Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana.
Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanyua mguu hata mmoja tu, mimi na wewe nani hadi Mungu ametutetea kiasi hiki hakuna kubwa tulilo litenda bali ni kwaupendeleo tu, hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha nguvu ya maarifa sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).
Bila ya kupoteza wakati nichukue nafasi hii kukukaribisha sana katika somo la leo ambalo linakichwa kinachosema Kuku wangu wanadonoana na kula mayai nifanyeje? tabia ya kuku kudonoana ni moja ya tabia ya hatari sana kwakuku kwanini hupelekea vifo kwa kuku wengi kama tatizo halitadhibitiwa, tatizo hili haliishii tu kwakuku kudonoana bali huenda mbele zaidi hadi kuku kula mayai yanayotagwa, hali hii inapotokea bandani inaumiza sana kwani husababisha hasara kubwa kwa mfugaji. Huenda na wewe ulishakutana na tatizo hili au upo kwenye tatizo hili kwasasa basi leo tunaenda kujifunza chanzo na jinsi ya kudhibiti tatizo hili kwakuku wako. Mala nyingi tatizo hili linakuwa kubwa kwakuku hasa wanafugwa kwa mfumo wa ndani. Baada ya kuona tatizo sasa twende moja kwa moja tukaona chanzo cha tatizo hili.
Chanzo kikubwa cha kuku kudonoana pamoja na kula mayai ni upungufu wa madini muhimu kwenye chakula chao, hii ni baadhi tu ya sababu lakini nyuma yake kuna sababu zingine ambazo zinapelekea kuku kudonoana kama vile kuku kuwa wengi kwenye banda dogo, kuku kuwa kwenye banda lenye mwanga mkali, kuku kukosa shughuri za kufanya kwenye banda (hapa kuku wanatakiwa kufungiwa bembea ndani ya banda ambalo litawafanya kuwa na shughuri nyingi bandani), kuku kupewa chakula kidogo na mwisho nitabia tu ya asili ya kuku wako. Hizi ndio sababu za kuku kula mayai pamoja na kudonoana, sasa baada ya kuona sababu sasa twende moja kwa moja kwenye suluhisho wa tatizo hili.
Suluhisho la tatizo hili nikama ifuatavyo.
~Hatua ya kanza ambayo unatakiwa kuchukua mala tu ya kubaini kuku wako wanatabia mbaya ya kudonoana na kula mayai ni kuwakata midomo, hii ni hatua muhimu sana kuifanya kwa kuku wenye tabia hizi mbaya za kudonoana pamoja na kula mayai, kwakawaida kuku anapaswa akatwe mdomo anapofika miezi mitatu hadi minne lakini kama wamekuwa na tabia ya kudonoana kabla ya mda huo unapaswa uwakate midomo yao haraka iwezekanavyo.
~ Hatua ya pili unapaswa kuwapunguzia mwanga bandani hii itawasidia sana kushindwa kuona kwa haraka mayia au hata kupata nafasi ya kumdonoa mwingine hii ni hatua muhimu sana kuifanya kwa kuku wako.
~ Hatua ya tatu badili chakula ambacho ulikuwa unawapa bila kujari chakula hicho ulitengeneza mwenyewe au ulinunua, tunafanya hivi kwasababu moja ya sababu ya kuku kudonoana ni kukosa virutubisho muhimu kwenye chakula hivyo hatua ya kubadili chakula inakuwa ni moja ya hatua muhimu sana kuwepo kwa kuku wako, baada ya kubadili chakula hakikisha chakula unachowapa nichakula Chenye virutubisho vyote muhimu hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kutengeneza chakula wewe mwenyewe kwakuzingatia unaweka kila kitu muhimu ndani ya chakula hicho (kwenye kitabu kiitacho tajirika kwa ufugaji wa kuku nimeeleza kwa undani sana kuhusu Kutengeneza chakula bora kwa kuku pia nimekupa formula mbalimbali za kutengeneza chakula hicho).
~hatua ya nne wape kuku wako chakula kulingana na idadi ya kuku uliona, hapa unapswa kuwapa chakula kiwango sahihi kulingana na idadi ya kuku wako, kama hufamu ni kiwango gani unatakiwa kuwapa kuku wako kwa siku basi kuna haja kubwa ya kuwa na kitabu kiitwacho Tajirika kwa ufugaji wa kuku kwenye ukurasa wa 145 nimeeleza kwa undani kipimo sahihi cha chakula ambacho kuku wako wanatakiwa kupewa kulingana na umri wao.
~hatua ya tano, wape kuku wako madini kwenye chakula pamoja na maji ya kunywa madini hayo yanaitwa DCP, unaweza kuwapa kijiko kimoja kwenye maji lita mbili pia waongezee chokaa kwenye chakula chao kipimo ni kilo moja ya chokaa changanya kwenye mchanganyiko wa kila tano za chakula. Tumia mfumo huu kwa siku tano na mabadiliko makubwa utayaona kwa kuku wako.
~Hatua ya sita;wape kuku wako mboga za majani kama vile chainizi, mchicha, hydroponic fodder, pamoja na Azolla.
~Hatua ya saba; waweke idadi sahihi ya kuku kwenye banda lao, hapa hakikisha kuku hawalundikani kwenye eneo dogo. Kwenye kitabu kile kile kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku kuna sura nzima ambayo nimefundisha ujenzi wa banda na kipimo cha banda kilingana na idadi yako ya kuku.
Ooooh! Rafiki kuna mengi Muhimu yakufanya katika eneo hili unaweza kujifunza zaidi kwenye kitabu hasa katika sura ile ya sita nimefundisha kwaundani sana somo hili hebu jipatie nakala yako uweze kunufaika na maarifa haya.
Nimimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243/0786115129
PIA UNAWEZA KUJIPATIA VITABU AMBAVYO VITAKUPA MAARIFA BORA ZAIDI
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=
*NGUVU YA MAARIFA*
SOFTCOPY 15000/=
HARDCOPY 10000/=
ASANTE KWA KUENDELEA KUWA PAMOJA NAMI, NAKUTAKIA BARAKA ZA MUNGU ZIWE PAMOJA NAWE.
0 Comments