Ad Code

Responsive Advertisement

NIVIFAA GANI MUHIMU VINATAKIWA KUWEKWA NDANI YA BANDA LA KUKU?




Habari rafiki yangu mpendwa? Nimatumaini yangu kuwa unaendelea vizuri kuhakikisha unatimiza ndoto/maono makubwa uliyonayo kwama ni hivyo basi nakupa hongera sana. Jambo la muhimu sana katika kutimiza ndoto/maono makubwa tuliyo nayo nikuchukua hatua kila siku bila kujari ukubwa wa hatua unaochukua hii itakufanya kila siku usogee karibu zaidi na maono makubwa uliyonayo, hivyo napenda nikukumbushe jambo hili mapema sana kwamba leo ndio siku muhimu sana ya wewe kuchukua hatua kuziendea ndoto zako, kwa kufanya hivi maisha yako yatakuwa bora sana.
Kabla ya kuendelea mbele nichukue nafasi hii yakipekee sana kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake, siyo kwa nguvu wala kwa ujanja wetu kuweza kukutana tena mimi nawewe wakati huu kwanjia ya maandishi bali nikwaneema yake tu hii nikutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi walitamani kuandika kama ninavyoandika mimi lakini leo niwagonjwa hawawezi hata kushika simu kuna wengine wengi walitama kuwa na wakati mzuri kama huu kuweza kuchukua hatua kuelekea ndoto zao lakini sasa hawana hata nguvu ya kunyanya hata mguu mmoja, mimi ni nani hadi Mungu amenitetea hivyo hakuna kubwa nililolitenda bali ni kwaupendeleo tu hivyo niwakati sahihi sasa kumshukuru Mungu kwanafasi hii nzuri ya upendeleo ambayo ametupatia siku hii ya leo, kumbuka haujapewa nafasi hii ili ufanye mambo mabaya hapana bali tumepewa nafasi hii ili tuweze kuyafanyia kazi yale makusudi ya sisi kuwepo hapa duniani hivyo tumia nafasi hii ya leo kuhakikisha unachukua hatua kuhakikisha unatumia uwezo wako wote kuhakikisha unafanyia kazi kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani (kama haujui kusudi la wewe kuzaliwa basi jipatie kitabu cha nguvu ya maarifa sura ile ya tatu nimefundisha kwa kina jinsi ya kugundua kusudi la wewe kuwa hapa duniani).

Bila ya kupoteza mda nipenda kukukaribisha sana kwenye somo la leo ambalo tunaendelea kujifunza mambo mbalimbali muhimu katika ufugaji wa kuku na leo ninakuleta somo linalosema nivifaa gani muhimu kuweka ndani ya banda la kuku hili nisoma muhimu sana. Kwanza nisema wazi banda la kuku nilazima liwe bora na ili liitwe banda bora nilazima ndani ya banda kuwe na vifaa muhimu ambavyo vitawasaidia kuku kuweza kuishi maisha mazuri ndani ya banda. Na ili kuweza kukaa vizuri ndani ya banda basi jua kuwa kuna mahitaji muhimu ambay yanatakiwa kuwepo ndani ya banda na yafuatayo ndio mahitaji muhimu kuwa ndani ya banda.

~Vifaa vya chakula; 
Hii ni vifaa muhimu sana kuwep ndani ya banda la kuku, katika eneo hili la vifaa vya chakula kuna vifaa vyenye uwezo wa kuhudumia kuku wa umri mbalimbali kama vile vifaa vyakuhudumia vifatanga na vifaa vyakuhudumia kuku wakubwa, hivyo nivema ukafahamu vyema kwa siyo kila kifaa kinafaa kuwahudimia kuku ila umri ndio unao amua kutumika kwa aina fulani ya vifaa. Najua unaswali je kuna umuhimu wowote wakuwa na vifaa  hivi? Ndio umuhimu nimkubwa sana wakutumia vifaa hivi vya chakula kwa kuku na moja ya faida kubwa ni kupunguza kwa asilimia kubwa upotevu wa chakula,  nahisi haujanielewa bado kwasababu naona bado unaswali ambalo unajiuliza nikwanamna gani nazuia upotevu ya chakula? Upotevu wa chakula nipale kuku wanapokuwa na vifaa ambavyo kuku wanakuwa rahisi kumwaga kile chakula sasa ukiwa na vifaa vya aina hivyo inakuwa nihasara kubwa sana kwa mfugaji kwasababu vyakula vinavyomwagwa chini kuku wanashindwa kula na kuishia kuvichezea hivyo jambo la muhimu kufanya nikuwa na vifaa vya chakula ambavyo haviwezi kumwaga chakula kwa urahisi.

~VIFAA VYA MAJI
Hivi ni vifaa muhimu sana ndani ya banda la kuku, vifaa hivi vinatakiwa kuwa na maji ya kinywa kwa mda wote wa siku nzima ili kuku waweze kunywa maji wakati wowote wanapojisikia kunywa hayo maj. Jambo la muhimu nikuwa unapokuwa na vyombo hivi vyamaji hakikisha kuku hawana uwezo wa kuyachafua na kama watachafua basi tafuta njia ambayo itasidia kuyakinga maji yako kwa njia hiyo, hii itakusaidia sana kupunguza changamoto kubwa ya magonjwa ya matumbo kwakuku ambayo chanzo chake kuku kunjwa maji machafu ambayo yamechafuliwa na kinyesi chake, vyombo hivi vipo madukani

~BEMBEA
Bembea ni kufaa muhimu sana ndani ya banda la kuku hasa kwakuku ambao huwa wanakaa ndani mda mwingi hali inayopelekea kuku kushindwa kutaga vizuri, hivyo njia moja wapo ya kuwapa kuku shughuri yakufanya wanapokuwa wenyewe bandani nikuwapa kuku wako bembea ambayo wataitumia kucheza, bembea inawafanya kuku waweze kuwa na afya njema pia wawe na uzito unaostahili, kuku waliofungiwa bembea bandani wanakuwa nafura uliojaa uchangamfu mzuri hali inayopelekea kuku kuwa nauzalisha mzuri.

~KIOTA;
Kiota nisehemu ambayo inatumiwa na kuku kuweza kutagia, kiota nikifaa muhimu sana kwa kuwepo ndani ya kuku, kuna faida nyingi za kuweka kiota ndani ya banda la kuku wanaotaga kwani husaidia kupaa mayai yaliyo katika ubora pia husaidia kupata mayai ambayo hayana nyufa hivyo kuwa katika ubora wa kutotoresha. ndani ya kitabu kiitwacho *tajirika kwa ufugaji wa kuku* nimefundisha kwa kina jinsi ya vifaa hivi vinavyotumika na mda wa kuwekwa pia nimeeleza jinsi ya kutengeneza vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa.

Ni mimi rafiki yako
FRANK MAPUNDA
www.nguvuyamaarifa.blospot.com
Simu; 0758918243, 0656918243, 0786115129

KWA MAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUJIPATIE NAKALA YA KITABU ILI KUJIFUNZA ZAIDI



*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=


*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

Post a Comment

0 Comments

Close Menu