote, hivyo mtu mwenye hisia ya namna hii anakuwa na maandalizi bora sana katika kuhakikisha anapata mafanikio makubwa na kweli anayapata.

~hisia ya kutaka kukua na kuwa bora zaidi kila siku. Hii ni moja ya hisia bora sana ambayo mtu aliye kwenye nafasi ya kupata mafanikio makubwa anakuwa nayo.  Mtu mwenye hisia ya namna hii anakuwa ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana kwasababu kila siku kweke inakuwa nisiku ya kuhakikisha anakuwa bora zaidi haijalishi ameajiriwa au amejiajiri bali yeye kukua na kuendelea kuwa bora zaidi ndio sehemu yake ya maisha,  watu wa namna hii kama wameajiwa basi wanakuwa na ufanisi mkubwa sana kwasababu kufanya kwako vizuri hakutokani na msukumo wa nje bali kunatoka ndani yake hivyo yeye kabla hata hajaambiwa kufanya kwa ubora yeye tayari anakuwa na shauku ya kufanya hivyo, hii haimaanishi kuwa mambo yanakuwa rahisi hapana bali wanakutana na changamoto na magumu mengi lakini kutokana na dhamila kubwa waliyonayo ndani yao ndio inayowafanya waendelee kuweka juhudi kubwa kila siku kuhakikisha wanaendelea kuwa bora zaidi.

~Unataka kuwa na kujiamini zaidi;
Uwezo wa kujiamini unatoka ndani ya mtu mwenyewe  na huu ndio ulio na mchango mkubwa katika kuhakikisha mtu anafanikiwa zaidi kwasababu anakuwa na shauku ya kufanya vizuri ili aweze kuaminika zaidi.

Hizi ni baadhi tu ya hisia ambazo mtu nayetaka kupata mafanikio anakuwa nazo. Kwa leo naomba niishishe hapa nikusihii tu rafiki usikose kuendelea kufuatilia mwendelezo wa masomo haya muhimu sana kwa maisha na mafanikio yako pia unaweza kuwatumia wengine wengi wengi zaidi ili awao waweze kujifunza zaidi.

Ni Mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243

KARIBU UJIPATIE VITABU AMBAZO VITAKUPA MAARIFA BORA ZAIDI KUELEKEA KWENYE MAFANIKIO MAKUBWA

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=


ASANTE SANA KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI, NAKUTAKIA BARAKA ZA MUNGU ZIENDELEE KUWA JUU YAKO.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu