Ad Code

Responsive Advertisement

NATUMIA GHARAMA KUBWA YA CHAKULA CHA KUKU NIFANYAJE?



Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kwama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua tunazochukua hii itatufanya kila siku tusogee karibu zaidi na maono makubwa tuliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake,
siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu,  hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu,  kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanyua hata mguu mmoja, mimi ni nani hadi Mungu amenitetea hivyo hakuna kubwa nililolitenda bali ni kwaupendeleo tu hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua,  kuhakikisha unatumia uwezo wako wote,  kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha nguvu ya maarifa sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).

Bila ya kupoteza mda nipende kukukaribisha sana kwenye somo la leo ambalo lipo kwa muundo wa swali ambalo linauliza natumia gharama kubwa ya chakula cha kuku nifanyaje hili niswali muhimu sana kwa wafugaji, kumekuwa na changamoto kubwa katika chakula chakuku hali inayopelekea bei za chakula kupanda kwa kiasi kikubwa sana huku kuku na mazao yao kama vile mayai  yakiendelea kubaki na bei ile ile hii inawafanya wafugaji wengi washindwe kukua kwasababu hawapati faida kwasababu gharama wanazotumia katika uendeshaji wa kuku kuwa na gharama kubwa hasa kwa upande wa chakula, gharama za chakula zinakuwa juu sana. Nami kwakuliona hilo nimeona nijambo jema sana kukuletea somo ambalo litakuwa suluhisho la changamoto  hiyo ambayo imekuwa kilio cha wafugaji wengi.

Kwanza nikiri kwamba nikweli bei ya chakula imekuwa ikipanda kwa kasi sana  hali inayopelekea ufugaji wa kuku uwe nikati ya uwekezaji ambao unatumia gharama kubwa sana. Hii inatokana na gharama za  uandaaji wa chakula kuwa juu. Hivyo kama waandaaji wachakula cha kuku wanahitaji faida hivyo dhidi gharama za uendeshaji zinapozidi kuwa juu na wao wanazidi kuongeza gharama ya chakula. Sasa changamoto inakuwa kwa wafugaji gharama za chakula zinaongezeka lakini bei za kuku pamoja na mazao kuku hasa mayai   zinabaki pale pale hali inayopelekea wafugaji wengi washindwe kuona faida ya uwekezaji wao, na mala chache faida wanayoipata inakuwa ndogo sana ukilinganisha na matarajio yao. na kama wanapata faida basi faida wanayoipata inakuwa ndogo sana tofauti na uhalisia.

Kama ni hivyo tunapaswa kujiuliza sasa tunafanyaje? Je tuendelee kuumia na gharama hizi au kunanjia yakuweza kupunguza gharama za chakula? Jibu lake nindio kwamba kuna njia bora sana ya kupunguza gharama ya chakula na kuendelea kufanya ufugaji wako ambao utakupa faida. Njia hiyo nikama ifuatavyo.

~TENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE. 
Ndio njia mojawapo ya kupunguza gharama ya chakula nikutengeneza chakula wewe mwenyewe, najua unajiuliza unawezaje kutengeneza chakula wewe mwenyewe? Pia unajiuliza je chakula unachotengeneza kitakuwa na ubora kama kile unachonunua? Bado unamaswali mengi kama  vile nikwajinsi gani utapunguza gharama za chakula cha kuku? Kama maswali yako nihayo basi endelea kuwa pamoja nani. Kutengeneza chakula mwenyewe kunakupa faida kubwa sana katika ufugaji wa kuku, kama vile kutumia gharama ndogo ya fedha kuliko unaponunua chakula ambacho kimeandaliwa tayari kwa malisho,  najua unajiuliza kivipi? Ndio unapunguza gharama ya chakula cha kuku kwasababu unaponunua mchanganyiko na kuja  kutengeneza wewe mwenyewe gharama inakuwa ndogo, ipo hivi rafiki yangu, wale wanaotengeneza chakula chakuku lengo lao kubwa kutengeneza chakula bora napia waweze kupata faida kupitia chakula wanachotengeneza, sasa katika kufanya mchakato wa chakula hadi kinafika dukani kunamichakato kadhaa wanakuwa wanaipitia kama vile kutengeneza chakula, kusafirisha nakwenda kuwauzia wauza maduka, sasa ukiangalia mchakato huu utaona kuna michakato mikubwa mitatu, moja kuengeneza chakula wametumia gharama inabidi wapate faida, mbili wanalipia usafiri hapa inabidi watoe fedha ya usafiri, tatu wanawauzia wauzaji wa mwisho hawa nao wanataka wapate faida, hivyo kama chakula cha kilo hamsini kilitengenezwa kwa elfu thelasini basi lazima waongeze bei ambayo itakuwa sehemu ya faida, pia lazima waongeze fedha ya nauli,  na mwisho yule anayenunua lazima apate faida hivyo nayeye ataongeza bei sasa ukiangalia mchakato huu mwisho utaona gharama inapanda kutoka elfu thelasini hadi elfu arobani na tano hadi hamsini. Sasa wewe unapotengeneza chakula mwenyewe unavunja michakato miwili hivyo nakubaki na mchakato mmoja pekee ambao kununua michanganyiko ya chakula na kuchanganya mwenyewe mwisho kuwapa kuku wako, hapa unakuwa umeepuka gharama nyingi zisozo za lazima. Kwa uzoefu wangu nikwamba chakula ninachotengeneza mwenyewe natumia gharama ndogo kuliko chakula ambacho nanunua dukani ambacho kinakuwa kimesha tengenezwa tayari kwa wastani nakuwa napunguza gharama ya chakula kwa asilimia 30 hadi 45 kulingana na msimu. Hapa ninamaanisha kama chakula cha kilo mia moja kinauzwa laki moja basi mimi ninapotengeneza nakuwa natumia elfu hamsini na tano hadi sabini kulingana na msimu hivyo  nanufaika zaidi na punguzo kubwa la bei ya chakula. Sasa wewe unayesema gharama kubwa ya chakula cha kuku hebu tengeneza mwenyewe na uone matunda yake.  Kwa wanaojua fursa hii ya kutengeneza chakua wenyewe wamekuwa wakinufaika zaidi na ufugaji wao kuliko wale wanaonunua chakula dukani. Najua unajiuliza sasa unawezaje kutengeneza chakula mwenyewe? Swali lako limepata jibu tayari kwenye kitabu kiitwacho *tajirika kwa ufugaji wa kuku* ukurasa wa 78 pia katika ukurasa tena wa 210 hadi 228, nimefundisha kwa kina njia na jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku chenye virutubisho bora kwa gharama ya chini sana kama haujapata nakala ya kitabu chako basi hakikisha unapata sasa.

Kwaleo naomba niishie hapa tutakutana tena wakati ujao

Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243/0786115129

KWA MAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUJIPATIA VITABU VITAKAVYOKUPA MAARIFA ZAIDI



*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE KWA KUELNDELA KUWA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI, MUNGU AKUBARIKI SANA.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu