Ad Code

Responsive Advertisement

UMEJIANDAAJE KWAAJIRI YA KUPATA MAFANIKIO? ~SEHEMU YA MWISHO




Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana.
Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanyua  mguu hata mmoja tu, mimi na wewe nani hadi Mungu ametutetea kiasi hiki hakuna kubwa tulilo litenda  bali ni kwaupendeleo tu,  hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha nguvu ya maarifa katika sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).

Bila ya kupoteza mda nipenda kukukaribisha sana kwenye somo la leo ambalo nihitimisho wa mfululizo wa masomo yetu ambayo yalikuwa nakichwa kikuu kinachosema umejiandaaje kwaajiri ya kupata mafanikio makubwa? naamini katika mfulilizo wa masomo haya ulipata nafasi nzuri ya kujifunza nakufanyia kazi maarifa hayo ambayo yalikuwa yanakupa utangulizi muhimu kuhusu mafanikio, naamini kuanzia sasa tayari umeanza kuishi kwa malengo kwasababu moja ya maandalizi muhimu katika kupata mafanikio nikuwa na malengo makubwa ambayo kama utayafanyia kazi basi maisha yako hayabaki kama yalivyo, pia naamini kuanzia sasa tayari umejua nikipaji au taaluma gani unatakiwa kuwa nayo ambayo itakuwa kama nguzo ya kukupa wewe mafanikio, hili nijambo muhimu sana ambalo tulipata kujifunza kwa kina katika masomo yaliyopita, sasa leo nimekuletea maswali ya kujitathmini au zoezi la kufanya kabla hatujaendelea na masomo mengine, nimuhimu sana kufanya mazoezi haya ili kuweza kuwa na manufaa makubwa na masomo haya na pele ambapo utakosa majibu ya maswali haya ujue kuwa kuna mahali haukuelewa vizuri somo ambalo nilifundisha hivyo usisite kunitafuta na nakuniuliza swali nami nipo kwaajiri yako nitakusaidia, siyo hivyo tu maswali haya yanakupa nafasi nzuri sana ya kujiandaa vyema kwaajiri ya kupata mafanikio makubwa hivyo kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanapenda kupata mafanikio makubwa basi nimuhimu sana kujibu maswali haya. Ngoja niongeze kidogo hapa, maswali haya haunijibu mimi bali unajijibu wewe mwenyewe yaani unajibu kwa faida yako na siyo kwafaida ya mtu mwingine hivyo kuwa nadhana mbili ambazo ni  notebook na kalamu ambayo itakusaidia kuandika majibu sahihi ya maswali yako na majibu ya maswali hayo yafanyie kazi naamini kwakufanya hivyo maisha yako hayatabaki kama yalivyo.

ZEOZI LA KUFANYA.
~je malengo yako makubwa katika maisha yako ni yapi? Andika malengo yako makubwa ya maisha yako na yagawe katika makundi mbalimbali kama vile malengo ya miaka hamsini, malengo ya miaka arobaini, malengo ya miaka therasini, malengo ya miaka ishirini, malengo ya miaka kumi, malengo ya miaka mitano, malengo ya mwaka mmoja, malengo ya miezi sita, malengo ya miezi mitatu, malengo ya mwezi mmoja, malengo ya wiki moja na malengo ya siku moja. Malengo ya mda mrefu ndio yanagawanywa katika malengo ya mda mfupi, kwamfano malengo yangu makubwa ni kufuga kuku laki tano ndani ya miaka ishirini, sasa hapa natakiwa kupunguza lengo langu kwa miaka kumi nataka  niwe na kuku laki moja, siishia hapo nagawa tena baada ya miaka mitano nataka niwe nakuku elfu hamsini, bado natakiwa kugawa lengo langu kwa kipindi cha miaka mitatu hapo nasema nataka niwe nakuku elfu ishirini, siishii hapo nagawa tena baada ya mwaka mmoja kutoka sasa natakiwa kuwa nakuku elfu kumi, bado naendelea kuligawa lengo langu kwamba kila mwezi natakiwa niongeze kuku mia tisa. Sasa unapokuwa na lengo la aina hii hupati nafasi ya kusahau lengo lako kuu kwasababu kila siku unajukumu la kulifanyia kazi lengo lako kuu la maisha yako, hivi ndivyo wanavyofanya watu wenye mafanikio makubwa unaowaona leo, hata kwako inawezekana chukua hatua sasa. Kumbuka kila siku nimuhimu kujikumbusha kwa kuandika kwenye notebook yako malengo/ lengo kuu la maisha yako na rudia kuligawa kwa vipindi hadi kupata jukumu la siku, unapofanya hivyo unaikumbusha akili yako na kuilazimisha ichukue hatua ili kuweza kutimiza malengo yako, hivyo kuanzia sasa hili litakuwa ndio zoezi lako la kufanya kila siku unapoamka, nimuhimu sana kupanga malengo yako kabla ya siku yakutimiza lengo haijafika hii inakupa nafasi ya kujipanga vizuri kabla yakufanyia kazi lengo lako, kwamfano leo ndio siku nzuri ya kupanga malengo kwaajiri ya kesho hivyo jenga tabia ya kupanga malengo kabla ya wakati wakutimiza lengo lako haujafika.

~sifa zipi unatakiwa kuwa nazo ili uweze kufikia malengo yako? Hapa unatakiwa kuandika tabia ambazo unatakiwa kuwa nazo ambazo zitakufanya wewe uweze kutimiza malengo yako. Huenda unatakiwa kuwa kuamka kila siku, au kusoma vitabu ambavyo vinaendana na lamalengo yako, au kuweka akiba kila siku, au kuwa na mahusiano bora na jamii au kuwakaribu na Mungu, huenda kuwa na afya bora, huenda kuacha mambo yasiyofaa, huenda kuacha kulalamika na badala yake kuchukua hatua, huenda kuwana juhudi kubwa,  mambo haya yote unatakiwa kuyafahamu kabla kuendea mafanikio ndio maana kichwa kikuu cha somo kiliitwa kujiaandaa kwaajiri ya kupata mafaniko makubwa.

~Je unatakiwa kuwa na kipaji/taaluma gani iliwe uweze kupata mafanikio? Hapa unahitaj kujua vipaji au taaluma ambayo unatakiwa kuijenga ambayo itakusaidia kupata mafanikio makubwa, nimuhimu kujua taaluma/kipaji hicho na kukifanyia kazi sasa.

~Je unataka kutoa huduma gani/ yanamna gani kwa watu?  Hapa unatakiwa kujua aina ya huduma ambayo unatakiwa kuitoa kwa jamii na njia ambayo utaitumia kuitoa hiyo huduma kwa jamii ni ipi? Kwakuwa na majibu haya kunakuandaa vizuri sana kwaajiri ya kuja kupata mafanikio makubwa kwasababu aina ya huduma utakayoitoa itawafanya wateja waje kwako zaidi.

~Unathamini kitugani katika maisha yako? Andika nini unathamini maisha mwako.

~Je unataka kutoa hisia gani kwa jamii? Andika hisia ambazo unataka kuziachilia kwa jamii, likitajwa jina lako jamii yako ione/ifikiri kitu gani?

Haya ndio maswali ya kujitathmini/zoezi la kutanya kabla ya kuendela na masomo yetu, nimuhimu sana rafiki yangu usiwe na haraka ya kuendelea na masomo mengine kabla ya kuelewa vizuri hapa  pamoja na kufanya zoezi hili.

Siyo mwingine ni yule yule anayejali mafanikio yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
0758918243/0656918243/0786115129

KWAMAARIFA ZAIDI KARIBU  UJIPATIE VITABU
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI,  BARAKA ZA MUNGU ZIWE PAMOJA NAWE NAKUTAKIA MAISHA BORA.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu