Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kwama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unazochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako,
kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana. Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanya hata mguu mmoja, mimi ni nani hadi Mungu amenitetea hivyo hakuna kubwa nililolitenda bali ni kwaupendeleo tu hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha *nguvu ya maarifa* sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).
Bila ya kupoteza mda nipenda kukukaribisha sana kwenye somo la leo ambalo nimwendelezo wa masomo yaliyotangulia ambalo linauliza *umejiandaaje kwaajiri ya kupata mafanikio?* Katika somo hili toka sehemu ya kwanza hadi sasa tumejifunza maandaalizi muhimu sana ambayo kama msafiri wa kuelekea mafanikio makubwa unatakiwa kuyafanya ili kuweza kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji na leo tunaenda kumalizia somo hili ambalo tumedumu nalo kwa siku kadhaa tukijifunza maandaalizi muhimu kwaajiri ya kupata mafanikio.
4~UNATHAMINI NINI KATIKA MAISHA YAKO.
Kujua kitu gani unachothamini katika maisha yako nihatua mojawapo kubwa ambayo inaenda kukusaidia sana kuweza kupata mafanikio mkubwa. Moja ya jambo muhimu sana ni kujua nini unachothamini katika maisha yako ili uweze kukipa kipaombele katika maisha yako, kwakufanya hivyo itakusaidia sana katika mchakato mzima wa wewe kupata mafanikio makubwa. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambao watu wanaojiandaa kupata mafanikio wanathamini sana hivyo kuweka kipaombele chao katika kuhakikisha wanafanyia kazi kitu hicho.
~je unathamini pesa?
Ndio katika mchakato wa kupata mafanikio kuna watu kitu kikubwa ambacho kinawafanya wahitaji mafanikio kwako ni pesa hivyo juhudi na nguvu zao zinawekwa katika kuzalisha fedha zaidi. Hili linakuwa jambo zuri nakweli fedha wanazipata lakini je fedha ndio kila kitu? Hapana fedha siyo kila kitu lakini je nimakosa kuithamini sana fedha katika maisha? Mimi sikupi jibu tafakari ni jipe majibu sahihi kwako.
~Je unathamini mchakato wakutengeneza fedha?
Ndio mchakato mzima wa kutengeneza fedha ndio unaowafanya watu wafanikiwe sana kwasababu fedha ni matokeo ya mchakato wa kuzalisha thamani? Je wewe unaudhamini huo mchakato? Sawa jibu unalo wewe lakini muhimu nikwamba kuwa nakitu ambacho unakithamini katika maisha yako kitu hicho ndicho kitakachokufanya wewe uwe mtu wa aina gani? Unapomwana mtu yeyote mwenye mafanikio yeyote ujue kunakitu ambacho anakithamini ndicho kilichompa mafanikio makubwa aliyo nayo na kinaendelea kumpa mafanikio makubwa.
~je unadhamini mafanikio ya watu wengine?
Ndio unapoona watu wengine wanafanikio wewe unajisikiaje au unafanya juhudi gani kuhakikisha watu wengine wanafanikiwa? Mimi sijui kwako nini unathamini lakini ninachofahamu nikwamba watu wengi waliofanikiwa na kuwa na mafanikio makubwa ni matokeo ya kuzalisha thamani bora ambazo zimekuwa na msaada kwa watu wengine kwamaana nyingine nikwamba wamekuwa sababu ya mafanikio kwa wengine ndio maana na wao wamefanikiwa, kwani hadi hapo bado haujanielewa? Ngoja twende mbele kidogo mtu aliyegundua na kutengeneza viatu aliangalia mafanikio ya mtu ambaye anatembea bila viatu hivyo akaamua kutengeza viatu kama sehemu yakumthamini mtu huyo na kwamtu ambaye alinunua kiatu hicho yeye kuvaa hicho kiatu ni sehemu ya mafaniko kwake, sasa wewe hapo bado hujaona jinsi mtu huyu aliyetengeneza viatu alivyo kuwa anathamini mafanikio ya watu wengine katika kuvaa viatu? Ooooh! Mimi sijui wewe unathamini nini ila ninachojua nikuwa kitu unachothamini kinamchango mkubwa wakukupa mafanikio makubwa au kukunyima hayo mafanikio.
~je unathamini ubora wa maisha ya wengine?
Ndio kuna watu wanathamini sana ubora wa maisha ya watu wengine na kupitia hili maisha ya wao wenyewe yamekuwa bora sana na kwakupitia wengine maisha ya mtu huyo nayo yamekuwa bora sana. Hawa ni wale ambao kila siku wanafikiria kuzalisha bidhaa au kitu bora zaidi ambacho kitakuwa na msaada mkubwa kwa wengine. Je wewe huoni kwamba kuna makampuni mengi sasahivi kila siku wanabuni magari bora zaidi? Au hauoni kuwa kila siku vitu vingi vinakuja vikiwa na ubora tofauti na jana? Mimi sijui kwako unathamini nini lakini ninachojua nikwamba watu wanaofanikiwa sana kwasasa niwatu ambao wanathamini ubora wa maisha ya watu wengine ndio maana kila siku wanafikiria kuja na vitu bora zaidi ambavyo vitakuwa na msaada mkubwa kwa wengine? Sijui wewe kwenye biashara/kazi yako unathamini nini lakini ninachofahamu nikuwa wale unaofanya nao biashara wanafanya juhudi kubwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata mafanikio zaidi kupitia kile wanachopata kupitia wao.
~Je unathamini uhuru wa kipato na mda?
Ndio hakuna mtu ambaye hapendi kuwa na uhuru wa kimapato na uhuru na mda kama yupo basi nampa pole, sasa kama hayupo mtu wa namna hiyo inamaana kweli wewe unathamini kitu hicho? Ooooh! Huenda sasa unafanya juhudi gani kuhakikisha unakuwa huru kimapato pia unakuwa huru na mda wako? Mmmh! Bado sijajua kwako lakini ninachofanamu mimi nikuwa ndani ya kitabu cha *nguvu ya maarifa* katika sehemu ya pili ya kitabu hicho mwandishi amefundisha kwa kina nikwanamna gani mtu yeyote anaweza kuwa na uhuru wa kimapato pia na uhuru wa mda mwandishi katika kitabu hicho ameeleza kanuni kuu saba ambaz mtu yeyote anaweza kuzipitia na kuziisha na maisha yake yatakuwa bora sana, sijui kama wewe unalijua hilo? Sawa.
~Je unathamini kuwa na Afya bora?
Oooh! Sijui kama kama kuna mtu apendi kuwa na afya bora lakini je nikweli unathamini afya yako? Je kile unachokula kinaenda kuleta faida gani kwenye mwili wako? Oooh! Katika eneo hili nimajanga makubwa kwa watu wengi je wewe ni mmoja ya watu wengi ambao wamekuwa sehemu ya majanga makubwa? Mimi sijui lakini ninachofahamu mimi nikuwa watu wanaothamini afya zao wanafanya mazoe, wanakula kwa afya vyakula vyenye faida kubwa kwa afya zao, wanaepuka vyakula vyote ambavyo vinaathiri maisha yako. Sasa kwako mimi sijui.
~Je unathamini kuwa na familia bora?
Ndio kuwa na familia bora nihitaji lamsingi sana kwa familia nyingi lakini je wewe familia yako ipo bora? Mimi sijui lakini unafanya juhudi gani kuhakikisha unakuwa na familia bora? Mimi sielewi ujue lakini ninachofahamu nikuwa familia bora ni ile yenye furaha na amani, familia bora ni ile ambayo inapata nafasi ya kuwa wote pamoja kama wanafamilia, familia bora ni familia ambayo wanafamilia wanapata mahitaji yote muhimu, familia bora nifamilia ambayo imejaa furaha, amani na upendo, familia bora nifamilia ambayo imekuwa sehemu yakusababisha mafanikio ya mwanafamilia mwezao anakuwa na mafanikio zaidi, mimi sijui kwako.
Ooooh! Rafiki nilipenda kuendelea kuwa na wewe lakini sasa natakiwa kwenda kuwajibika sehemu nyingine! Oooops! Nisamehe kwa leo naomba niishie hapa tukutane wakati mwingine.
Ni mimi rafiki yako
Frank mapunda
Www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu:0758918243/0656918243/0786115129
UNAWEZA KUJIPATIA VITABU AMBAVYO VITAKUPA MAARIFA ZAIDI KATIKA KUELEKEA KWENYE SAFARI BORA YA MAFANIKIO MAKUBWA
*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=
*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=
ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI, BARAKA ZA MUNGU ZIWE PAMOJA NAWE.
0 Comments