Ad Code

Responsive Advertisement

NAWEZAJE KUFANYA UFUGAJI WAKUKU WAKATI SINA MTAJI WAKUTOSHA?



Habari rafiki yangu mpendwa sana, nimatumaini yangu umekuwa salama kabisa, bila kusahau kanuni yetu yakuchukua hatua kila siku kuhakikisha tunafikia mafanikio makubwa tunayoyahitaji, ndio nimuhimu kuwa na mafanikio makubwa maishani kwasababu kuzaliwa kwetu hakukuwa kwa bahati mbaya bali nimipango ya Mungu kwamba mimi nawewe tuzaliwe na kuja kufanya mambo makubwa hapa duniani hivyo niwajibu wetu mkuu kuhakikisha tunakuwa na maono makubwa ambayo tunapaswa kuyafanyia kazi kila siku kwakuchukua hatua ndogondogo ambazo zinatuelekeza kwenye mafanikio makubwa, huu ndio msingi mkuu wa mafanikio yeyote nikuchukua hatua kila siku, kuwa kama mjenzi ambaye anamaono makubwa ya kujenga nyumba ya ghorofa kumi lakini anaanza na tofari moja zidi anavyoendelea kuweka tofari moja moja ndio ghorofa linavyozidi kukua hata wewe unaweza kutimiza maono yako makubwa kwa kuanza na kuchukua hatua kidogo kidogo kila siku.



Kwa nafasi ya kipekee sana Tumshukuru Mungu kwa Mema yote aliyotutendea na anayoendelea kututendea, siyo kwa nguvu zetu wala kwa uwezo wetu bali nineema tu ambayo anaendelea kutuoneshea sisi watoto wake hii nikutokana na upendo mkubwa kwetu pia kwasababu kunakusudi kubwa ambalo ameliweka ndani yetu hivyo tunatakiwa tuitumie vizuri nafasi hii kwakufanya yale yaliyo makusudi ya Mungu kutuleta hapa duniani. Bila ya kupoteza mda sasa twende moja kwa moja kwenye somo la leo ambalo linauliza nawezaje kuanza ufugaji wakuku wakati sina mtaji wakutosha?

Kumekuwa na tatizo kubwa kwa watu wengi wenye maono/ndoto ya kufanya ufugaji wa kuku lakini changamoto kubwa imekuwa ni mtaji, wengi wanaishia kusema kuwa mtaji ndio tatizo kubwa la kushindwa kwao kufanya ufugaji wa kuku, huenda nawewe umekuwa na changamoto ya aina hiyo kuwa unatamani sana kufanya ufugaji wa kuku lakini changamoto kubwa imekuwa mtaji (kwenye kitabu kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku katika sura ile ya kumi nimefundisha kwa undani zaidi jinsi ya kuanzia chini hadi mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku). Sasa baada ya kuliona jinsi tatizo hilo lilivyo kubwa basi leo nitakupa maarifa machache lakini muhimu ambayo yatakusaidia kuanza kuifanyia kazi ndoto yako huku ukiwa na mtaji mdogo. Yafuatayo ni mambo yakuzingatia katika kuanza kufanya  ufugaji wa kuku bila ya kuwa na mtaji mkubwa.

1~KUWA NA MALENGO MAKUBWA LAKINI KUBALI KUANZA KWA UDOGO.

Hii nikanuni muhimu sana ambayo nimekuwa nikiitumia kwa mda mrefu na imekuwa ikinipa mafanikio makubwa sana, pia hii ndio kanuni ambayo niliitumia kipindi naanza ufugaji wa kuku. Hivyo hata wewe rafiki yangu ambaye unatamani kufanya ufugaji wa kuku kitu cha kwanza kabisa unahitaji kuweka malengo makubwa juu ya ufugaji wako, (katika masomo yaliyopita nilieleza kwa undani nikwanamna gani unatakiwa kuweka malengo ambayo yana sifa ya kuitwa malengo, baada ya kuweka malengo makubwa kimaandishi unatakiwa kuandika kuyagawa katika makundi madogo madogo ambayo yatakufanya uanze kuchukua hatua mala moja. Na hapa katika kuweka malengo nimuhimu kujua unataka kufuga kuku wa aina gani, na kwanini unataka kufuga kuku wa aina hiyo? Unapojiuliza maswali hayo nakujua aina gani yakuku basi twende hatua ya pili.

2~TAFUTA ENEO LA KUFANYIA UFUGAJI WAKO.

Hili ni hitaji muhimu sana kwa ufugaji wa kuku hauwezi kufanya ufugaji wa kuku bila kuwa na eneo. Sasa hapa kwenye eneo ndipo ilipo changamoto kubwa kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa nashauku kubwa ya kufanya ufugaji wa kuku lakini eneo limekuwa changamoto kubwa( kwenye kitabu kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku ukurasa wa 115-122 nimefundisha kwa undani zaidi jinsi ya kupata eneo la kufanyia ufugaji wa kuku kwa gharama nafuu sana) nikigusia kwa ufupi eneo hili nikwamba unahitaji kupata eneo dogo ambalo litafaa kuweza kulala kuku wako hapa siyo lazima liwe linasakafu ya simenti hapana bali linatakiwa kuwa eneo ambalo litafaa kuku wako kulala tu hivyo linatakiwa liwe safi pia unaweza kufunga bembea ambayo itasaidia kuku wako kulala, kumbuka hii siyo sehemu ya kudumu kwa kuku wako bali nisehemu ya kuanzia tu hivyo utakapokuwa na uwezo basi unatakiwa kujenga banda la viwango ambalo linatakiwa kujengwa kwaajiri ya kuku wako, hivyo kwakuwa hauna mtaji mkubwa basi tafuta kieneo tu kidogo ambacho utatumia kuanza ufugaji wako. Baada ya kuwa na eneo tayari unahitaji kuwenda hatua ya tatu.

3~CHAGUA AINA BORA YA KUKU
Hili ni eneo muhimu sana katika kufanya ufugaji wa kuku kwa mafanikio makubwa, aina ya kuku unayochagua inamchango mkubwa sana katika kukupa mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku, hivyo jambo la Muhimu sana ambalo unatakiwa kulifanya basi nikufanya chaguzi bora ya kuku kwaajiri ya uwekezaji wako, kuku wa kuanza nao niwale ambao wanauwezo wa kustahimili magonjwa lakini pia chagua aina ya kuku ambaye anauwezo mkubwa wa kukua kwa haraka pamoja na uwezo mkubwa wauzalishaji, hapo ndipo utakutana na kuku chotara aina ya kroila (kuna mengi ya kujifunza hapa kiasi ambacho kinahitaji mda kuweza kuelezea, lakini ndani ya kitabu nimeeleza haya kwaundani zaidi)

4~CHAGUA NJIA BORA YAKUZALISHA CHAKULA KWA GHARAMA NDOGO.

Hapa unahitaji kuwa mbunifu kidogo na ukizingatia somo letu linahusu kukosa mtaji mkubwa hivyo kuna njia kadhaa ambazo unaweza kutumia ili kupunguza gharama ya chakula kwa kiasi kikubwa, hivyo yafuatayo ni mambo yakuzingatia ambayo yatakusaidia kupunguza gharama ya chakula kwa kuku.

~WAACHIE KUKU WAKO WATAFUTE CHAKULA WENYEWE

Kwakuwa hauna mtaji mkubwa basi nimuhimu sana kuwaacha kuku waweze kujitafutia chakula wao wenyewe hii itakusaidia sana kupunguza gharama ya chakula kwa kiwango kikubwa, hii siyo ndio njia pekee ambayo unatakiwa uitumie bali unatakiwa kutengeneza chakula nakuwapa kama chakula cha ziada, najua huna mtaji basi chukua pumba changanya na azolla wape kuku wako wale hii itawafanya kuku wako waweze kukua vizuri nakuwa na uzalishaji bora. Pia tengeneza Hydroponic fodder na wape kuku wako wale hii itakusaidia sana kupunguza gharama za chakula kwa kiwango kikubwa hivyo tengeneza chakula hicho na wape kuku wako wale. Pia unaweza kuzalisha wadudu kama vile funza na mchwa chakula hiki kinamanufaa makubwa sana kwa kuku wako. (Haya yote unaweza kujifunza ndani ya kitabu kiitwacho tajirika kwa ufugaji wa kuku jipatie nakala yako ili uweze kunufaika zaidi)

5~ANZA NA ULICHONACHO

Hii ni moja ya kanuni muhimu sana kwa upande wa mafanikio katika ufugaji wa kuku. Hapa unatakiwa uanze na ulicho nacho ili kuweza kupata mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku, kanuni hii nimekuwa nikiieleza mala kwa mala, baada ya kukaa na kusubili mambo ya kae sawa unatakiwa uanze na ulichonacho, (kanuni hii nimeieleza kwa undani zaidi kwenye kitabu katika ukurasa wa 115)

Kwa leo naomba niishie hapa tukutane tena wakati ujao

Ni mimi rafiki yako
FRANK MAPUNDA
E-mail:Nguvuyamaarifa1@gmail.com
Blogs:www.nguvuyamaarifa.blogspot.com
Simu:0758918243;0656918243;0786115129

JIPATIE VITABU AMBAVYO VITAKUONGEZEA MAARIFA ZAIDI KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA



*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA*
HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI TOKA MWANZO HADI MWISHO WA SOMO HILI.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu