Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana
. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanyua mguu hata mmoja tu, mimi na wewe nani hadi Mungu ametutetea kiasi hiki hakuna kubwa tulilo litenda bali ni kwaupendeleo tu, hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha nguvu ya maarifa sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani.
Bila kupoteza mda twende moja kwa moja kwenye somo letu la leo ambalo lipo katika mfumo wa swali linauliza ni nisifa zipi zinatumika katika kuchagua aina ya kuku wa kuwafuga hili niswali muhimu sana la kujiuliza kabla ya kufanya maamuzi ya kuku gani ufuge. Ipo kawaida kuwa katika kufanya maamuzi bora ya kuchagua kitu chochote nimuhimu kuwa makini ili kuweza kufanya chaguzi iliyo bora, hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa ufugaji wa kuku kunahitaji umakini mkubwa katika kufanya maamuzi sahihi ya kuku gani ufuge, hili linatokana na kuwa na aina mbalimbali za kuku lakini aina hizi zinatofautiana na matumizi. Kwenye kitabu kuna sura nzima ambazo nimefundisha aina zote za kuku faida na hasara zake. Jambo la muhimu sana katika kufanya chaguzi sahihi ya aina gani ya kuku unaotakiwa kufuga nikuangalia jua sifa za kuku wote waliopo na kuangalia mahitaji ya soko katika eneo lako. Ipo hivi siyo kila kuku anafaa kufugwa kila eneo hapana bali mahitaji ya soko ndio yanayoamua kuku gani afugwe katika eneo gani, iwapo utakosa kujua jambo hili muhimu nirahisi sana kuingia kwenye ufugaji na kupata hasara ambayo itakurudisha nyuma kwa namna moja ama nyingine. Sasa nini kifanyike ili kuzuia aina hizi za hasara?
Leo nitakupa aina chache za kuku na jinsi ya kufanya maamuzi kulingana na soko. Katika ufugaji wa kuku nimuhimu kujua kwamba kuna aina nyingi za kuku ambao wanafugwa hapa nchini lakini siyo kwamba kila kuku anafaa kufugwa na kila mtu, kwa kulifahamu hili basi utakuwa na uwezo mkubwa wa kuepuka au kupunguza kupata hasara. Kitu muhimu katika kuchagua aina hizi za kuku ni kuangalia mahitaji ya soko kabla ya kuingia kufuga aina hiyo yakuku, iwapo utajua aina hizi za kuku na kufahamu kuwa kuku hawa wanasifa gani kubwa basi utafanya maamuzi sahihi katika kuchagua aina ya kuku kufuga.
Muhimu:
Katika kufanya maamuzi ya aina gani ya kuku ufuge epuka kufuata mkumbo bali chukua hatua ya kufanya tafiti kabla ya kuingia kwenye aina hiyo ya kuku, hili nijambo la muhimu sana na kama utafanya tafiti kabla ya kuingia katika ufugaji basi maamuzi utakayoyachukua yatakuwa bora sana.
Hapa chini nimeeleza kwa uchache sana aina za kuku karibu tuendelee kujifunza.
~Aina ya kwanza ambayo napenda tuizungumzie sasa nikuku wa asili au kuku wakienyeji kama wengi tulivyozoea kumwita, kuku huyu amekuwa akifugwa katika maeneo mengi hapa nchini, sifa kubwa ya kuku huyu nikuwa na nyama yenye radha nzuri sana, lakini pia kwa upande wa ufugaji nikuku ambaye anauwezo mkubwa wa kujitafutia yeye mwenyewe chakula lakini kwa manufaa ya ufugaji wako ili uweze kuwa na manufaa makubwa basi nimuhimu kuwapa chakula cha ziada kwa kufanya hivi utaongeza kasi ya ukuaji na uzarishaji wa mayai kwa kuku wako, kila kilicho na uzuri hakikosi kuwa nachangamoto ndivyo ilivyo kwa kuku hawa, changamoto kubwa walio nayo kuku hawa nikuwa na maumbo madogo lakini pia kuwa na uzarishaji mdogo sana wa mayai kwa mwaka, kwa kawaida kuku wa asili kwa mwaka anataga kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka mzima. Hivyo kama mfugaji unapotaka kufanya ufugaji nimuhimu kujua sifa na changamoto za kuku hao.
Aina ya pili nikuku wa mayia, hawa ni aina ya kuku wakisasa ambao sifa yao kubwa nikuwa na uwezo mkubwa wakutaga mayai mengi kwa kawaida hutaga mayai kuanzia 250 hadi 300 kwa kuku mmoja kwa mda wa mwaka mzima pia wanawahi sana kuanza kutaga tofauti na kuku waasili kwani hawa huanza kutaga kati ya umri wa miezi minne na nusu hadi sita wakati kuku wa asili huanza kutaga akiwa na umri kuanzia miezi sita hadi kumi na mbili. Licha ya faida kubwa ya kuku hawa bado wanachangamoto zake kwani wanahitaji umakini mkubwa katika kuwatunza ikiwa nipamoja na kuwapa chakula bora, iwapo kuku wako watakosa chakula bora basi tegemea matokeo mabaya kwa kuku wako ikiwa nipamoja ya kuku kushindwa kutaga pamoja na kuku kuugua mala kwa mala. Uzuri wa kuku hawa katika soko nikuwa na umbo kubwa la yai pamoja na kuwa na watumiaji wengi wa mayai yao hili linawafanya kuku hawa kupendwa na wengi.
Aina ya tatu ya kuku ni kuku wanyama, hawa ni aina ya kuku ambao hufugwa kwa mda mfupi sana hadi kuweza kukua na kuliwa kwa wastani huchukua mda wa wiki nne hadi sita kuweza kuingia sokoni, kuku hawa wamekuwa wakipendwa sana na watu wengi hasa watu wa kipato kidogo na chakati kutokana na bei yake kuwa chini ukilinganisha na kuku wa asili pamoja na kuku chotara, Licha kuwa kuwa na faida kuku hawa pia wanachangamoto zake kama vile kuhitaji umakini mkubwa sana katika kuwatunza iwapo utawakosea kidogo basi nirahisi sana kupata hasara kubwa kutokana na kuku kudumaa hivyo kushindwa kukua vizuri. Pia unapowafuga kuku hawa unatakiwa kutafuta soko mapema kwa sababu kwa kadri wanavyoendelea kukua gharama ya chakula inaongezeka na bei inabaki pale pale. Hivyo unapofuga kuku hawa kuwa makini nao sana hasa katika ulishaji pia tafuta wateja mapema.
Aina ya nne ni kuku chotara, sifa kuu ya kuku hawa ni kukua kwa haraka na kuwa na maumbo makubwa kuliko aina yeyote ya kuku, katika kundi la kuku hawa kuna makundi manne ya kuku chotara namakundi haya yanatambulika kulingana na sifa kuu za kuku hao kama vile chotara aina ya saso hawa ni aina ya kuku chotara kwaajiri ya nyama tunasema chotara kwaajiri ya nyama kwasababu ya sifa yao kubwa ya kuku hawa nikuwa na maumbo makubwa pia kukua kwa haraka, changamoto kubwa ya kuku hawa nikuwa na uzarishaji mdogo wa mayai kuliko kuku wengine chotara japo nikuwa ukilinganisha na kuku wa Asili kuku hawa wanakuwana utagaji mzuri tofauti na kuku asili.
Aina nyingine ya kuku chotara ni kuku aina ya malawi, kuku hawa wanatambulika kwa rangi yao nyeusi na sifa yao kubwa nikuwa na uzalishaji mkubwa wa mayai kuliko aina yeyote ya kuku chotara lakini changamoto yake kubwa nikuwa nyama yao haina radha nzuri pia haifai kwa baadhi ya matumizi kama vile matumizi ya supu.
Aina nyingine ya kuku chotara ni kenbro kuku hawa nimaarufu sana katika mkoa wa mbeya na sifa kuu kuku hawa nikuwa na maumbo makubwa vile kuwa na uzalishaji mkubwa wa mayai lakini pia kuku hawa changamoto yao kubwa nikuwa na mda mfupi wa utagaji kwa lugha ya ufugaji tunasema hawakawii kuzeeka kutokana namaumbo yao kuwa makubwa.
Aina ya mwisho ya kuku chotara ni kroila, sifa kuu ya kuku hawa ni kuw na uwezo mkubwa wa utagaji huku pia wakiwa na uwezo wa kutaga kwa mda mrefu hivyo kwa lugha ya ufugaji tunasema kuku hawa wanachelewa kuzeeka, licha ya kuwa na sifa nzuri bado changamoto haziwezi kukosekana basi changamoto yao kubwa ni kupasukia mayai tumboni pale wanapokuwa wamezeeka au kuwa na umri mkubwa.
Kwa leo naomba tuishie hapa naamini umejifunza mengi kwa undani zaidi unaweza kupata kitabu kiitwacho tajirika kwa ufigaji wa kuku katika ukurasa wa 42 nimeeleza kwa kina aina zote za kuku hawa na sifa zao na madhaifu haya.
Nimimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0786115129/0656918243
KWA MAARIFA ZAIDI JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUPA MAARIFA ZAIDI
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFYCOPY 7000/=
0 Comments